Video Information

Utafiti uliofanywa na kundi moja la wachanganuzi kuhusu ulinzi unasema kuwa kundi la wapiganaji la Islamic State limepoteza zaidi ya robo ya eneo ililokuwa ikidhibiti.
Ripoti hiyo inasema kuwa eneo hilo limepungua kwa asilimia 28 tangu kundi hilo lianze kushambulia na kudhibiti maeneo hayo mwaka 2015.Kundi hilo sasa linadaiwa kudhibiti eneo lenye ukubwa wa taifa la Siri-Lanka pekee.
