Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

Sukari yashuka bei

Views:
Video Information

 
Utafiti mdogo uliofanywa na Mwananchi  Dar es Salaam na mikoani unaonyesha kuwa sehemu kubwa, sukari inauzwa kwa wastani wa Sh2400 kutoka zaidi ya Sh3,500 iliyokuwepo miezi miwili iliyopita.
Kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo kunatoa ahueni kwa wananchi wengi waliolazimika kutoboa mifuko yao ili kuimudu bidhaa hiyo muhimu katika uandaaji wa vyakula mbalimbali pamoja na chai.
Hata hivyo, bidhaa hiyo katika maeneo mengi haijashuka kufikia bei elekezi iliyotolewa na Bodi ya Sukari (SBT) ya Sh2,200 kwa kilo.
sehemu kubwa ya maduka ya jijini Dar es Salaam yalikuwa yakiiuza bidhaa hiyo kwa wastani wa Sh2,200.
Wakazi wa Iringa walieleza kuridhishwa na bei ya sukari wakidai imeshuka kutoka Sh3,600 ya awali hadi Sh2,200.
Mkazi wa mji huo, Grace Kyando alisema licha ya kushuka kwa bei ya sukari pia upatikanaji wake kwa mkoa wa Iringa ni wa kuridhisha.
Huko mkoani Manyara, wakazi wa Babati wananunua sukari kati ya Sh2,200 hadi Sh2,500 huku wakieleza kuwa inapatikana kwa wingi tofauti na awali.
Pamoja na bei kushuka kwa kiasi hicho, bado walieleza kuwa haijafikia kiwango cha Sh2,000 iliyokuwa ikitumika awali kabla haijaanza kupaa. Mkazi wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro, Haji Ngokwe alisema hivi sasa sukari ipo kwa wingi kwenye eneo hilo na inauzwa kwa sh2,200 kwa kila kilo moja.
 
 
Similar Videos