Video Information

Mabingwa watetezi wa Ligi ya England Leicester City wameanza msimu wa 2016/17 kwa kuchapwa ugenini na Hull City.
Leicester wamechapwa 2-1, mabao ya Hull yakifungwa na Adama Diomande (46+2') na Robert Snodgrass (55').Bao la kufutia machozi ya Leicester City limefungwa na Riyad Mahrez kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 47.

Matokeo ya mechi zilizochezwa Jumamosi
- Hull 2-1 Leicester
- Burnley 0-1 Swansea
- Crystal Palace 0-1 West Brom
- Everton 1-1 Tottenham
- Middlesbrough 1-1 Stoke
- Southampton 1-1 Watford