Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

Meya Boniface akutana na wanafunzi walioshinda vizuri kidato cha nne (Tanzania One)

Views:
Video Information
MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Kinondoni Boniface Jacob jana tar 29/7/2016 alikutana na wanafunzi walioshinda vizuri mitihani ya kidato cha nne na waliongoza katika michezo mbalimbali.
assa 3
Akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliofika katika hafla hiyo wakiwa na wazazi na walimu wao, Meya Jacob aliwapongeza kwa kushinda vizuri na kuwataka kuendelea hivyo hivyo ili kuweka historia ya kuwa watu muhimu nchini.
assa2
Meya Jacob alisema ili wanafunzi hao waendelee na vipaji vyao, serikali inapaswa kuanzisha taratibu za kuwahudumia wanafunzi hao mpaka mwisho (utotoni hadi uzeeni) ili waweze kuwa hazina ya taifa yaani (property government).
“Serikali yetu ni vizuri ikaiga kwa wenzetu Wamarekani na wengine ambao wanawatunza watu wao wenye vipaji vya mambo mbalimbali ambao baadae sana wanakuwa wagunduzi wa vitu au vifaa todauti” alisema
Meya Jacob alisema kuwa kwa upande wao kama Halmashauri, ni kuwatengenezea mazingira mazuri ya kusomea kwa kutafuta wafadhili wa kuwafundisha shughuli za kitaalam kwa kuwa sasa hazifanyiki.
“Nitoe pia rai kwa wawakilishi bungeni kuusemea mitaala ya kufundishia ambavyo aikidhi kiwango / ina mapungufu ….sasa hivi watu wenye uwezo hakuna kama zamani maana hawajatengenezwa kama zamani. Serikali inapaswa kurejesha mitaala ya zamani ili wawe wenye ujuzi tofauti waende katika shule zao” alisema
Mzazi wa Butogwa aliyeshika nafasi ya Kwanza nchini nzima (Tanzania One 2016) Shijja Msikula alisema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopata mwanae kwani amemlea katika mazingira ya hali ya kawaida.
Mapema akimkaribisha Meya Jacob kutoa tuzo kwa wanafunzi hao, Mwenyekiti wa waratibu wa tuzo za wanafunzi nyota (ASSA) Aron Mbwana (Dj Aron Tanzania) alisema walianzisha tuzo hizo ili kutoa motisha kwa wanafunzi ili waendelee kufanya vizuri.
Chini ni risala ya waandaji wa tuzo hizo.
Karibuni katika utambulisho tunzo za kwanza za wanafunzi bora za Afrika Mashariki, shughuli yenye lengo la kukuza uwezo wa kuifanya vizuri miongoni mwa wadogo zetu walioko mashuleni kwa kipindi kilichopo, ili kujenga uimara na uthabiti wa kifikra na kiutendaji katika kwa kizazi kijacho kitakachoiwakilisha Afrika Ya mashariki. Ndugu zetu, hii ni shughuli iliyotunyima sana usingizi kwa takriban miezi mitano mfululizo, mikwamo ya hapa na pale, tukihangaikia wadhamini na wawezeshaji mbali mbali tuliohisi watatuunga mkono katika nia yetu hii njema, ya kuwapa hamasa vijana wetu lakini hapa ndio tulipofikia, tunawaomba sana, mtuvumilie pale mtakapoona mapungufu, safari hii hatukujiskia kuiahirisha, tulipania kuwaonesha uthubutu na huu ndio uthubutu wetu.
Kabla sijaongea mengi napenda kuchukua wasaa kuwapongeza wanakamati wote waliokosa usingizi kama mimi, kujitahidi kuhangaika huku na kule, kuhakikisha kwamba hili linafanikiwa, wafanyakazi wenzangu wa AllStana pamoja na Bongo 5 Luca Neghesti,Mwalimu Mtanga, Chiku Lweno ambao mpaka hapa ninavyoongea kila mtu kichwa kinamuuma, kuangalia ni jinsi gani mwakani tutaliendesha zoezi hili kwa ufasaha na kushirikisha wadau wengi zaidi. Leo kwa mara ya kwanza katika histioria ya nchi hii, wanafunzi saba, watatunukiwa, kutokana na kufanya kwao vizori kitaaluma na michezo wakiwa mashuleni pia wadau waliojitoa kusaidia sekta ya elimu ili kutoa motisha kwa wengine, mwakani kufanya vizuri zaidi, ili nao mungu akijaalia wapate tunzo hizi, na watambulike kwa jamii yao.
Imani yetu ni kwamba, zoezi hili linaweza kuleta chachu kwa wanafunzi walio mashuleni kote nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla, kufanya vizuri katika masomo yao ili kujenga tabaka la viijana wenye uwezo mkubwa kitaaluma kwa manufaa ya Taifa letu lijalo. Lengo letu lilikuwa ni kutoa tunzo kwa vijana zaidi ya hawa, lakini kutokana na sababu za kiufundi, tukajikuta tunawatunza hawa tu, ingawa tunajua, wapo wengi, lakini tunaahidi klwamba mwakani, tutafanya hivyo maana shughuli yetu, kupitia nyinyi mliokuja leo, itakuwa na uwakilishi mzuri huko mashuleni, na maofisini mweu na kwa nduh]gu na jamaa ambao hawatasita kutuunga mkono pindi tutakapowapigia hodi kutaka msaada.
Tunatamani kuona jamii ya watanzania inajikita katika kuunga mkono masuala ya elimu, na kwa kufanya hivyo, elimu linabaki kuwa suala la ushindani, ambapo kwa kila mwanafunzi anajitahidi kufanya vizuri kuliko mwenzake, jambo ambalo linaweza mwisho wa siku kusababisha kila mwanafunzi, kuwa na ari ya kufanya vizuri na kupunguza idadi ya wanafunzi wanaofeli masomo yao Tanzania na nje ya mipaka yakie.Ni eneo pialitakalojenga ukaribu kati ya waalimu, wanafunzi na wadau wa elimu kwa pamoja, lengo likiwa ni kuwaweka watu hawa pamoja ili kujadili mustakabali wa sekta hii muhimu kwa Taifa lijalo, kujua njinsi ya kutatua chawngamoto zinazoikabili, na kwa pamoja kuzitatua kama wadau na kuisogeza taaluma hii muhimu katika hatua nyingine.
Tunakijua kilio cha waalimu, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika juu ya kutopewa kipaumbele kwao katika jamii na kufanywa watu wa tabaka la mwisho kabisa, wakati ukweli ni kwamba hawa ndio siri ya mafanikio ya kila mtu humu ndani, tunaahidi tutafanyia kazi kipengele cha kujua mchango wa waalimu katika maisha yetu ya kila siku.Leo haikuwa siku ya maneno mengi, mengi yatakuja baada ya shughuli hii ndugu zetu, tunaomba sana mtupokee tulivyo, Mungu awabariki sana, ahsanteni kwa kuja.
Similar Videos