Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

STORY ZA BURUDANI NA MICHEZO KWA WIKI HII KAMA ULIZIKOSA HIZI HAPA.

Views:
Video Information
STORY AMBAZO ZIMETREND WIKI HIIIIII KWA SANAA NA KILA KONA KATIKA BURUDANI.

USIKU WA KUAMKIA LEO Mach 5 2016 Tanzania imeingia kwenye headlines tena baada ya waigizaji wa Tanzaniakuchukua Tuzo Africa Magic Viewer’s Choice Awards 2016 zilizotolewa Lagos Nigeria ambapo mwimbaji toka Tanzania Alikiba  alikuwa mmoja kati ya wasanii waliotumbuiza kwenye tuzo hizo.
Wasanii wa Filamu Tanzania Elizabeth Michael na Single Mtambalike wamefanikiwa kuondoka na tuzo moja kila mmoja ambapo Elizabeth Michael (Lulu) amechukua Tuzo ya Best Movie East Africa kupitia movie yake ya Mapenzi na Single Mtambalikeamechukua Tuzo ya Best Indigeous Language Movie/TV Series Swahili kupitia Movie ya Kitendawili
Nimekuwekea list ya washindi wote kwenye Tuzo za Africa Magic Viewer’s Choice Awards 2016
BEST ART DIRECTOR (MOVIE/TV SERIES)
The refugees – Frank Raja Arase
BEST TELEVISION SERIES
Daddy’s Girls – Ariyike Oladipo
BEST MAKEUP ARTIST (MOVIE/TV SERIES)
Ayanda – Louiza Calore
BEST SHORT FILM
A day with death – Oluseyi Amuwa
BEST WRITER (MOVIE AND TV SERIES)
Ayanda – Trish Malone
BEST LIGHTING/DESIGN
Common Man- Stanley Ohikhuare
BEST CINEMATOGRAPHY
Tell me sweet something- Paul Michaelson
BEST SOUND EDITING
Marquex Jose Guillermo
BEST PICTURE EDITING
Rebecca- Shirley Frimpong-Manso
BEST COSTUMING
Uche Nancy- Dry
BEST INDIGENOUS LANGUAGE MOVIE (SWAHILI)
Kitendawali- Single Mtambalike
BEST INDIGENOUS LANGUAGE MOVIE (HAUSA)
Dadin Kowa- Salisu Balarabe
BEST INDIGENOUS LANGUAGE MOVIE (YORUBA)
Binta Ofege – Abiodun Jimoh and Jumoke Odetola
BEST INDIGENOUS LANGUAGE MOVIE (IGBO)
Usekwu Igbo- Paul Igwe
BEST DOCUMENTARY
Faaji Agba- Remi Vaughan Richards
BEST SUPPORTING ACTOR
A soldier’s story- Sambassa Nzeribe
BEST SUPPORTING ACTRESS
Before 30- Tunbosun Aiyedhin
BEST ACTOR IN A COMEDY
Jenifa’s Diary- Folarin Falana
BEST ACTRESS IN A COMEDY
Jenifa’s Diary- Funke Akindele
TRAILBLAZER AWARD
Kemi Lala-Akindoju
INDUSTRY MERIT AWARD
Sadiq Daba
Bukky Ajayi
BEST MOVIE- SOUTHERN AFRICA
JOYCE MHANGO CHAIGUALA
BEST MOVIE- EASTERN AFRICA
Mapenzi- Elizabeth Michael
BEST MOVIE- WESTERN AFRICA
Chinny Onwugbenu, Chichi Nwoko and Genevieve Nnaji – Road to Yesterday
BEST ACTRESS IN A DRAMA
Falling- Adesua Etomi.
BEST ACTOR IN A DRAMA
A Soldier’s Story- Daniel K. Daniel
BEST DIRECTOR
Tell me Sweet Something- Akin Omotosho
BEST OVERALL MOVIE
Dry- Stephanie Linus
…………………………………………………………………………………….

Juma lililopita mwanamuziki Juma Nature alionekana akizungumzia suala la kuwa na management na kama anajutia kutofanya kazi na Fela, katika kazi zake za muziki ambapo Nature alisema hawezi kumtafuta Fella na labda Fella ndio amtafute yeye.

Usiku wa kuamkia leo kupitia show ya Friday Night Live inayoruka saa tatu usiku ndani ya EATV na EA Radio, Mkubwa Fella alilizungumzia suala hilo la Juma Nature nakusema kuwa kama itatokea kutaka kufanyakazi na msani huyo basi atamtafuta na kufanya naye kazi.

Hapo awali mwanamuziki Juma Nature alishawahi kufanya kazi chini ya Mkubwa Fella, huku kwa sasa Fella akiwa anafsnya kazi na makundi mbalimbali ya muziki na wanamuziki mbalimbali. Kati ya makundi ya muziki anayo fanya nayo kazi nakufanya vizuri ni Yamoto Band na Salamu TMK.
……………………………………………………
Msanii Chid Benz alimaarufu kama Chuma amefunguka na kusema wakati wana rekodi wimbo wa 'Hasira za Nini' ambao alimshirikisha Ali Kiba anadai ilifika mahali msanii King Kiba alidondosha chozi.

Kupitia kipindi Cha Planet Bongo cha East Africa Radio ambapo Chid benz alipewa "Heshima ya bongo fleva" alifunguka na kusema wakati wapo Mj Records kufanya kazi hiyo Ali Kiba alidondosha chozi sababu yeye alimfungia mlango ndani na kumwambia hawezi kutoka mpaka atakapo maliza kuweka vocal.


"Unajua mdogo wangu Ali Kiba alipoingia booth mimi nikamfungia mlango kabisa ili asitoke so akawa analalamika maana mle ndani kulikuwa na joto sana, lakini nikamwambia mdogo wangu huwezi kutoka mpaka umalize kazi baada ya hapo akalia kisha akakaa zake chini baadae aliinuka na kuendelea na kazi mpaka mzigo ulipoisha ndio nikamfungulia mlango na kutoka " Amesema Chid Benz

Katika hatua nyingine Chid Benz amesema licha ya yeye kufanya muziki wa Hip hop lakini alikuwa na mashabiki wengi wakike kutokana na sauti yake pamoja aina ya nyimbo alizokuwa akiimba.

"Unajua kwangu mimi niliweza kuwa na mashabiki wa kike wengi kutokan na ukweli kwamba wanawake wanapenda sana sauti nzuri na nzito na mimi Mungu amenijalia sauti lakini pia nilikuwa naimba sana mapenzi lakini napochana kwenye mapenzi nilikuwa sifanyi zile ngumu lakini kingine nilikuwa naweza kuyaelezea vizuri mapenzi" Aliongeza Chid Benz.
……………………………………………………………….
Mwanamuziki Harmonize amefafanua kwanini alishoot video yake ya Aiyola nje na sio Tanzania kuwa kunasaidia kukuza muziki wetu kuwa mkubwa na vifaa wanavyotumia ni rahisi sio kama nchini. Na pia amekanusha kauli yakusema kuwaTanzania hakuna ma director wazuri.
AMESEMA  nje ukishoot video ni rahisi kwa kupata material na location kiurahisi japokuwa unatumia pesa nyingi.


Amefafanua kuwa mfano nchini Afrika Kusini uki shoot video ukiwa unahitaji gari la polisi basi kweli utapata gari la polisi, Lakini kwa nchini ni vigumu. Pia amempongeza director Hanscana kwakujiongeza na kuonyesha uaandaaji wa studi yake kwaajili ya kutengeneza video.
………………………………………………….
Wengi walipoona picha ya mwanamuziki wa bongo fleva Nasib Abdul aka Diamond Platnumz aliyoipiga na mwanamuziki nguli wa rap kutoka Marekiani rapper Kanye West wengi wametamani kuona kuwa msanii wetu anafanya kazi na mwanamuziki huyo kwa kuangusha comment zao za kumpongeza kwa namna anavyo jituma kujitangaza.

Tupia comment zako hapo chini kuwa unaona inawezekana kwa Diamond Platnumz  kufanya ngoma ya pamoja na rapperKanye West?
………………………………………………..
Msanii wa muziki kutoka ‘label’ ya WCB, Harmonize amesema wazo la wimbo wake mpya ‘Bado’ aliyomshirikisha Diamond, lilikuja baada ya kumuuliza Diamond ni mwanamke gani ambaye ameachana nae lakini bado anashindwa kumsahau.

Akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV Ijumaa hii, Harmonize amesema baada ya kupata wazo kutoka kwa Diamond ndipo akaanza kuandika wimbo.

“Idea ilikuja kuna siku tulikuwa kwenye gari nikamuuliza (Diamond) kuna mwanamke gari ulimpenda sana hadi leo unashindwa kumsahau, akaniambia hakuna masihara kwenye mahusiano, mimi ndio nikapata idea,” alisema Harmonize.

Aliongeza, “Nikaona kama ni Diamond sio Diamond peke yake ambaye amekutwa na mambo hayo kwenye mahusiano, hata mimi mwenyewe yameshanikuta. Kwa hiyo nikaanza kuandika, nilivyoandika mistari yangu, nikampa producer akanipa beat nikachagua. Baada ya hapo kwa sababu Diamond alikuwa Nigeria alivyorudi siku nipo nae kwenye gari nikaiplay akaikubali akasema na mimi nitaingiza verse ya pili,”
………………………………………………………….
Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini, Flora Mbasha, amekimbilia nchini Kenya kurekodi albamu yake mpya anayotarajia kuipa jina tofauti na nyimbo zitakazokuwa katika albamu hiyo.

Mwimbaji huyo ambaye kwa sasa amefungua darasa la kufundisha uimbaji wenye mafanikio, alisema albamu hiyo inayotarajiwa kuingia sokoni mwishoni mwa Machi, imerekodiwa nchini humo kwa lengo la kubadili ladha ya muziki tofauti na ule anaorekodia hapa nchini.

“Nyimbo tatu kati ya nane zilizomo kwenye albamu hiyo ndizo nimezirekodia hapa nchini, nyingine zote nimerekodi nchini Kenya na lengo langu ni kupata ladha tofauti,’’ alieleza.

Flora alizitaja nyimbo zitakazokuwa katika albamu hiyo kuwa ni ‘Rafiki wa Kweli’, ‘Nakupenda Yesu’, H’akuna Kama Yesu’, ‘Nikuone Mungu Wangu’, ‘Sema Zaidi’, ‘Jipe Moyo (remix)’, ‘Mungu Umenivusha’ na ‘Kwa Yesu Nasimama’.
…………………………………………………
Staa wa muziki Ali kiba amedai anatamani kufanya kazi na producers wa Kitambo kwenye sanaa Tanzania, Master Jay wa MJ Records pamoja na P Funk Majani wa Bongo records.

Akizungumza katika kipindi cha The playlist cha Times Fm, Kiba amesema hakuwahi kufanya nao kazi ndio maana ana hamu nao sana.

“Kiukweli Master Jay na P funk natamani sana kupiga nao kazi, na naahidi kuwatafuta na kufanya nao kazi, kwa hiyo fans wangu wategemee kazi nzuri ntakazofanya nao” alisema.

Katika ‘line’ nyingine King kiba amedai, anamkumbuka sana pia producer aliyetengeneza kazi zake kadhaa, KGT kwa sababu alikuwa ni zaidi ya mwalimu wa muziki kwake.
……………………………………………………
Msanii na muandaaji wa nyimbo za bongo fleva hapa nchini Nahreel amesema baba yake mzazi alikuwa anataka yeye awe mpiga kinanda wa kanisani jambo ambalo lilimfanya kuchelewa kuanza kujihusisha na muziki. Nahreel ambaye ni mmoja wa wanaounda kundi la Navy Kenzo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Kazi kinachorushwa na kituo cha EATV.

''Baba alitamani sana mimi niwe mpiga kinanda wa kanisa lakini kila mara nilikuwa nikirudi nyumbani kutoka shule nasikiliza muziki napenda muziki nikisoma magazeti stori nyingi ni muziki ikanibidi kuupenda muziki moja kwa moja'' Amesema Nahreel.

Aidha msanii huyo anaetamba na wimbo wa 'Kamatia' amewataka wanamuziki chipukizi nchini kutokata tamaa na kujitambua na kuamini kuwa kile ambacho kipo ndani yao na kuhakikisha wana weka mikakati ya kufikia malengo husika.

Wakati huo huo msanii mwenzake anaeunda kundi hilo la Navy Kenzo Aika amesema kuwa katika muziki ni lazima kujipanga na kuwekeza ili kuweza kufikia malengo ambayo msanii anakuwa amejiwekea.
…………………………………………………..
Mwanamuziki kinara wa nchini Uganda, Eddy Kenzo amelazwa katika hospitali ya Malcolm nchini humo baada ya kuugua Typhoid na Malaria masaa machache tu baada ya kutoka jiji la Nairobi kwenye show aliyo ifanya huko.

Kwamujibu wa chanzo cha karibu na staa huyo, Eddy Kenzo imemlazimu kusimamisha show zake alizokuwa azifanye mpaka itakapo malizika Pasaka.

Kutokana na kudhoofu sana ndani ya mwili, Dakitari wa mwanamzuiki huyo amemshauri pia apate muda mrefu wa kupumzika kutokana na mwili wake kuchoka zaidi.
………………………………………………………..
Mwanamuziki nyota Kylie Minogue anajaribu kumzuia ''Kylie'' Jenner kutotumia jina Kylie kama nembo yake nchini Marekani. Na mawakili wa mwanamuziki huyo hawataki vita. Wamewasilisha stakhabadhi mahakamani wakisema kwamba nyota huyo wa kipindi cha ''keeping up with the Kardashians'' hana umuhimu mkubwa katika kipindi hicho na kwamba huonekana katika ''maonyesho ya picha''. Wamesema kuwa kumpatia nembo ya Kylie J kutamuharibia Minogue nembo yake ya Kylie M.


Stakhabadhi hizo zinamuelezea Kylie Jenner kama ''msichana aliyehitimu masomo nyumbani'' zikisema kwamba onyesho lake la picha na machapisho yake yamezua hisia kali kutolka kwa makundi ya watu walio na ulemavu pamoja na jamii za Waafirika wa Marekani.

Hilo lilionekana wakati Kylie Jenner alipopiga picha akiwa katika baiskeli ya walemavu mbali na hisia alizopata baada ya kuchapisha picha za nywele zake katika mtandao wa instgram.

Mashabiki wa mwanamuziki huyo pia wanamuunga mkono wakisema kuwa katika tweeter kwamba #TheresOnlyOneKylie. Wengine wanasema kuwa kuna Kylie M mmoja kwa kuwa hawamjui Jenner ni nani.
………………………………………
Mkali wa wimbo wa ‘Aiyola’ na ‘Kidonda Changu’, Harmonize, amezidi kumng’ang’ania mkali wa Bongo Fleva Afrika Mashariki, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa kuendelea kumshirikisha katika wimbo wake mpya wa ‘Bado’.

Harmonize alisema ameamua kumshirikisha mkali huyo kutokana na maoni ya mashabiki wao kufananisha uimbaji wao, hivyo wameamua kuimba pamoja ili mashabiki wao waone utofauti wao.

Beat ya wimbo huo imetengenezwa na prodyuza Fraga ambaye awali alimtumia midundo mitatu tofauti akachagua huo.

Pia video ya wimbo huu imefanyika nchini Afrika Kusini na muongozaji ni Nick, aliyeongoza video ya Aiyola ya Harmonize, ‘Make Me Sing’ ya Aka na Diamond, ‘Love Boat’ ya Kcee na Diamond na ‘Walk it off’ ya Fid Q.
………………………………………………………………….

Hii hapa ni orodha ya washindi wa makala ya 88 ya Tuzo za Oscars waliotangazwa katika hafla kuu jijini Los Angelez zilizotolewa jumatatu.


Filamu bora zaidi
Mshindi: Spotlight
The Big Short
Bridge of Spies
Brooklyn
Mad Max: Fury Road
The Martian
The Revenant
Room


Mwigizaji bora wa kiume
Mshindi: Leonardo DiCaprio - The Revenant
Bryan Cranston - Trumbo
Matt Damon - The Martian
Michael Fassbender - Steve Jobs
Eddie Redmayne - The Danish Girl


Mwigizaji bora wa kike
Mshindi: Brie Larson - Room
Cate Blanchett - Carol
Jennifer Lawrence - Joy
Charlotte Rampling - 45 Years
Saoirse Ronan - Brooklyn


Mwigizaji bora msaidizi wa kiume
Mshindi: Mark Rylance - Bridge of Spies
Christian Bale - The Big Short
Tom Hardy - The Revenant
Mark Ruffalo - Spotlight
Sylvester Stallone - Creed


Mwigizaji bora msaidizi wa kike
Mshindi: Alicia Vikander - The Danish Girl
Jennifer Jason Leigh - The Hateful Eight
Rooney Mara - Carol
Rachel McAdams - Spotlight
Kate Winslet - Steve Jobs


Mwelekezi bora
Mshindi: Alejandro G Inarritu - The Revenant
Lenny Abrahamson - Room
Tom McCarthy - Spotlight
Adam McKay - The Big Short
George Miller - Mad Max: Fury Road


Filamu bora ya kutokana na kitabu
Mshindi: The Big Short (Adam McKay and Charles Randolph)
Brooklyn
Carol
The Martian
Room


Filamu bora ya hadithi asili
Mshindi: Spotlight (Tom McCarthy na Josh Singer)
Bridge of Spies
Ex Machina
Inside Out
Straight Outta Compton


Filamu bora ya katuni hai
Mshindi: Inside Out
Anomalisa
Boy and the World
Shaun the Sheep Movie
When Marnie Was There


Filamu bora ya lugha ya kigeni
Mshindi: Son of Saul - Hungary
Embrace of the Serpent - Colombia
Mustang - France
Theeb - Jordan
A War - Denmark


Filamu bora fupi ya katuni hai
Mshindi: Bear Story (Gabriel Osorio na Pato Escala)
Prologue
Sanjay's Super Team
We Can't Live without Cosmos
World of Tomorrow


Filamu bora ya sinema
Mshindi: The Revenant (Emmanuel Lubezki)
Carol
The Hateful Eight
Mad Max: Fury Road
Sicario


Filamu yenye mavazi bora
Mshindi: Mad Max: Fury Road (Jenny Beavan)
Carol
Cinderella
The Danish Girl
The Revenant


Filamu bora ya makala
Mshindi: Amy
Cartel Land
The Look of Silence
What Happened, Miss Simone?
Winter on Fire: Ukraine's Fight for Freedom


Filamu bora ya makala fupi
Mshindi: A Girl in the River: The Price of Forgiveness
Body Team 12
Chau, Beyond the Lines
Claude Lanzmann: Spectres of the Shoah
Last Day of Freedom


Filamu iliyohaririwa vyema zaidi
Mshindi: Mad Max: Fury Road (Margaret Sixel)
The Big Short
The Revenant
Spotlight
Star Wars: The Force Awakens


Filamu bora zaidi ya kuigizwa moja kwa moja
Mshindi: Stutterer
Ave Maria
Day One
Everything Will Be Okay (Alles Wird Gut)
Shok
Filamu ambayo waigizaji wamepambwa vyema zaidi
Mshindi: Mad Max: Fury Road (Lesley Vanderwalt, Elka Wardega and Damian Martin)
The 100-Year-Old Man Who Climbed Out the Window and Disappeared
The Revenant


Filamu yenye midundo bora asili
Mshindi: The Hateful Eight
Bridge of Spies
Carol
Sicario
Star Wars: The Force Awakens
Filamu yenye wimbo bora asilia
Earned It, The Weeknd - Fifty Shades of Grey
Manta Ray, J Ralph & Antony - Racing Extinction
Simple Song #3, Sumi Jo - Youth
Til It Happens To You, Lady Gaga - The Hunting Ground
Writing's On the Wall, Sam Smith - Spectre


Filamu yenye maandalizi bora
Mshindi: Mad Max: Fury Road (Colin Gibson and Lisa Thompson)
Bridge of Spies
The Danish Girl
The Martian
The Revenant


Filamu iliyohaririwa sauti vyema
Mshindi: Mad Max: Fury Road (Mark Mangini and David White)
The Martian
The Revenant
Sicario
Star Wars: The Force Awakens


Filamu iliyochanganywa sauti vyema
Mshindi: Mad Max: Fury Road (Chris Jenkins, Gregg Rudloff and Ben Osmo)
Bridge of Spies
The Martian
The Revenant
Star Wars: The Force Awakens


Filamu yenye picha zilizobuniwa vyema
Mshindi: Ex Machina (Andrew Whitehurst, Paul Norris, Mark Ardington na Sara Bennett)
Mad Max: Fury Road
The Martian
The Revenant
Star Wars: The Force Awakens
……………………………………………………………
Staa wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ baada ya kudai kuwa weupe wake unatokana na kunywa maji mengi na kufanya mazoezi na siyo mkorogo, makampuni manne yanayojishughulisha na masuala ya maji yamemtaka awe balozi wao.

Akizungumza na gazeti la Mtanzania jana, Ray alisema kubadilika kwake kwa ngozi kumeleta gumzo kubwa kwake na pia kumempatia neema kutokana na makampuni hayo kutaka awe balozi wao.

“Kunywa kwangu maji kwa wingi na kushiriki mazoezi ipasavyo ndiyo kumepekekea ngozi yangu kuwa nyororo na makampuni yaliyojitokeza kwa sasa nimewaambia wasubiri kwanza hadi nitakapokuwa tayari kuwa balozi wao,’’ alieleza Ray.
,…………………………………………….
Baba Levo ambaye hivi sasa ni mheshimiwa Diwani Kata ya Mwanga Kigoma kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka na kusema kuwa wanaosema Shilole amechuja ni kina nani hao? Baba Levo alijiuliza hilo na kuzua utata kwani baadhi ya watu walianza kuhisi kwamba watu hao ni wapenzi kutokana na ukaribu wao pindi Baba Levo anapokuwa Dar es Salaam.

Kufuatia kuzua utata kipindi cha eNEWS cha EATV kilimtafuta Baba Levo ili kutatua utata juu ya suala hilo na kutaka kufahamu kama kweli Baba Levo anatoka na Shilole, lakini Baba Levo alikana kutoka kimapenzi na Shilole na kudai kwamba Shilole anatakiwa kutoka na wahanagwa wenzake lakini sio yeye, na kudai wao ni marafiki tu wa karibu.

"Shilole hawezi kuwa na mtu kama mimi, unajua mimi ni kiongozi saizi hivyo huyo Shishi anatakiwa kutoka na wahanagwa wenzake sio mimi nikija Dar es Salaam nakaa kwangu, na kuhusu mimi kuchukua gari la Shilole na kuweka bond hizo ni stori tu kwani natambua kuna watu ambao wanataka kunichafua, lakini hawajui mimi ni mchafu kwani nilishachafuliwa sana kwenye siasa lakini wale walionichafua walishindwa wao na mimi nikashinda na kuwa Mh. Diwani." Alisema Baba Levo.
MATOKEO YA MECHI KATIKA LIGI MBALIMBALI.
ENGLAND.
05/03
                                                                                                                              Swansea
05/03
05/03
05/03
05/03
06/03
06/03
12/03
12/03
12/03
………………………………………..
HISPANIA.
03/03
05/03
05/03
05/03
05/03
06/03
06/03
06/03
06/03
06/03
………………………………….


Similar Videos