Video Information
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Jaffar Michael afanya
ziara ya kutembelea masoko
yaliyopo mjini Moshi kwa kusikiliza kero mbalimbali za wafanyabiashara
zinazowakabili.
Bw
Jaffar alikuwa ameambatana na mstahiki meya wa manispaa ya moshi Bw Raymond
Mboya walitembelea masoko mbalimbali kwa kusikiliza kero mbalimbali na kuona
namna gani ya kuboresha masoko hayo.
Miongoni
mwa masoko yaliyotembelewa ni pamoja na soko la pasua,soko la majengo,soko la
mbuyuni,alikutana na kero mbalimbali ambazo zinawakibili wafanyabiashara katika
hayo msoko mh Jaffar aliyofanya ziara.
Mbunge
huyo Mh,Jaffar alipata fursa ya kumsikiliza kiongozi wa soko la mbuyuni
aliyejulikana kwa jina la Lameck ambaye aliweza kumweleza matatizo ambayo
wanakutana nayo wawapo sokoni hapo pamoja na kumuomba aweze kutatua kero ambazo
ameweza kukutana nazo katika hayo masoko.