Video Information
M AISHA.
KATIKA sayansi ya mafanikio kuna mambo mengi sana yanahusika
kutufikisha pale tunapopataka. Pia kuna njia tofauti zinazopendekezwa na
wataalamu wa masuala ya saikolojia. Mfano mwanafilosofia wa Ugiriki, Aristotle
anasema: “Binadamu ni kiumbe wa malengo.” Pia kuna watu wanaweza wakahoji kwa
nini tuwe na malengo katika maisha yetu ya kila siku. Zifuatazo ni sababu
chache tu za kwanini tuwe na malengo. Kwa sababu mafanikio ni malengo na
vingine vinafuata kwa hiyo kama unataka mafanikio ya kweli inabidi uwe na malengo, bila malengo unakuwa ni sawa na kisiwa chenye utajiri mwingi, lakini bado hakijavumbuliwa, kwa hiyo jitahidi uwe na malengo ikiwa ndiyo njia ya kufanikiwa. Malengo ni kama mafuta katika safari ya kufanikiwa, umuhimu wa malengo unafananishwa na mafuta katika gari kwani bila mafuta haiwezi kwenda, ni sawa na malengo katika kazi hata kama una bidii sana kufanya kazi bila malengo itakuwa vigumu kupima utendaji wako mwenyewe wa kazi wa kila siku. Malengo yanakusaidia kufikiria kile unachotaka, na kuwa na uwezo wa kufikiria kile unachokitaka inakusaidia kuwa na nguvu ya ziada kuelekea kupata yale unayoyataka katika maisha, ili uweze kufanikiwa ni lazima uwe na maono ya kule unakoelekea. Malengo yanakupa uwajibikaji kwa sababu mtu unakuwa unajua nini unachokitaka au umepanga kufanikiwa nini kwenye sehemu yako ya kazi. Malengo pia yanakusaidia kutumia muda vizuri ambao ni kitu muhimu katika maisha, ukishindwa kutunza muda huwezi kufanikiwa. Lakini vitu vya msingi ni kujifunza kwa mbinu tofauti ili tuweze kufikia malengo. Kwa mfano mwandishi mmoja anaitwa Brian Tracy, anaelezea umuhimu wa malengo katika kitabu chake kinachoitwa Goals. Anasema malengo ndio kitu pekee kinachosababisha mafanikio na jinsi ya kuwa na mtazamo wa mbele kuelekea kile unachokitaka. Kuna sababu nyingi sana za kwanini watu hawaweki malengo katika maisha licha ya kuwa njia majawapo ya kufikia mafanikio. Zifuatazo ni baadhi ya sabababu za kwanini watu hawaweki malengo. Kuogopa kukataliwa kama kitu unachopanga kufanya watu watakikataa, hivyo utajikuta unakata tamaa na kuhisi kukataliwa kihisia. Hiyo inasababisha kuogopa kuweka malengo, hasa pale unapohisi utashindwa kuyafanikisha, kwa ushauri tu jiamini, jipange na usije ukamwambia mtu yeyote malengo na anza kuyatekeleza acha waone matokeo ya kile unachokifanya. Hofu ya kushindwa Kushindwa kitu chochote kunaumiza na kunakatisha tamaa na msongo wa mawazo. Lakini inabidi ujifunze kukabiliana navyo kwa sababu unapoanza kitu chochote kipya ujue kuna changamoto zake. Hapa namaanisha kwamba usije ukadhani unavyoanzisha kitu kipya utakutana na urahisi, hapana kushindwa ni sehemu ya kujifunza. Kutojua jinsi ya kuweka malengo Watu wengi hawajui jinsi ya kuweka malengo wanafananisha malengo na matarajio. Kwa mfano kuwa na familia yenye furaha na pesa nyingi hivi kila mtu anavyo, malengo ni yale yaliyoandikwa kiufasaha na yanaeleweka pia yakiwa na muda. Pia watu wengi hawajui umuhimu wa kuweka malengo katika maisha, pia familia nyingi hazina utamaduni wa kuwa na malengo, sasa basi jiwekee utaratibu wa kuwa na malengo. Malengo hayana umuhimu Kama unaishi na watu ambao hawana malengo au familia ambayo hawazungumzii umuhimu wa malengo ni kweli utafika umri wa utu uzima bila kujua umuhimu wa kuweka malengo. Ukiwa hujaweka malengo yoyote katika maisha ni bure. Wengi tuna matarajio mengi bila ya kuwa na malengo. Mara nyingi watu ambao hawana malengo ni wale ambao hawana furaha katika kazi na ndoa zao, kwa sababu siri ya kupata furaha ya kweli ni kuwa na mipango inayokuletea mafanikio. Kabla hutujaangalia ni kwa namna gani ambavyo mtu unaweza kuweka malengo, lazima tuelewe malengo ni nini hasa na yana sifa zipi. Malengo lazima yaandikwe vizuri tena katika lugha nyepesi, pale unapoyaandika yanakuwa yanajiandika kwenye moyo wako na kusababisha uyakumbuka kila siku. Malengo yawe rahisi kueleweka. Ina maana kwamba malengo ili iwe rahisi kufikiwa ni lazima yawe rahisi kuelezea na ili lengo liweze kufanikiwa ni lazima liwe na wazo moja la msingi likiwa ndilo wazo kuu na la msingi katika lengo lako. Kwa mfano ukiandika unataka kufanikiwa, ukaishia hapo bila kueleza kwenye nyanja ipi, lazima uandike iwe ya kifedha au vinginevyo. Malengo lazima yawe yamejieleza vya kutosha, mfano unataka kuongeza kipato kwa kiasi gani kama ni 350,000 kwa mwezi lazima uandike unataka kuongeza kipato kwa kiasi gani katika lengo lako kuu, usipoweka kiasi mwisho wa siku utashindwa kujipima kama kweli umefikia lengo au la. Na kisha ainisha ni kwa kiasi gani, itakusaidia kuweka mikakati ya jinsi ya kufikia pale unapopataka. Baada ya kuangalia jinsi malengo yanaweza kuandikwa, tuangalie ni jinsi gani tunaweza kuweka malengo. Angalia au chunguza tatizo ambalo linakuzuia kushindwa kufika pale unapopataka na unawajibika kwa kiasi gani katika kutatua hilo tatizo, kikwazo au changamoto inayokukabili. Ukishajua tatizo linalokufanya uwe hapo ulipo na sio pale unapopataka itakusaidia kuwa na mikakati na malengo ya jinsi utavyotatua tatizo au jinsi ya kukabili changamoto ambayo unayo katika kufikia lengo. Jione wewe mwenyewe kama ndio rais au mmiliki wa maisha yako mwenyewe, hakuna yeyote anayehusika na kubadilisha hali ambayo unayo katika maisha yako. Acha kulaumu mtu yeyote kwa makosa yaliyojitokeza au matatizo, cha kufanya ni kuchukua jukumu la kutatua tatizo kuliko kulalamika. Kulalamika hakutatui tatizo ila kunakupunguzia uwezo wa kufikiria na kutatua matatizo. Hivyo basi, chukua hatua matatizo yanapojitokeza ili kujijengea uwezo wa kiutendaji na uwajibikaji. Punguza sababu pale unapokosea, zaidi jikite katika kutatua tatizo, utajijengea misingi imara ya kuwa na malengo katika kazi zako za kila siku na utakuwa na mchango chanya katika eneo lako la kazi. Ukiwa unatoa sababu sana huwezi kuwa mtendaji mzuri na pia utakosa mipango kwa sababu kila kitu unajitetea baada ya kuvaa uwajibikaji wa jinsi ya kutatua tatizo. Jione wewe ndio chachu ya mabadiliko katika maisha yako mwenyewe, kwa sababu uko hapo ulipo kwa sababu ya uamuzi uliofanya na mipango uliyoifanikisha na pia upo hapo kwa uamuzi na mipango uliyoshindwa kuifikia. Hivyo, weka mipango ya jinsi unavyotaka kuwa na kufanikiwa katika nyanja ipi. Kwa kuanzia sasa chukua uamuzi wa kumsamehe mtu yeyote aliyekukosea, msamehe na usijadili tena mambo yaliyopita na weka malengo ya nini unataka kufikia katika maisha yako. Kwa mfano, kama umepunguzwa kazi usimlaumu bosi wako, kama umeonewa jipange upya na anza kutafuta njia nyingine ya kuishi au kupata kazi, usipende kujadili watu wanaokufanyia fitina za kukurudisha nyuma, cha msingi weka mikakati ya kufikia malengo.

…………MAKALA YA AFYA……………..
Utafiti mpya uliotolewa nchini
Marekani, umebainisha kuwa watu wanaopenda kulala bila nguo wanapata faida
nyingi ikiwamo ya kuwa na uwezekano mdogo wa kupata ugonjwa wa kisukari.
Ripoti hiyo ya utafiti iliyotolewa na Taasisi ya Kitaifa ya Usingizi
(NSF), inaeleza umuhimu wa watu kulala bila nguo kuwa ni kuimarisha uhusiano
kwenye ndoa na kupunguza kalori nyingi.
Wataalamu wa usingizi wanasema kwamba ni vizuri mtu akawa katika
hali ya utulivu wakati wa usiku kwa kuwa joto la mwili linahitaji kuteremka
hadi nyuzi 50 za kipimo cha Fahrenheart ili mtu aweze kulala.
Wakati ubongo ukiendeshwa kwa ‘saa’ iliyo ndani ya mwili, hutuma
ujumbe kuutaka moyo ufunguke au kufunga
“Joto la mwili huwa juu saa 5 usiku na kuwa chini saa 10 asubihi,”
anasema Mkurugeni wa Edinburg Sleep Centre, ambaye pia ni mwandishi wa Kitabu
cha Sound Asleep, Dk Chris Idzikowski.
“Kama kitu chochote kitazuia joto lisishuke, ubongo utahakikisha
unajua kinachoendelea, hii inamaanisha, utahangaika kupata usingizi au utakuwa
na usingizi wa mang’amunga’amu,” anasema mtaalamu huyo.
Ripoti hiyo inasema kuwa mtu anapolala bila nguo inakuwa rahisi kwa
mwili kupoa na kuwezesha upatikanaji wa kiwango sahihi kinachohitajiwa na
ubongo kufanya kazi.
Profesa Russell Foster, mtaalamu wa circadian neuroscience katika
Chuo Kikuu cha Oxford, anathibitisha kuwa kulala bila nguo kunaboresha
usingizi.
“Kama ulikuwa unavaa nguo nyingi za kulalalia, itakuwa vigumu kwako
kupunguza joto. Kwa hiyo, punguza nguo unavyoweza,” anasema.
Anasema kuwa ikiwa usingizi umekatishwa kwa sababu ya joto kali,
haimaanishi kwamba utapata usingizi mdogo wakati wote, bali unaweza kupata
usingizi wa kushtuka shtuka.
Usingizi mzuri ndiyo unaofaa kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa
kumbukumbu na uzalishaji wa homoni, kitendo ambacho ni muhimu kwa ukuaji wa
seli na kuzifanyia marekebisho.
Kwa nini mwili unapoa wakati umelala?
Utafiti unasema kuwa siyo vizuri kuoga maji ya moto jioni wakati wa
kwenda kulala, badala yake mtu anapaswa kupasha moto kigodo mikono na miguu
yake. Hiyo ni kwa sababu ili joto la mwili lishuke hadi kufikia kiwango cha
chini kinachochochea usingizi, mwili unatakiwa utoe jasho.
“Jambo hili linafanyika kwa kutuma damu kwenye mishipa karibu na
ngozi- hasa kwenye mikono na miguu, ambako joto linapotea kwa njia ya ngozi,”
inasema ripoti hiyo.
Hata hivyo, kama Profesa Foster alivyoeleza, kama mikono na miguu
yako ni baridi, mishipa ya damu karibu na ngozi itapunguza kasi ya damu
kutembea katika harakati za kutafuta joto na kuzuia lisipotee.
“Hii ina maanisha kuwa joto lako la kawaida haliwezi kushuka
kirahisi,” inasema ripoti.
Taarifa hiyo inasema kwamba ndiyo maana watu wenye ugonjwa wa kuwa
na mikono na miguu ya baridi sana (ugonjwa huo unawaathiri zaidi ya watu
milioni 10 Uingereza, asilimia 10 wakiwa ni wanawake), ambao ndiyo wenye hatari
zaidi ya kupata ugonjwa wa kukosa usingizi, ‘insomnia’.
Hali hiyo husababisha mishipa ya damu kusinyaa, kupunguza kasi ya
damu kutembea, kwa hiyo ingawa watu wanaosikia mikono yao ni ya baridi sana,
joto lao huwa juu sana.
Ripoti hiyo inaendelea kufafanua kuwa wazee wana kawaida ya
kujisikia baridi usiku, labla kwa sababu matatizo ya mzunguko wa damu kwao ni
kawaida.
“Wanawake ndiyo wenye hatari zaidi ya kupatwa na matatizo ya baridi
mikononi na miguuni, hasa wakati fulani wanapokuwa kwenye hedhi.
Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2008 na Taasisi ya Netherland
inayojishughulisha na Sayansi ya Neva, pia unaeleza uhusiano wa joto la mwili
na kulala.
Kuna baadhi ya watu walijitolea kuvaa nguo zinazozuia mabadiliko ya
joto la mwili, ili kuwaruhusu watafiti kuchunguza joto kwenye ngozi bila
kuathiri kiwango cha kawaida cha joto mwilini.
Timu ya watafiti hao waligundua kuwa wakati joto kwenye ngozi
linapopanda kwa nyuzi 0.4, watu waliokuwa wanafanyiwa utafiti walikuwa na
uwezekano mdogo wa kuamka wakati wa usiku. Lilipojitokeza kundi la wazee
kufanya majaribio kama hayo, matokeo yalishangaza. Joto lilipofikia nyuzi 0.4,
lilikaribia kuwa mara mbili ya hali ya kawaida ya kulala, pia lilipunguza
uwezekano wa kuamka mapema kwa asilimia 50 hadi nne.
“Joto kwenye ngozi lilipoongezeka lilisababisha mirija ya damu
kupanuka, hivyo joto kupotea kwa urahisi zaidi. Waliongeza uwezo wa kulala kwa
kuongeza joto na kuruhusu kasi yake kutembea kutoka katikati ya mwili,” anasema
Profesa Foster.
Kwa maneno mengine, ukitaka kulala kirahisi unahitaji kuwa na joto
kali kiasi cha ambacho mishipa ya damu haiwezi kusinyaa, lakini siyo kuwa na
joto kali mpaka mwili wako ukashindwa kupoa.
Namna ya kufanya
“Kuhakikisha kuwa joto lako la mwili linashuka vizuri, badala ya
kuvaa soksi unapolala weka miguuni dumu la maji ya moto,” anasema Dk
Idzikowski.
“Soksi haziruhusu joto kupungua miguuni, badala yake utaishia tu
kuungua. Chupa ya maji ya moto inafanya miguu yako kuwa ya moto, lakini itapoa
au unaweza kuondoa,” anasema.
Kisukari
Kwa mujibu wa utafiti kuhusu kisukari uliofanyika Marekani,
wataalamu waligundua kuwa mtu akilala kwenye chumba chenye baridi anaweza
kuongeza mafuta (brown fat) kwa watu wazima.
Vijana watano wenye afya nzuri walilala kwenye chumba chenye joto
maalumu kwa miezi minne. Mwezi wa kwanza chumba kilikuwa na joto la nyuzi 24,
baadaye lilishushwa hadi nyuzi 19, kisha likapandishwa hadi nyuzi 24 na mwezi
wa mwisho ilipandishwa hadi nyuzi 27.
Vijana hao walikuwa wakila viwango sawa vya kalori na kuangalia
namna insulini inavyofanya, kiasi gani kinahitajika ili kiwango cha sukari
mwilini kiwe sawa, vyote vilikuwa vinapimwa kila siku.
Matokeo yalikuwa ya kushangaza. Baada ya wiki nne za kulala kwenye
chumba chenye nyuzi joto 19, vijana hao walikuwa wameongeza mara mbili kiwango
chao cha mafuta ya kahawia mwilini. Matokeo yalionyesha kuwa waliunguza kalori
nyingi zaidi mchana wakati chumba chao cha kulala kilikuwa na baridi kali
(ingawa si kiasi cha kupunguza uzito) na utendaji wa insulini nao uliimarika.
Mwandishi mkuu wa ripoti hiyo, Francesco Celi anasema kuwa utafiti
umebainisha kuwa kutumia muda mrefu kulala kwenye chumba cha baridi kuwaweza
kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari.
Profesa wa maendeleo ya saikolojia katika Chuo Kikuu cha Nattingham
na mtaalamu wa mafuta ya kahawia, Michael Symonds, anasema kulala bila nguo
kuna faida kubwa.
”Mafuta ya kahawia yanaweza kuzalisha joto mwilini mara 300 kuliko
kuliko kiungo kingine chochote mwilini, inamaanisha kama ukiacha iendelee hivyo
kwa muda mrefu ungeweza kupunguza nguvu ya ziada,” alisema.
Aliongeza: “Kwa hiyo chochote unachoweza kufanya kuchochea, kama
vile kupunguza ‘thermostat’ na kulala kwenye baridi, linaweza kuwa jambo la faida
sana.”
Hata hivyo, mtaalamu huyo anaonya kuwa joto kwenye chumba lisiwe
chini ya kiwango ambalo hutajisikia huru, vinginevyo utashindwa kulala.
Anaendelea kusema kuwa watu wanaosikia joto kali usiku na wanapenda
kulala bila nguo, wanaweza kuwa na kiwango kikubwa cha mafuta ya kahawia,
ambayo yanasababisha mtu ajisikie joto.