Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI ZA WIKI NZIMA KAMA ZILIKUPITA HIZI HAPA MTU WANGU KWA USHIRIKIANO WA KIBO FM.

Views:
Video Information
MAKALA YA MICHEZO NA BURUDANI MARCH 05,2016.

HABARI ZA MICHEZO KITAIFA.
Kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara, Hamis Kiiza wa Simba amesema kesho Jumapili ataichezea timu yake dhidi ya Mbeya City kwa nguvu kubwa ili afunge mabao mengi ili asifikiwe na mpinzani wake Amissi Tambwe wa Yanga.
Kiiza raia wa Uganda hadi sasa amefunga mabao 16 katika ligi kuu akifuatiwa na Tambwe raia wa Burundi aliyefunga mabao 15. Tambwe leo ataichezea Yanga dhidi ya Azam FC katika ligi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Katika mchezo wa kwanza kati ya timu hizo, Simba ilishinda bao 1-0 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. 
Kiiza alisema: “Najua Mbeya City watanikamia kupita kiasi, mimi nitapambana vya kutosha kuhakikisha naongeza idadi ya mabao.”


“Kitu kikubwa ninachotaka kukifanya ili mpinzani wangu Tambwe asinipite ni kutodharau mechi nitakayoicheza na badala yake ni kutumia kila nafasi nitakayoipata kwenye kila mechi ya ligi kuu.


“Siyo kitu rahisi, lakini nitahakikisha ninapambana na kufunga mabao kwenye kila mechi, nitaanza na mchezo wetu wa Jumapili (kesho) dhidi ya Mbeya City.”



Mbeya City yenyewe katika ufungaji itawategemea zaidi Raphael Alpha mwenye mabao matano na Haruna Moshi ‘Boban’ aliyefunga mabao matatu hadi sasa katika ligi.
……………………………………………………………….
Kocha wa JKT Ruvu, Abdallah Kibadeni amemwambia mwenzake wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ aache kuchonga badala yake wakutane uwanjani leo katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara. 



JKT Ruvu inacheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani baada ya kuhama kutoka Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.


Kibadeni: “Ukiwa mwoga maneno ya Julio yanaweza kukupa wasiwasi lakini mimi namwambia tukutane uwanjani.”


Julio amekuwa akikisifia kikosi chake namna kilivyo fiti na kinaweza kufanya mambo kwa uhakika huku akisisitiza hawana hofu na JKT inayosuasua.


Kibadeni amewahi kuwa kocha wa Julio wakiwa Simba, mara ya mwisho alikuwa bosi wake kwa kuwa Kibadeni alikuwa kocha mkuu na Julio msaidizi, wote wakatupiwa virago Simba.
…………………………………………………………………………
Uongozi wa Coastal Union ya Tanga umesema mara tu wachezaji wao watakaporejea kutoka Morogoro walipokwenda kucheza na Mtibwa Sugar, watawamalizia madai yao yote ya fedha zilizobaki.


Wiki iliyopita wachezaji wa timu hiyo waliandamana kudai walipwe mishahara yao ya miezi mitatu, ambapo uongozi wao ulijitahidi ukawalipa mshahara mwezi mmoja.



Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Coastal Union, Salim Bawazir, amesema: “Tutawalipa wachezaji wetu haki zao zilizobaki wakirejea kutoka Morogoro.”


Wachezaji Coastal Union waliandamana kutaka kulipwa mishahara yao ya miezi mitatu.


Baadaye uongozi ulilazimika kuwalipa mshahara wa mwezi mmoja na wenyewe wakaingia uwanjani na kuichanja Mtibwa Sugar kwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho.
………………………………………………………………………………..
Vijana wawili wa Yanga wanaendelea kuja kwa kasi, Simon Msuva na Salum Telela, wameipa matumaini Yanga kufanya vizuri katika mchezo wao wa leo dhidi ya Azam FC.


Lakini matumaini yameongezeka baada ya mshambulijiaji mkongwe, Amissi Tambwe naye kuanza mazoezini pia.


Juzi Msuva na Telela hawakufanya mazoezi wakiwa majeruhi huku Tambwe akisumbuliwa na mafua lakini jana asubuhi wote walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gombani.


Pia Ngoma yeye alirejea Yanga mapema wiki hii akitokea kwao Zimbabwe alipokwenda katika msiba wa mdogo wake aliyefariki wikiendi iliyopita baada ya kugongana uwanjani.


Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm, alisema wachezaji hao wamerejesha matumaini ya timu yao kufanya vizuri katika mchezo wa leo dhidi ya Azam na ule unaofuata dhidi ya African Sports.


“Nilikuwa kwenye wakati mgumu lakini sasa nimerudi katika matumaini baada ya wachezaji hawa kurejea katika hali zao za kawaida, nina kikosi imara sasa,” alisema Pluijm, raia wa Uholanzi. 



Hata hivyo, Pluijm aliwaomba mashabiki wa Yanga kuendelea kuisapoti timu yao ili iendelee kufanya vizuri katika Ligi Kuu Bara na michuano mingine. Yanga imerejea jana jijini Dar es Salaam kutoka Pemba tayari kwa mchezo na Azam.
…………………………………………………………………………………….
Umeona tabia ya kibabe ya mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma? Basi usifikiri kaanza juzi au jana, Kocha Mkuu wa Mbeya City, Kinnah Phiri anamjua vizuri


Ngoma, raia wa Zimbabwe, amekuwa gumzo kwa uwezo wa kufunga mabao na matumizi ya nguvu awapo uwanjani kiasi cha kuwachosha mabeki wengi wa timu pinzani.


Phiri, raia wa Malawi, aliliambia Championi Jumamosi kwamba, anamfahamu vizuri Ngoma tangu alipokuwa anacheza FC Platinum ya Zimbabwe kuwa ni ‘mtu wa kazi’ awapo uwanjani.


“Namjua vizuri Ngoma kwamba ni mtu asiye na mzaha anapokuwa mbele ya lango la timu pinzani, nilimfuatilia wakati naifundisha Malawi kwani ilikuwa kazi yangu kumjua mchezaji wa nchi jirani.



“Bahati nzuri sijawahi kukutana naye nikiwa kocha na yeye timu pinzani, ni mtu anayejua wajibu wake na kama ukimpanga na beki mwenye wasiwasi atafanya anavyotaka,” alisema Phiri.
……………………………………………………………….
Kocha Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja ana aimani kubwa kikosi chake kitaingusha Mbeya City, kesho Jumapili lakini nahodha wake, Mussa Mgosi ameenda mbali kwa kusema uwepo wa Haruna Moshi ‘Boban’ na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwenye kikosi cha wapinzani wao si sababu ya kukosa ushindi.


Mayanja asema, yeye pamoja na wachezaji wenzake watapambana  kuhakikisha wanashinda mechi ya kesho huku wakiombea leo, Azam FC na Yanga zitoke sare ili warudi kileleni.


Simba ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 45 huku Yanga ikiwa kileleni na pointi 46 sawa na Azam iliyo nafasi ya pili.


“Tupo vizuri kushinda mechi na Mbeya City tutaomba Yanga na Azam watoke sare kwani ikiwa hivyo sisi tutarejea kileleni, kikosi kipo vizuri kwa mapambano,” alisema Mayanja.


Kwa upande wake, Mgosi alisema watahakikisha wanashinda mechi hiyo bila kujali uwepo wa Boban na Redondo katika kikosi cha Mbeya City.



“Tunawaheshimu Boban na Redondo, hawa ni wachezaji wakongwe na wazoefu lakini hawawezi kutuzuia tusishinde mchezo huu tutapambana kuhakikisha tunashinda,” alisema Mgosi aliyewahi kucheza nao Simba.
………………………………………………………..
Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inatarajiwa kuchezwa wikiendi ya mwisho wa mwezi Machi mwaka huu, huku timu nane zikichuana kusaka nafasi ya kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.


Machi 26, 2016 utachezwa mchezo mmoja ambapo Wachimba dhahabu wa Geita Gold watakua wenyeji wa wachimba Almasi wa mkoa wa Shinyanga timu ya Mwadui FC katika uwanja wa CCM Kirumba.


Alhamisi ya Machi 31, 2016, Young Africans watawakaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku timu ya Azam FC wakiwa wenyeji wa maafande wa jeshi la magereza Tanzania Prisons katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.


Mchezo wa mwisho wa robo fainali utachezwa Aprili 6, 2016 kwa Simba SC kucheza dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Aprili 7, 2016 itachezeshwa droo ya hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) mojamoja (live) katika Luninga.

Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho msimu huu, ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) 2017.
………………………………………………………………………………
MECHI ZILIZOPITA ZA AZAM NA YANGA:
Oktoba 17, 2015 
Yanga SC 1-1 Azam (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
Agosti 22, 2015
Yanga 0-0 Azam FC (Yanga ilishinda kwa penalti 8-7 Ngao ya Jamii)
Julai 29, 2015
Azam 0-0 Yanga SC (Azam ilishinda kwa penalti 5-3 Robo Fainali Kombe la Kagame)
Mei 6, 2015
Azam 2-1 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
Desemba 28, 2014
Yanga SC 2-2 Azam (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
Septemba 14, 2014
Yanga SC 3-0 Azam FC (Ngao ya Jamii)
Machi 19, 2014; 
Yanga SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
Septemba 22, 2013; 
Azam FC 3-2 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
Februari 23, 2013;  
Yanga SC 1-0 Azam FC (Ngao ya Jamii)
Novemba 4, 2012;  
Azam FC 0-2 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
Machi 10, 2012; 
Yanga SC 1-3 Azam FC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
January 07, 2012
Azam FC 3-0 Yanga SC (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
Septemba 18, 2011;  
Azam 1-0 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
Machi 30, 2011;  
Yanga SC 2-1 Azam FC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
Oktoba 24, 2010; 
Azam FC 0-0 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
Machi 7, 2010;  
Yanga SC 2-1 Azam FC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
Oktoba 17, 2009; 
Azam FC 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
Aprili 8, 2009;  
Yanga SC 2-3 Azam FC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
Oktoba 15, 2008;  
Azam FC 1-3 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
(Rekodi hii inahusisha mechi za mashindano tu, tangu Azam na Yanga wanaanza kukutana)

MWELEKEO wa wapi taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara litaelekea msimu huu tutaanza kuuona leo baada ya mchezo baina ya timu mbili zinazoongoza mbio za taji hilo.
Yanga, mabingwa watetezi wanatarajiwa kumenyana na Azam FC kuanzia Saa 10:00 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo ambao mshindi atapanda kileleni na kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi tatu. Zote zina pointi 46, kila moja baada ya kucheza mechi 19, ingawa Yanga wapo kileleni kwa wastani wa mabao. 
Ni pambano la pili kuzikutanisha timu hizo mwaka huu, na la tano kwa ujumla msimu huu tangu zilipokutana katika Kombe la Kagame Julai mwaka jana, kila timu ikishinda mara moja na nyingine zote kutoka sare.
Julai 29, mwaka jana, timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake iliifunga Yanga SC kwa penalti 5-3 katika Robo Fainali ya Kombe la Kagame kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
Agosti 22, mwaka huu, Yanga SC ikalipa kisasi baada ya kushinda kwa penalti 8-7 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 katika mchezo wa Ngao ya Jamii kabla ya sare mbili mfululizo za 1-1, kwanza kwenye Ligi Kuu Oktoba 17, mwaka jana na baadaye kwenye Kombe la Mapinduzi Januari 5, mwaka huu.

Oktoba 17, mwaka jana Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 45 kupitia kwa Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma aliyepokea krosi ya Juma Abdul na kuwachambua mabeki wa Azam kisha kupachika mpira nyavuni – kabla ya Muivory Coast Kipre Tchetche aliyetokea benchi kipindi cha pili kwenda kuchukua nafasi ya Mkenya Allan Wanga kuifungia Azam bao la kusawazisha dakika ya 83 akimalizia pasi ya Farid Mussa.
Katika mchezo huo, Yanga walipata penati baada ya kipa wa Azam Aishi Manula kumuangusha winga wa Yanga Simon Msuva kwenye eneo la hatari, lakini kiungo Mzimbabwe Thabani Kamusoko akampelekea mikononi kipa wa Azam shuti lake.
Na Januari 5, licha ya Azam FC kucheza pungufu baada ya Azam FC kumpoteza Nahodha wake, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyeonyeshwa kadi ya pili ya njano na refa Mfaume Ali Nassor dakika ya 62, lakini ikamudu kumaliza mechi kwa sare ya 1-1.
Azam FC walitangulia kupata bao dakika ya 58 baada ya shambulizi la kushitukiza – sifa zimuendee mfungaji wa bao hilo, Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast aliyewakokota mabeki watatu wa Yanga SC hadi karibu kabisa na boksi na kufumua shuti lililompita kipa Deo Munishi ‘Dida’. 
Lakini beki Mtogo, Vincent Bossou aliisawazishia Yanga SC dakika ya 83 akimalizia mpira ulioparazwa kwa kichwa na Malimi Busungu baada ya kona ya Simon Msuva.
Na kwa ujumla mchezo wa leo ni 19 wa mashindano kuzikutanisha timu hizo, ikiwemo Ligi Kuu, Kombe la Kagame na Kombe la Mapinduzi, kila timu ikishinda mechi saba, moja kati ya hizo kila timu imeshinda kwa penalti, zimetoka sare mara tano na Yanga imefunga mabao 24, wakati Azam imefunga mabao 23. 
Makocha wa timu zote, Stewart John Hall raia wa Uingereza anayefundisha Azam FC na Mholanzi Hans vad der Pluijm wa Yanga wanajua mchezo wa leo utakuwa mgumu.
Mara ya mwisho zilipokutana katika Kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Amaan, Zanzibar mapema mwaka huu mechi ilitawaliwa na undava na Nahodha wa Azam, John Bocco aliondolewa uwanjani kwa kadi nyekundu timu hizo zikitoka 1-1.
Hall alimvaa Pluijm baada ya kipindi cha kwanza akataka kumchapa makofi, lakini baadaye akajutia uamuzi wake na kabla ya kuanza kipindi cha pili wakamaliza tofauti zao.
Yanga wanaingia uwanjani wakitokea kwenye kambi ya wiki moja kisiwani Pemba, wakati FC wanatokea makao makuu yao, Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Ni mechi ya mshike mshike mzito Yanga na Azam, wakati mwingine inafikia hata viongozi kununiana na mashabiki kuchapana makonde. Leo Taifa kazi ipo!
………………………………..
TANZANIA, Twiga Stars imejiweka katika mazingira magumu ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake baadaye mwaka huu Cameroon, baada ya kufungwa mabao 2-1 nyumbani na Zimbabwe jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Tanzania sasa itabidi ishinde ugenini kwa tofauti ya mabao mawili, au 2-1 ili mshindi aamuliwe kwa mikwaju ya penalti.
Katika mchezo wa leo uliohudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, Twiga Stars walianza vyema baada ya kutangulia kupata bao kupitia kwa kiungo wake mahiri, Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ dakika ya 17 kwa shuti kali la mbali baada ya kupokea pasi ya Asha Rashid ‘Mwalala’.

Iliwachukua dakika mbili tu Zimbabwe kuchomoa bao hilo baada ya Erina Jeke kusawazisha kwa shuti la mbali dakika ya 19. 
Mwanahimisi Gaucho alikaribia kufunga dakika ya 39 kama si shuti lake kutoka nje na dakika 45 za kwanza zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1.
Kipindi cha pili, Twiga Stars inayofundishwa na Nasra Juma ilirudi ikiwa dhaifu zaidi na kuwaruhusu wageni kutawala mchezo.
Zimbabwe ‘waliwakera’ mamia ya Watanzania waliojitokeza Uwanja wa Chamazi baada ya kupata bao la pili dakika ya kwanza tu ya kipindi cha pili, mfungaji Erina Jeke aliyefumua shuti akimalizia krosi ya Majory Nyauwe.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Fatuna Omary, Stumai Abdallah, Maimuna Khamis/Fatuna Khatib dk73, Fatuma Issa, Annastazia katunzi, Donisia Minja, Happinnes Mwaipaja, Amina BIlali, Shlder Boniphace/Fatuma Makusanya dk21, Asha Rashid ‘Mwalala’ na Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’. 
Zimbabwe; Chido Dzingirai, Felistus Muzingodi, Eunice Chibanda, Sheila makoto, Nobhule Majika, Luntet Mutokuto, Daisy Kaitano/Rejoice Kapfuvuti dk75, Emmaculate Msipa, Majory Nyauwe, Erina Jeke/Mavis Chirandu dk79 na Rudo Neshamba/Patience Mujuru dk90.
……………………………………………………….
KOCHA Mkuu wa Mbeya City FC, Mmalawi Kinnah Phiri amesema kipa Juma Kaseja 'Baba Wawili' hatakuwamo kwenye programu ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba SC Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kutokana na sababu za kifamilia.
Muda mfupi uliopita kocha Phiri ameudokeza mtandao huu kuwa ilikuwa waungane na kipa huyo leo asubuhi kwenye kambi ya muda hapa Morogoro lakini imemlazimu kumuongezea muda zaidi wa kukaa  karibu na familia yake ili kushughulikia masuala kadhaa ya kifamilia aliyonayo hivi sasa.
“Wakati anaondoka Mbeya siku tano zilizopita tulikubaliana kuwa ataungana nasi hapa siku ya leo, nimezungumza nae leo asubuhi kuna mambo muhimu ya kifamilia amenieleza hivyo basi nimeamua kumuongezea siku  kadhaa za kubaki nyumbani kushughulikia  yale yote yaliyopo kwenye familia yake na imani yangu kuwa ataungana na kikosi mara tu tutakaporejea mbeya kujiandaa na mchezo dhidi ya Stand United March 10.
Juma  Kaseja aliondoka jijini Mbeya mara  baada ya mchezo wa Kombe la FA  dhidi ya Tanzania Prison  uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine kufuatia taarifa njema  ya mkewe kujifungua watoto mapacha.
Wachezaji wanzeke na uongozi wa City  kwa ujumla unampongeza Juma Kaseja na kumtakia  kila la kheri kwenye malezi ya watoto wake.
Mbeya City imeweka kambi Morogoro kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba na inatarajiwa kuingia Dar es Salaam kesho.
……………………………………………
KIUNGO wa Mbeya City, Ramadhani Chombo 'Redondo' amesema historia itawabeba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Redondo amesema Mbeya City ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo kwa sababu imekuwa na historia nzuri kila inapokutana na Simba kwenye uwanja wa Taifa.

“City imeshinda mara kadhaa mbele ya Simba, hili ni jambo zuri kisaikolojia, kwa sababu linaleta kujiamini, imani yangu kubwa dakika 90 za Jumapili zitakuwa nzuri upande wetum” alisema.
Hata hivyo, kiungo huyo wa zamani wa Ashanti, Simba na Azam FC, amesema kwamba mchezo huo utakuwa mgumu kwa sababu timu zote zitakutana zikitoka kupoteza mechi zake zilizopita za Ligi Kuu.
“Ni wazi utakuwa mgumu, hii ni kwa sababu kila timu inahitaji matokeo mazuri baada ya kupoteza mchezo uliopita, Simba na timu nzuri na wako kwenye nafasi nzuri pia, lakini wasitegeme kupata ushindi kwa sababu sisi tunauhitaji zaidi yao,” alisema.
…………………………..
HABARI ZA KIBURUDANI.
WASANII wa muziki mbalimbali hapa nchini, Jumamosi hii wanatarajiwa kukinukisha vilivyo katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam, katika tamasha la Amsha Mama Festival. Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake, Balozi wa tamasha hilo  Khalid Ramadhani ‘Tundaman’, ambaye amepewa Ubalozi  huo kupitia waandaaji wa tamasha la (AFWAB)  AMSHA MAMA Festival 2016, lililo chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa lebo ya Candy na Candy   Records Joe Kariuki, alisema tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Machi 5 mwaka huu katika uwanja wa Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam. Tundaman na Muandaaji wa tamasha hilo Kariuki, wamesema kwamba maandalizi ya shoo hiyo tayari yameshakamilika kwa kiasi kikubwa hivyo angependa kutumia fursa hii kuwaalika wakazi wote wa jiji la Dar, kujumuika siku hiyo kushuhudia burudani mbalimbali zitakazotolewa na wasanii kibao ambao tayari wemedhibitisha kufanya makamuzi siku hiyo. “Tunapenda kuwaalika Watanzania wote kwa ujumla siku ya jumamosi hii ya Machi 5, mwaka huu waje kwa wingi katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar  Salaam, ili tujumuike kwa pamoja katika tamasha la kuhamasisha wanawake kujikwamua katika shughuli zao mbalimbali za kiuchumi. Tamasha hili litakuwa ni la wazi kwa maana kwamba watu wote watapata burudani kibao bila malipo yaani bure kabisa hivyo waje kuwashuhudia wasanii kama, Khadija Kopa, Mr Blue, Snura, Msaga Sumu, Ali Chocky na Tunda Man wakitoa burudani ya hali ya juu kwani  ulinzi na usalama siku hiyo ni wa uhakika,” alisema Tunda Man. Kwa upande wake,  Joe Kariuki ambaye ni mratibu mkuu wa tamasha hilo ametumia muda huu kuongea na baadhi ya akinamama wanaojishughulisha na biashara za vitu mbalimbali hususani mama ntilie, wauza matunda na wauzaji wa mitumba ili nao wajitokeze kwa wingi kuja kunadi bidhaa zao  siku hiyo kwani hiyo ndiyo fursa yao ya kipekee ya kujitangaza bure.

…………………………………….
Mama mzazi wa Banza Stone Bi Hadija au Sozi alizikwa jijini Dar es Salaam kwenye makaburi ya Sinza jirani kabisa. Mama huyo akazikwa jirani kabisa na kaburi la mwanae - Banza Stone aliyefariki mwaka jana. Mazishi ya mama wa Banza yalikwenda sambamba na ya mjukuu wake au wajina wake Sozi Masanja ambaye ambaye ni mtoto wa dada yake Banza. Mama wa mjukuu huyo alishafariki kiasi cha miaka sita iliyopita. Mjukuu huyo wa mama yake Banza mwenye umri wa miaka 45 amekuwa akichukuliwa na majirani wengi kama mtoto wa mama yake Banza hali iliyoleta mchanganyiko kwa wengi wakati wa kuripoti vifo vyao. Mjukuu huyo aliyeacha watoto wawili alifariki juzi asubuhi akiwa njiani kupelekwa hospitali baada ya kuzidiwa na mmoja wa watu walioshiriki kumwingiza kwenye gari kwa safari ya kuwahishwa hospitali ni mama yake Banza. Masaa wawili baada ya kifo cha mjukuu wake, mama wa Banza nae akafariki kwa msongo wa mawazo
……………………………………..
STAA wa kike wa muvi za Kibongo, Kajala Masanja amesema kwamba mambo ya kimjini kama wafanyavyo mastaa wengine, kwa sasa ameyapa mgongo kwa madai kuwa anaona anaelekea uzeeni. Akiongea na Saluti5, Kajala alisema kwamba kila akijiangalia anaona kabisa kuwa alivyokuwa zamani sio alivyo sasa hivyo ana kila sababu ya kubadilika na kuwa na utulivu. “Kiukweli najiona kabisa naelekea uzeeni, ule usichana unapotea na hivyo ni vyema sasa mambo mengine ya kimjini nikayapa kisogo,” alisema Kajala. “Kwenda klabu usiku nimepunguza na kuna siku nitaacha kabisa, nguo za ajabuajabu najifikiria mara mbilimbili kuzitia mwilini,” aliongeza staa huyo.
…………………………………………..
MKALI wa Bongofleva, Baraka da Prince amemkana laivu staa wa filamu, Nisha akisema kuwa hajawahi kuwa na uhusiano nae wa kimapenzi. Katika mahojiano na kipindi cha E – News cha runinga ya EATV, Baraka da Prince aliulizwa kwa mafumbo kama ana uhusianao na msanii huyo (hakutajwa jina). Kabla hajakana, Baraka da Prince kwanza alijifanya kutomfahamu msanii anayehusishwa naye, ambapo baada ya sekunde kadhaa ndipo alipojifanya kumkumbuka na kusema: “Ahaaa… Nisha sio? Hapana mi sijawahi ku date na yule dada,” alisema Baraka anayetikisa anga la Bongofleva kwa nyimbo zake nyingi kali.
HABARI ZA MICHEZO KIMATAIFA.
BARCELONA imezidi kukimbia kivuli chake katika Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga baada ya ushindi wa mabao 5-1 usiku huu dhidi ya wenyeji Rayo Vallecano Uwanja wa Rayo Vallecano mjini Madrid.
Mwanasoka bora kabisa kuwahi kutokea duniani, Lionel Messi amefunga mabao matatu peke yake usiku huu katika dakika za 23, 53 na 72, huku mabao mengine ya Barca yakifungwa na Ivan Rakitic dakika ya 22 na Arda Turan dakika ya 86.
Bao pekee Rayo Vallecano limefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Angola, Manucho Goncalves dakika ya 57 na sasa Barca inafikisha pointi 66 baada ya kucheza mechi 26 na kuendelea kujinafasi kileleni mwa La Liga, ikifuatiwa na Atletico Madrid yenye pointi 61 za mechi 27 na Real Madrid yenye pointi 57 za mechi 27 pia.
Rayo Vallecano inabaki na pointi zake 26 za mechi 26 na kuendelea kushika nafasi ya 16 katika ligi ya timu za 20. 
Katika mchezo huo, Rayo iliwapoteza wachezaji wake wawili waliotolewa kwa kadi nyekundu, Diego Llorente aliyemchezea vibaya Rakitic dakika ya na Manuel Iturra aliyemuangusha Luis Suarez kwenye boksi. Lakini Suarez alikosa penalti iliyotolewa baada ya kuangushwa kwake.
…………………………………
TIMU ya Liverpool imeichapa mabao 3-0 Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Anfiled.
Ushindi huo ni sawa na kisasi cha kufungwa kwa penalti 3-1 katika fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup Februari 28, Uwanja wa Wembley baada ya sare ya 1-1.
Katika mchezo wa leo, mabao ya Liverpool yamefungwa na Adam Lallana dakika ya 34, James Milner dakika ya 41 na Roberto Firmino dakika ya 57.


Mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya England usiku huu, Manchester United imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga 1-0 Watford, bao pekee la Juan Mata dakika ya 83 Uwanja wa Old Trafford.
Arsenal imefungwa 2-1 nyumbani na Swansea City Uwanja wa Emirates katika mchezo mwigine wa ligi hiyo. Mabao ya Swansea yamefungwa na Wayne Routledge dakika ya 32 na Ashley Williams dakika ya 74, wakati la Gunners limefungwa na Joel Campbell dakika ya 15.


Stoke City imeilaza 1-0 Newcastle United, bao pekee la Xherdan Shaqiri dakika y 80 Uwanja wa Britannia.
West Ham United imeilaza 1-0 Tottenham Hotspur, bao pekee la Michail Antonio dakika ya saba.
………………………………..
BEKI wa kimataifa wa Ivory Coast, Emmanuel Eboue anaweza kurejea Ligi Kuu ya England, baada ya klabu ya Sunderland kuonyesha nia ya kumsajili.
Beki huyo wa zamani wa Arsenal amekuwa kivutio kwenye mazoezi ya Sunderland na leo anatarajiwa kusaini Mkataba wa hadi mwishoni mwa msimu.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 32 kwa sasa ni mchezaji huyu baada ya kutemwa na klabu ya Galatasaray mwaka jana. Kwa wiki tatu amekuwa akifanya mazoezi na Sunderland na akacheza dakika zote 90 Jumatatu U21 ya klabu hiyo ikiifunga Leicester City.

WASIFU WA EMMANUEL EBOUE  

Mwaka Timu  Mechi Mabao
2001–2002 ASEC     25- (3)
2002–2005 Beveren 70- (4)
2005–2011 Arsenal  132-(5)
2011–2015 G'tasaray 77-(4)
Kocha Sam Allardyce aliuangalia mchezo huo wakati kocha wa U21, Andy Welsh alivutiwa na mchango wa mchezaji huyo wa Ivory Coast. 
"Nilizungumza naye na alisema hizo zilikuwa dakika 90 za kwanza kucheza kwa zaidi ya mwaka," amesema Welsh. 
"Alionyesha juhudi nzuri na alionekana vizuri wakati mchezo ukiwa mkali. Amekuwa mtu mzuri kwenye chumba cha kubadilishia nguo akiwa na wachezaji nyota Chipukizi, anawasaidia, hivyo sijapata malalamiko yoyote.
……………………….
SHIRIKISHO la Soka Rwanda (FERWAFA) iatsaini mkataba wa muda mredu na klabu ya Feyenoord ya Uholanzi kwa ajili ya maendeleo ya soka Rwanda.
Rais wa FERWAFA, Vincent Degaule Nzamwita amekutaka na Meneja Uhusiano wa Kimataifa wa klabu hiyo, Gido Vader Jumanne kukamilisha mipango kwa ajili ya akademi ya vijana nchini Rwanda.
Balozi wa Rwanda nchini Uholanzi, Jean Pierre Karabaranga pia alihudhuria mkutano huo, makao makuu ya klabu hiyo mjini Rotterdam.
“Mkutano ulilenga kuangalia uwezekano kuyafanyia kazi yale ambayo tuliyajadili katika mikutano yetu ya awali na kipi kinahitajika ili kuimarisha uhusiano wetu na Feyenoord,” amesema Nzamwita.


“Tangu tumepanga kuwa na mashindano ya U-15, msaada wao wa kiufundi utakuwa muhimu sana sana kukuza skka yetu nchini. Tunaamini muda si mrefu tutaanza kunufaika na msaada wao wa kiufundi. Pia tunamhsukuru Balozi Karabaranga kwa msaada wake kuhakikisha kwamba Feyenoord inakuja kusaidia kuendeleza sekta ya soka,” amesema.
Mwaka jana FERWAFA ilinzisha mashindano ya ligi za vijana chini ya umri wa miaka 15 na miaka 13 (U-15 na U-13) kwa wote, wasichana na wavulana.
Na mabingwa mara 14 wa Ligi ya Uholanzi, maarufu kama Eredivisie wanasifika kwa kuzalisha wachezaji nyota duniani kama Robin Van Persie ambaye kwa sasa anachezea Fenerbahce ya Uturuki baada ya kuwika Arsenal na Manchester United za Ligi Kuu ya England.
Wengine ni Giovanni van Brockhorst, Johan Cruyff, Ruud Gullit, Dirk Kuyt, Bruno Martins Indi na Ron Vlaar.
Akademi ya vijana ya Feyenoord pia ina uhusiano na nchi za Ghana, Nigeria, Afrka Kusini na Vietnam.
Akademi ya Feyenoord inayojulikana kama Varkenoord, ina mfumo mzuri unaoheshimika nchini Uholanzi ambayo imeshinda tuzo ya Rinus Michels kama akademi bora ya vijana kwa miaka mitano mfululizo tangu mwaka 2009.
Varkenoord ilitoa wachezaji 11 katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil, ambayo ni idadi kubwa kuliko akademi zote duniani.
…………………………….
MABINGWA wa Afrika, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wataanza kutetea taji lao kwa kumenyana na St George ya Ethiopia katika hatua ya timu 32 Bora.
Timu hiyo ya mshambuliaji wa Tanzania, Thomas Ulimwengu itaanzia ugenini Machi 11, mwaka huu kabla ya kurudiana mjini Lubumbashi, wiki moja baadaye.


RATIBA KAMILI 32 BORA LIGI YA MABINGWA AFRIKA .


Warri Wolves
v
El Merreikh
TBC
Olympique Khouribga
v
ES Sahel
TBC
Stade Malien
v
Coton Sport FC
TBC
US Douala
v
Zamalek
TBC
AS Vita Club
v
Clube Ferroviário de Maputo
TBC
APR FC
v
Young Africans
TBC
St. George
v
TP Mazembe
TBC
Jumapili Machi 13, 2016


Mamelodi Sundowns
v
AC Leopards
TBC
Zesco United
v
Horoya A.C
TBC
Club Africain
v
MO Béjaïa
TBC
Etoile du Congo
v
ES Setif
TBC
Recreativo do Libolo
v
Al Ahly
TBC
Ahly Tripoli
v
El Hilal
………………………….
KLABU ya Liverpool imebainisha azma yake ya kusainisha wafumania nyavu walio na uwezo na sasa wanamuhitaji Edin Dzeko anayekipiga AS Roma kwa mkopo akitokea Manchester City. Hatua hiyo ya kocha wa sasa wa majogoo hao wa jiji, Jurgen Klopp inakuja siku chache baada ya kukiri anahitaji kuona anapata straika wa kuwasaidia akina Divock Origin a Christian Benteke. Katika nia hiyo ya kusuka idara ya ufumaniaji nyavu, bosi huyo wa majogoo wa jiji yumo katika mbio za kumwania pia Danny Ings wa Burnley. Dzeko anadaiwa kuwaniwa pia na mabingwa wa zamani wa England, Chelsea. Lakini hata hivyo, kwa taratibu za masuala ya uhamisho, Dzeko anaweza kuhama kwa kukubaliana baina ya klabu yake na timu inayohitaji mchango wake ambako dau la kumng’oa limetajwa kufikia pauni mil. 25. Taarifa za ndani ya Liverpool zinasema kuwa Klopp yumo katika mpango wa kuwatema jumla ama kwa mkopo baadhi ya wanandinga wake.

……………………………………………………………………………….
KLABU ya Manchester United wameendelea kuichokoza tena Real Madrid na sasa wamepania tena kupata saini ya Gareth Bale. Taarifa za ndani ya Klabu ya Manchester United zinasema kuwa bosi wao, Louis Van Gaal amepewa ridhaa na uongozi kwa ajili ya kumsajili Bale kwa gharama ambayo haikutajwa. Mpango wa mwaka huu Manchester United ni kama wanakumbusha kidonda cha mwaka jana ambapo klabu hizo mbili ziliingia vitani kwa kila moja kuhitaji mchezaji wa upande wa pili. Katika harakati hizo, united walikuwa wanamwania beki Sargio Ramos ambapo Madrid walikuwa wakisaka saini ya mlinda mlango wa United, David de Gea. Mwishoni mwa msimu uliopita, magazeti ya michezo nchini Hispania, likiwemo Marca liliandika taarifa za awali za Real Madrid kumtengea dau david de Gea kiasi cha pauni 28.6 huku ikisema kuwa bado wana nafasi ya kufika bei wanayoitaka United. Pamoja na De Gea, pia vigogo hao wa La Liga walikuwa wanahitaji pia saini ya mlinzi wa timu ya taifa ya Ureno, Fabio Coentrao. Wakisikiliza tetesi hizo, Manchester United wamweka mezani dau la pauni mil. 29 na bila shaka wamewalenga Real Madrid.

………………………………………………………….
KLABU za jiji la Manchester za Manchester United na Manchester City zimejikuta zikichuana kuwania saini ya nyota wa Juventus ya Italia, Alex Sandro. Hata hivyo maombi ya klabu zote hizo ya kumtwaa mchezaji huyo anayetesa katika Ligi ya Italia ya serie A, yamekataliwa kwa mujibu wa Calcio Melcato.

…………………………………………………………………..
NYOTA Pablo Zabaleta amesema kwamba anavyoamini Manchester City inaweza kutumia uzoefu wake na kuzinduka na kisha ikatwaa ubingwa wa michuano ya Ligi Kuu England. Man City ilitwaa taji lake la kwanza msimu huu Jumapili kwa kuichapa Liverpool kwa mikwaju ya penati na kufanikiwa kutwaa Kombe la Ligi baada ya timu hizo kufungana bao 1-1 mtanange uliopigwa kwenye uwanja wa Wembley. Miamba hiyo inautana tena leo kwenye uwanja wa Anfield huku Man City waiwa nyuma kwa pointi tisa baada ya kufungwa na timu zinazoongoza Ligi hiyo, Leicester City na Tottenham katika mechi zake mbili ilizokutana nazo. Hata hivyo Zabaleta anaamini kwa sasa mirari wao upo juu kutokana na ushindi wa mabao 3-1 walioupata Jumatano dhidi ya Dynamo Kiev katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya na taji hilo la Wembley. Mbali na hilo, Muargentina huyo anakumbushia Man City walivyotwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2011/12 licha ya kuwa ilikuwa nyuma kwa pointi nane dhidi ya Manchester United huku zikiwa zimebaki mechi sita na jinsi ilivyozinduka wiki za mwisho na kuipindua Liverpool kutoka kileleni mwa Ligi msimu wa 2013/14. “Bado kuna pointi 36 za kushindania katika michuano ya Ligi Kuu ambazo ni mechi nyingi,” Zabaleta alisema wakati akinukuliwa na gazeti la Manchester Evening News. “Miaka michache iliyopita tuliwahi kuwa katika hali kama hii. Tulipotwaa ubingwa wa Ligi kama hii tulikuwa nyuma kwa pointi nane dhidi ya timu zilizokuwa zikiongoza na sasa bado tuna mechi mkononi,” aliongeza. Alisema kuwa katika kipindi hiki ni kuelekeza nguvu zao kwenye michuano hiyo ya Ligi Kuu na wajaribu kushinda mechi yao ya leo.

…………………………………………………………….
STAA wa timu ya New York City, Andrea Pirlo ameshindwa kukataa kuwapo kwa uwezekano wa kuongeza mkataba wake na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS). Mkataba wa sasa wa Pirlo unamalizika Desemba mwaka huu, baada ya kiungo huyo wa timu ya taifa ya Italia kuungana na nyota wenzake, David Villa na Frank Lampard akitokea Juventus mwaka jana. Kwa sasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 36 yupo katika dakika zake za mwisho katika kibarua chake, lakini Pirlo anafurahia maisha ya jijini New York na ameshaonekana wazi kuna uwezekano wa kuendelea kuchezea klabu hiyo inayotumia uwanja wa Yankee. “Siwezi kukataa mawazo ya kuendelea kubaki mahali hapa,” Pirlo aliliambia gazeti la New York Times. “Hiki ni kitu ambacho kinaweza kuvutia kutokana na kwamba mara zote nimekuwa nikipenda kuja hapa kucheza, lakini sijawahi kuwaza kama ingekuwa hivi karibuni,” aliongeza staa huyo.

………………………………………………………
BEKI wa Liverpool, Kolo Toure anaamini Ligi ya Europe inaweza akuiokoa timu yake baada ya kupoteza mechi ya Kombe la Capital One. Kikosi hicho cha jurgen Klopp kilitunguliwa na Manchester City kwa mikwaju ya penati na kupoteza nafasi nzuri ya kunyanyua Kombe msimu huu. Wakiwa katika nafasi ya tisa Ligi Kuu, Liverpool watawakabili Manchester United katika timu 16 za mwisho Ligi ya Europe. Toure, 34, anahisi Ligi ya Europe itakuwa tumaini kwa Liverpool msimu huu wa 2015/16. “Tunaweza kumaliza msimu wetu vizuri kwa kushinda Kombe la Europe ingawa Ligi ya Uingereza bado haijaisha,” alisema.   “Tuna mechi nyingi mbele yetu. Tuna mechi nyingine muhimu zaidi. Tunahitaji kusahau kipigo cha City ili tuweze kuendelea na majukumu mengine,” aliongeza.

………………………………………………………………..
NI kama vile kamchongea, nyota wa zamani wa Arsenal, Paul Merson amesema kwamba kocha Arsene Wenger ni lazima afukuzwe endapo timu za Leicester City ama Tottenham zitashinda katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England. Arsenal ambayo haijawahi kutwaa ubingwa wa michuano hiyo tangu mwaka 2004, kwa sasa ipo nyuma ya pointi tano dhidi ya Leicester City kutokana na kipigo cha Jumapili cha mabao 3-2 kutoka kwa majeruhi Manchester United, huku Spurs wao wakiwa wamebaki nyuma kwa pointi mbili dhidi ya vijana hao wa Claudio Ranieri baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya vinara hao.   Vijana hao wa Wenger baadae leo wanakutana na Swansea kabla ya kucheza ‘derby’ kali ya jiji la London dhidi ya Spurs na Merson ambaye aliwahi kucheza chini ya Mfaransa huyo msimu wa 1996-97, anasema kwamba anavyodhani kocha huyo mwenye umri wa miaka 66 na ambaye ameinoa klabu hiyo kwa muda wa miaka 20, anatakiwa kuachia nmgazi endapo timu hiyo itashindwa tena mwaka huu kutwaa ubingwa mbele ya washindani wake hao. 

……………………………………………………………………
MECHI ZA LEO KATIKA LIGI MBALIMBALI ZILIZOCHEZWA NA ZA LEO.
ENGLAND.
02/03
02/03
02/03
02/03
02/03
05/03
05/03
05/03
05/03
05/03
……………………………………………..
HISPANIA.
02/03
02/03
03/03
03/03
03/03
05/03
05/03
05/03
05/03
06/03
……………………………………………..
UJERUMANI.
02/03
02/03
02/03
02/03
02/03
Borussia dotmund
05/03
05/03
05/03
05/03
Bayer Leverkusen
05/03
MSIMAMO WA LIGI MBALI MBALI.
HISPANIA.

Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Barcelona
27
22
3
2
74
22
52
69
2
Atletico de Madrid
27
19
4
4
39
11
28
61
3
Real Madrid
27
17
6
4
74
26
48
57
4
Villarreal
27
15
8
4
33
18
15
53
5
Sevilla
27
12
8
7
38
28
10
44
6
Celta de Vigo
27
12
6
9
39
44
-5
42
7
Athletic Club
27
12
5
10
42
36
6
41
8
Eibar
27
10
6
11
40
36
4
36
9
Valencia CF
27
8
10
9
32
30
2
34
10
Real Sociedad
27
9
7
11
36
38
-2
34
11
Malaga
27
8
8
11
24
25
-1
32
12
Deportivo de La Coruna
27
6
14
7
34
36
-2
32
13
Real Betis
27
7
10
10
24
36
12
31
14
Espanyol
27
8
4
15
26
53
27
28
15
Las Palmas
27
7
6
14
29
40
11
27
16
Getafe
27
7
5
15
26
44
18
26
17
Rayo Vallecano
27
6
8
13
37
58
21
26
18
Granada CF
27
7
5
15
29
51
22
26
19
Sporting de Gijon
27
6
6
15
30
48
18
24
20.
Levante
27
5
5
17
25
51
26
20
…………………………………………………

German Bundesliga | LOGS


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
FC Bayern Munchen
24
20
2
2
59
13
46
62
2
Borussia Dortmund
24
18
3
3
59
25
34
57
3
Hertha BSC
24
12
6
6
33
24
9
42
4
Borussia Monchengladbach
24
12
3
9
49
40
9
39
5
1. FSV Mainz 05
24
12
3
9
34
30
4
39
6
FC Schalke 04
24
11
5
8
34
31
3
38
7
Bayer 04 Leverkusen
24
10
5
9
33
30
3
35
8
VfL Wolfsburg
24
9
7
8
36
31
5
34
9
FC Ingolstadt 04
24
8
7
9
18
25
-7
31
10
1. FC Koln
24
7
9
8
25
30
-5
30
11
Hamburger SV
24
7
7
10
28
34
-6
28
12
VfB Stuttgart
24
8
4
12
35
48
-13
28
13
FC Augsburg
24
6
7
11
27
35
-8
25
14
SV Darmstadt 98
24
6
7
11
25
38
13
25
15
SV Werder Bremen
24
6
6
12
31
47
16
24
16
Eintracht Frankfurt
24
5
8
11
27
39
12
23
17
TSG 1899 Hoffenheim
24
4
9
11
25
37
12
21
18
Hannover 96
24
5
2
17
21
42
21
17
……………………………………………………….

English Barclays Premier League | LOGS


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Leicester City
28
16
9
3
51
31
20
57
2
Tottenham Hotspur
28
15
9
4
49
22
27
54
3
Arsenal
28
15
6
7
44
28
16
51
4
Manchester City
27
14
5
8
48
31
17
47
5
Manchester United
28
13
8
7
37
26
11
47
6
West Ham United
28
12
10
6
42
31
11
46
7
Stoke City
28
12
6
10
30
33
-3
42
8
Liverpool
27
11
8
8
41
36
5
41
9
Southampton
28
11
7
10
35
28
7
40
10
Chelsea
28
10
9
9
42
38
4
39
11
Everton
27
9
11
7
49
36
13
38
12
Watford
28
10
7
11
29
29
0
37
13
West Bromwich Albion
28
9
9
10
29
36
-7
36
14
Crystal Palace
28
9
6
13
31
37
-6
33
15
Bournemouth
28
8
8
12
32
44
12
32
16
Swansea City
28
7
9
12
27
37
10
30
17
Sunderland
28
6
6
16
34
53
19
24
18
Norwich City
28
6
6
16
31
53
22
24
19
Newcastle United
27
6
6
15
27
50
23
24
20
Aston Villa
28
3
7
18
22
51
29
16
…………………………………………………..


Italian Serie A | LOGS


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Juventus
27
19
4
4
48
15
33
61
2
Napoli
27
17
7
3
55
22
33
58
3
Roma
28
16
8
4
59
29
30
56
4
Fiorentina
28
16
5
7
49
31
18
53
5
Internazionale
27
14
6
7
34
25
9
48
6
Milan
27
13
8
6
39
28
11
47
7
Sassuolo
27
10
11
6
34
31
3
41
8
Lazio
27
10
7
10
34
36
-2
37
9
Bologna
27
10
5
12
29
31
-2
35
10
Chievo
27
9
7
11
32
36
-4
34
11
Empoli
27
9
7
11
33
40
-7
34
12
Torino
27
8
8
11
33
34
-1
32
13
Atalanta
27
7
9
11
26
31
-5
30
14
Udinese
27
8
6
13
24
40
-16
30
15
Genoa
27
7
7
13
27
32
-5
28
16
Sampdoria
27
7
7
13
39
46
-7
28
17
Palermo
27
7
6
14
27
47
20
27
18
Frosinone
27
6
5
16
26
53
27
23
19
Carpi
27
4
9
14
24
44
20
21
20
Verona
27
2
12
13
24
45
21
18
………………………………………

French Ligue 1 | LOGS


Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Paris Saint-Germain
28
23
4
1
68
15
53
73
2
Monaco
29
13
12
4
42
32
10
51
3
Caen
29
13
4
12
32
38
-6
43
4
Lyon
28
12
6
10
40
30
10
42
5
Nice
28
11
8
9
39
32
7
41
6
Rennes
28
10
11
7
36
33
3
41
7
St Etienne
28
12
5
11
33
32
1
41
8
Nantes
27
10
10
7
26
24
2
40
9
Angers
28
10
8
10
29
29
0
38
10
Lorient
28
9
10
9
40
41
-1
37
11
Bastia
27
11
4
12
27
29
-2
37
12
Bordeaux
28
9
10
9
37
43
-6
37
13
Marseille
27
8
12
7
37
28
9
36
14
Montpellier
28
10
5
13
36
33
3
35
15
Lille
28
7
13
8
21
23
-2
34
16
Guingamp
28
8
8
12
33
40
-7
32
17
Reims
28
8
8
12
32
39
-7
32
18
GFC Ajaccio
27
6
10
11
28
38
10
28
19
Toulouse
28
4
10
14
27
47
20
22
20
Troyes
28
2
8
18
20
57
37
14
MWISHOOOOOOOOOO.


Similar Videos