Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

KAMA ULIKOSA KUPATA HABARI ZA MICHEZO KWA WIKI INAYOISHA LEO HIZI HAPA

Views:
Video Information

MAKALA YA MICHEZO NA BURUDANI 
……..MUKHTASARI WAKE……..
- Kazi ipo Uwanja wa Taifa kesho Jumapili wakati Yanga itakapoivaa Friends Rangers katika michuano ya Azam Sports au Kombe la FA.
- Kiungo kinda wa Simba, Said Ndemla, anatarajia kwenda kufanya majaribio kwenye kikosi cha TP Mazembe ya DR Congo ili kusaka nafasi ya kucheza soka katika klabu hiyo.
- Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambi rambi kwa klabu ya Tanzania Prisons inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kufuatia kifo cha Mwenyekiti wake Hassan Mlilo kilichotokea  katika hospital ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
KIMATAIFA.
- Manchester United wamekanusha habari kwamba walikutana na kuzungumza na meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola.
HABARI KAMILI ZA KIMICHEZO.
Kazi ipo Uwanja wa Taifa kesho Jumapili wakati Yanga itakapoivaa Friends Rangers katika michuano ya Azam Sports au Kombe la FA.

Friends Rangers timu ya Ligi Daraja la Kwanza, imepanga kuwatumia mastraika wake hatari ambao wamewahi kucheza katika klabu za Sweden na Dubai ili kuhakikisha wanashinda mechi hiyo.


Kocha wa Friends Rangers, Herry Mzozo, alisema atamtumia straika, Juma Mgaya ambaye amewahi kucheza nchini Sweden na Cosmas Lewis ‘Balotelli’ aliyewahi kucheza Dubai.


 “Hao Yanga ni timu kongwe tu na siyo timu ya kututisha sisi, tuna mikakati yetu ya kuhakikisha tunashinda, ndiyo maana tunao hao wachezaji,” alisema Mzozo. 


Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, alisema: “Tumejiandaa vizuri kwa mechi hii, labda niseme wazi tu kwamba tutatumia kikosi cha pili kwa lengo la kupumzisha wachezaji wetu.”


Katika michuano hiyo, leo Jumamosi Simba itacheza na Burkina Faso kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakati jijini Mwanza, Pamba itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.



Mjini Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Ndanda FC itacheza na Mshikamano FC. Mechi nyingine za kesho Jumapili, Njombe Mji itacheza na Prisons kwenye Uwanja wa Amani, Njombe na Stand United itaivaa Mwadui FC kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.
…………………………………………………..
Kiungo kinda wa Simba, Said Ndemla, anatarajia kwenda kufanya majaribio kwenye kikosi cha TP Mazembe ya DR Congo ili kusaka nafasi ya kucheza soka katika klabu hiyo.


Hivi karibuni, Watanzania, Abuu Ubwa na Haruna Chanongo walienda kufanya majaribio Mazembe ambapo kwa sasa hatua iliyobaki ni makubaliano kati yao na Stand United inayowamiliki wachezaji hao.


Jamali Kisongo ambaye ni meneja wa Mbwana Samatta, amesema kuwa, ataendelea kuwasaidia wachezaji wa Tanzania kupenya kwenye soka la kimataifa kama Samatta.


“Nimewapeleka Ubwa na Chanongo kufanya majaribio TP Mazembe, kinachoendelea sasa ni mazungumzo kati ya Stand na Mazembe kwa ajili ya usajili.


“Ndemla naye nitampeleka akafanye majaribio kule, lengo ni kuwasaidia wachezaji wengi wa hapa nyumbani kupata fursa ya kucheza soka nje ya mipaka ya nchi yetu.


“Mbali na Ndemla, pia kiungo wa Mtibwa (Sugar), Mohammed Ibrahim, naye anahitajika kule baada ya awali safari yake kushindikana,” alisema Kisongo.
………………………………………………………………
Hii ndiyo habari ya mjini pale mjini Shinyanga, kwmaba straika Elias Maguri wa Stand United hana nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu yake jambo linalompa ugumu kupambana na Amissi Tambwe wa Yanga kuwania ufungaji bora.


Katika Ligi Kuu Bara hadi sasa, Tambwe anaongoza kwa ufungaji akiwa na mabao 13, akifuatiwa na Hamis Kiiza wa Simba mwenye mabao 10 huku Maguri akiwa na mabao tisa sawa na Donald Ngoma wa Yanga.


Maguri amepoteza nafasi kikosi cha kwanza baada ya kuvurugana na kocha wake, Patrick Liewig siku chache baada ya kung’ara na kikosi cha Taifa Stars na Kilimanjaro Stars.


Taifa Stars ilipocheza dhidi ya Algeria mwaka jana kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018, Maguri aliifungia Stars bao moja katika sare ya mabao 2-2 jijini Dar es Salaam. 


Maguri alisema; “Sina nafasi kikosi cha kwanza, hivyo siwezi tena kuwania tuzo ya mfungaji bora na nawaachia vita hiyo, Tambwe na Kiiza.


“Kocha hataki kunipanga kwa sababu eti mimi ni staa na yeye hataki mchezaji staa katika kikosi chake jambo ambalo siyo kweli, Tambwe na Kiiza wao wana nafasi katika vikosi vyao, hivyo wanaweza kufanya vizuri.” 



Alipotafutwa Liewig, alisema; “Mtu hajitumi nimpe nafasi ili iweje? Tangu aliporudi amekuwa wa kawaida mno kikosini.”
…………………………………………………………………..
Uongozi wa klabu ya Friends Rangers, umesema klabu ya Yanga isitarajie mteremko katika mchezo wao wa kutania Kombe la  FA, utakaofanyika keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Ofisa habari wa klabu hiyo Asha Kigundula, amesema licha ya kujua wanacheza na timu inayoongoza Ligi Kuu, wao wamejipanga kushinda mchezo huo.

"Kikosi chetu kipo kambini na kila kitu kinakwenda vizuri kabisa kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo ya Jumapili.


"Kikubwa nilitaka kuwatahadharisha Yanga, wasitarajie mteremko eti kwa kuwa wanakuja kucheza na Friends Rangers. Tuko vizuri na tutawashangaza," alisema Kigundula akionyesha imani kubwa na kikosi chake.

Kigundula alisema Yanga isiifananishe timu yao na timu iliyoifunga mabao 5-0, hivyo kwao wanakuja kamili kuhakikisha wanaitoa na kuendelea katika hatua inayoufuata.

"Tumejipanga kushinda hivyo Yanga ifute ndoto za kutufunga kwa sababu juzi ilipata ushindi wa mabao mengi, wameifunga timu ambayo ilipanda kizengwe wasubili waone tutakachowafanya"alisema Kigundula

Hata hivyo Kigundula amewataka mashabiki wa timu hiyo wajitokeze kwa wingi katika mchezo wao ili waweze kuwapa hali zaidi wachezaji wao wacheze kwa kujiamini.
……………………………………………………….
Kikao cha Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kilichoketi jana na kupitia taarifa mbalimbali za michezo ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa pili, kimeiondoa klabu ya Ashanti United kwenye michuano hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na klabu ya Africa Lyon.


Katika kikao hicho kamati ilipokea malalamiko ya klabu ya Africa Lyon dhidi ya Ashanti United kwa kumchezesha mchezaji Enock Balagashi kwa jina la Awesu Abdu katika mchezo namba 3, uliochezwa tarehe 15 Disemba, 2015 na Ashanti kuibuka na ushindi kwa mikwaju ya penati.


Kamati imejiridhisha baada ya kupitia taarifa ya mchezo huo, na kubaini klabu ya Ashanti United ilifanya udanganyifu wa kumtumia mchezji huyo kwa jina la mchezaji mwingine, huku ikitambua kuwa kufanya hivyo ni makosa na mchezo huo ulikuwa ukionyeshwa moja kwa moja kwenye kituo cha luninga cha Azamtv.


Kwa mujibu wa Kanuni no. 41 (12) ya uthibiti wa viongozi kufungiwa miezi 12, Kamati imemfungia Katibu Mkuu wa klabu ya Ashanti kutojihusisha na masuala ya mpira wa miguu kwa kipindi cha miezi 12.


Aidha Kamati pia kwa kutumia kanuni ya 37 (15) ya udhibiti wa wachezaji, mchezaji Enock Balagashi amefungiwa kwa kucheza mpira kwa kipindi ch amiezi 12 na faini ya shilingi laki tatu (300,000).


Kamati imevitaka vilabu vya ngazi zote nchini kuheshimu vipindi vya usajili kwa kufanya usajili wa wachezaji watakaowatumia, na kuheshimu kanuni na taratibu zinazoendesha michuano inayoandaliwa na TFF.



Africa Lyon watacheza dhidi ya Azam FC mznguko wa tatu siku ya Jumatatu katika Uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
………………………………………………………………………………………….
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambi rambi kwa klabu ya Tanzania Prisons inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kufuatia kifo cha Mwenyekiti wake Hassan Mlilo kilichotokea jana katika hospital ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.


Katika salamu zake, Malinzi amewapa pole familia ya marehemu Hassan Mlilo, ndugu, jamaa, marafiki na klabu ya Tanzania Prisons, na kusema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini amesema TFF ipo pamoja nao katika kipindi hichi kigumu cha maombolezo.



Mwili wa marehemu Hassan Mlilo unatarajiwa kusafirishwa leo mchana kuelekea mkoani Mbeya, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho katika mji wa Rujewa mkoani humo.
………………………………………………………………………
Mshambuliaji Mbwana Samatta, juzi Jumatano amerejea katika klabu yake ya TP Mazembe ya DR Congo, amejikuta katika mazingira mapya baada ya kukabidhiwa kwa kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Togo, Hubert Velud.


Velud raia wa Ufaransa ambaye pia aliwahi kuwa kocha wa Paris FC mwaka 1995 mpaka 1999, ambayo kwa sasa inashiriki inashiriki Ligue 2 ya Ufaransa, ametua Mazembe akitokea Klabu ya USM Alger ya Algeria na kuchukua mikoba ya Mfaransa mwenzake Patrice Carteron.


Samatta ambaye alikuwa mbioni kutua Genk ya Ubelgiji, dili lake lilikwama kutokana na mmiliki wa Mazembe, Moise Katumbi kugoma kumuachia.


Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo, ameliambia Championi Ijumaa kuwa nyota huyo amerejea katika kituo chake cha kazi ili kuweza kuongeza msukumo wa kuondoka kutokana na Katumbi kutokuwa tayari kupata hasara kutoka kwa straika huyo.


“Samatta tayari amerejea Congo…Hili litasaidia kumpa presha Katumbi ya kumuuza maana hatoweza kukubali apate hasara ya jumla, hivyo atalazimika kukubali matakwa ya mchezaji mwenyewe.



“Lakini pia tumeacha nafasi kwa serikali nayo ione inaweza kutusaidia vipi kwa kuwasiliana na Katumbi ili kuweza kulimaliza jambo hili,” alisema Kisongo.
……………………………………………………………..
Baadhi ya mashabiki wa Mbeya City wamemtaka kocha mkuu wa timu hiyo Meja Mstaafu Abdul Mingange,  pamoja na uongozi kuachia ngazi kutokana na matokeo mabaya ambayo timu hiyo inayapata.


Tangu Mbeya City ilipoanza kuwa chini ya Mingange imeshinda michezo miwili, imefungwa michezo minne, sare nne.


Kutokana na matokeo hayo mashabiki wengi wamekuwa wakionyesha kuwa na hasira dhidi ya viongozi.


Wakizungumza na hekaheka viwanajani kwa nyakati tofauti mashabiki hao walilalama kuwa matokeo hayo yakiendelea hivyo, basi kuna uwezekano mkubwa wa timu kushuka daraja, hivyo ni bora hatua zikachukuliwa mapema.


Upande wa uongozi wa Mbeya City kupitia kwa katibu mkuu, Emmanuel Kimbe, alisema watakaa na benchi la ufundi kujua tatizo na kuwataka mashabiki kutulia. 
…………………………………..
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limejitoa katika sakata la aliyekuwa nahodha wa Taifa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ likisema kuwa suala hilo anahusika nalo kocha mkuu wa timu hiyo, Boniface Mkwasa.

Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa alisema suala hilo hawatakiwi kuliingilia na badala yake wamemuachia kocha mwenyewe.


“Tunashangaa suala hilo kuchukuliwa kubwa na kukuzwa na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na isitoshe wakati Cannavaro anapewa unahodha hakupewa barua zaidi ya kuonekana akivaa kitambaa uwanjani.



“Pia maamuzi ya kuichezea au kutoichezea Stars tumemuachia kocha mwenyewe anayeona mchezaji yupi anafaa kuichezea Stars,” alisema Mwesigwa.
……………………………….

Kweli sasa Yanga hawataki “utani na kazi” baada ya kurejea kileleni kwa kukausha maji ya mto ruvuma kwa kuitwanga Majimaji ya Songea kwa mabao 5-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Wakati Yanga ikirejea kileleni kwa idadi kubwa ya mabao ya kufunga na machache ya kufungwa, mshambuliaji wake Amissi Tambwe, amepiga hat trick.


Tambwe raia wa Burundi amefunga mabao matatu huku mawili yakifungwa na Wazimbabwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko aliyefunga la kwanza.


Kamusoko alifunga bao la kwanza lililodumu hadi mapumziko na baadaye Yanga ikacharuka kipindi cha pili na kuwatandika vijana wa Kalimangonga Ongalla aliyewahi kuichezwa Yanga.



Deus Kaseke leo alikuwa mwiba kwa mabeki wa Majimaji akishirikiana na beki wa kulia, Juma Abdul.
…………………………….
KIMATAIFA..
Liverpool imeamua kumfungia kazi mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk Alex Teixeira kocha Jurgen Klopp akijaribu kufanya usajili wa kwanza tangu alipotua Anfield. Majogoo hao wa England wako tayari kulipa pauni milioni 24.5 kwa saini ya mchezaji huyo wa miaka 26. Hata hivyo kilabu hiyo ya Ukraine inasema kuwa Texeira ambaye pia amehusishwa na uhamisho wa kwenda Chelsea, atagharimu pauni milioni 39. Klopp anapanga kuimarisha safu yake ya ushambuliaji huku Danny Ings,Divock Origi na Daniel Sturridge wakiwa wanauguza majeraha. Wakati Christian Benteke aliyeighrimu kilabu hiyo pauni milioni 32 akisalia kama mshambuliaji pekee,Liverpool imefunga mabao 25 pekee katika mechi 22 za ligi msimu huu. Shakhtar ambao wako katika mazoezi mjini Florida wanamthamini sana Texeira. Amefunga mabao 22 katika mechi 15 na mabao manne katika mechi 10 za klabu bingwa Ulaya msimu huu. Alianza kuchezea kilabu ya Vasco da Gama kabla ya kuelekea Shakhtar mwaka 2010.

………………………………………………
Manchester United wamekanusha habari kwamba walikutana na kuzungumza na meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola kuhusu uwezekano wake kuwa meneja wao. Hapo kabla tovuti ya France Football ilifichua hilo na kusema mkutano huo ulifanyika mjini Paris lakini United wamesema habari hizo si za kweli. Meneja wa sasa wa United Louis van Gaal anakabiliwa  na shinikizo la kutemeshwa kibarua chake baada ya klabu hiyo kutofanya vyema Ligi Kuu Uingereza na Ulaya. Guardiola tayari ameshaweka wazi kuwa atahamia Uingereza msimu ujao huku Manchester City na Manchester United zikitajwa kugombania huduma yake. Guardiola, 45, anataondoka Bayern Munich majira yajayo ya joto na amesema amepokea maombi kutoka kwa klabu kadha za Uingereza.

………………………………………………
Javier Mascherano amehukumiwa kwenda jela kwa mwaka mmoja jela pamoja na faini ya pauni 625,000 kwa kukwepa kodi mara mbili. Hata hivyo mwanasheria wa difenda wa Barcelona na Argentina David Aineto ana matumaini kuwa mteja wake hatakwenda jela kufuatia jaribio lao la kutaka adhabu hiyo igeuzwe na kuwa faini. Nyota huyo anadaiwa kutumia ulaghai kukwepa kulipa kodi ya jumla ya pauni 1.15. Mascherano, 31, awali alikiri makosa mawili ya kukosa kutangaza mapato yake kamili ya 2011 na 2012. Kwa mujibu wa taratibu za Hispania, mtu aliyehukumiwa kifungo cha miaka miwili kurudi chini, anaruhusiwa kulipa faini, labda tu iwe amehukumiwa kwa makosa ya kutumia nguvu au ujangili. Nyota huyo wa zamani wa Liverpool na West Ham aliandika kwenye Twitter: “Mimi ni mchezaji soka ya kulipwa, sifahamu sana masuala ya ushuru na sheria. “Kuangazia masuala hayo magumu, mimi huwategemea watu wengine. “Katika maisha yangu ya uchezaji, nimekuwa mtu mwaminifu, wa kuwajibika na anayeheshimu wachezaji wengine na klabu ambazo nimechezea.” Mascherano tayari alishalipa kiasi kiasi alichokwepa (pauni milioni 1.15) kabla adhabu haijatolewa. Alihukumiwa kwenda jela kwa miezi minne kwa kosa la kwanza huku kosa la pili likimpa hukumu ya mieiz minane.

…………………………………..
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uruaguay anayecheza katika klabu ya Barcelona, Luis Suarez amesema kwamba hatatizwi na kauli kwamba hakuwa chaguo la kwanza la timu hiyo wakati anasajiliwa. Nyota huyo aliyehamia kutoka kikosi cha Liverpool amesema kwamba hata kama hakuwa anatakiwa sana na wenye timu, lakini sasa anajua kwamba wataumiza vichwa tena wakisikia anataka kuhama. “Sijali kama sikuwa chaguo lao, achana na habari hiyo. Tuseme sasa nataka kuhama, utasikia habari hiyo kwamba ninatakiwa kuwa wa kwanza kuuzwa? Najua hakuna anayetamani niondoke leo na hiyo ndio tofauti na maneno na vitendo,” amesema. Mkurugenzi wa michezo wa zamani wa Barcelona, Andon Zubizarreta alisema klabu yake iliamua kumsajili Luis Suarez kwa sababu chaguo lao la kwanza la mchezaji waliyemwitaji hakuwa anauzwa. Ikasemwa kwamba kauli hii imewashangaza wengi ila ndio ukweli, Luiz Suarez hakuwa chaguo la kwanza katika usajili wa Barcelona. Suarez mwenyewe amesema kama hakuwa chaguo sahihi kwa FC Barcelona sasa ndio ametua na anaendelea kufanya vema, watasema nini tena? Kumbe mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero ndio lilikuwa chaguo la kwanza kwa Barca katika mpango wao wa kupata safu ya ushambuliaji itakayokuwa na makali kama wapinzani wao, Real Madrid. Zubizarreta juzi ameeleza kwamba Barca ilimuhitaji Aguero aungane na Lionel Messi na Naymar kuunda safu ya ushambuliaji itakayoendana na kasi ya BBC ya Real Madrid. Alisema: “Tulikuwa na machaguo machache, chaguo letu la kwanza halikuwa Suarez, yeye mwenyewe anajua hili.”  “Tulijaribu kumsaini Aguero lakini ikashindikana na mpaka kufikia hapo hatukuwa na uamuzi mwingine wa kufanya zaidi ya kumsajili Suarez.” Zubizarreta pia anasema, suala la Suarez kufungiwa kwa kumng’ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini liliwapa nafasi zaidi wao kwa sababu timu nyingine ziliamua kuachana na mipango yao ya kumtaka mchezaji huyo. Aliongeza: “Wakati tupo kwenye majadiliano ya Liverpool likatokea lile sakata la Suarez na Chiellini.” “Suala hili lilileta mashaka makubwa kwenye vichwa vya viongozi wa timu nyingine waliokuwa wakimtaka Suarez.” “Tabia yake ilikuwa kwenye mjadala mkubwa na hakuna aliyekuwa anajua atafungiwa kwa muda gani, muda huohuo ndipo nafasi ya kumsajili ikawa kubwa na tukakamilisha kila kitu.”

……………………………….
NYOTA wa klabu ya Atletico Madrid, Matias Kranevitter amekiri tetesi za kuwaniwa na timu kadhaa za premier, lakini Chelsea na Manchester City ndio wanaongoza mbio hizo. Lakini matajiri wa jiji la London, Chelsea wameongeza kasi ya kumwania kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa ajili ya kutua darajani mwezi huu wa Januari. Awali Kranevitter amekuwa akihusishwa na tetesi za kutaka kujiunga kwa Washika Mitutu wa jiji la London na Arsene Wenger ameweka mezani ofa kwa ajili yake. Lakini kocha wa sasa wa mpito wa matajiri hao, Guus Hiddink inasemekana ameingilia kati dili hilo na anapambana kuhakikisha kiungo huyo anatua katika kikosi cha Stanford Bridge. Akinukuliwa, kiungo huyo amesema ndoto zake za kutua Emirates zinaweza kuyeyuka kwa sababu Hiddink ameongeza kasi ya mazungumzo. “Nimekuwa nikisikia malengo ya Hiddink kwangu na kadri ninavyotambua mpango uko hivyo.” “Ni kati ya makocha wazuri duniani wanaovutua kufanya kazi nao, kila mchezaji anaota ndoto ya kufundishwa na mwalimu wa mfano wake.” “Kwa nyakati tofauti nimekuwa nikifundishwa na makocha wengine. Kama kuna siku inatokea Napata nafasi ya kufanya kazi chini yake nitakuwa na furaha kubwa.” “Lakini kwa sasa bado nipo Atletico. Najisikia furaha kuwa hapa, hakuna tatizo kuwa hapa.” “Kucheza katika timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa ni kati ya malengo yangu pia. Kila mchezaji anaota mafanikio kama hayo.” “Ninataraji kuwa katika kiwango hicho cha mafanikio, ninaamini kuna siku nitafikia hatua hiyo, ni suala la kusubiri kuona,” alisisitiza Matias Kranevitter.

……………………………………………………..
HABARI zinazomhusu mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani, Ilkay Gundogan zinatatanisha. Awali, mwanzoni mwa mwaka huu imedaiwa kwamba mchezaji huyo hajausaini mkataba wa muda mrefu na Borussia Dortmund akitaka ahamie katika klabu mpya kwenye Ligi ya Bundesliga. Hata hivyo, habari mpya ni kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye amekuwa katika klabu ya Dortmund tangu mwaka 2011, anataka kumfuata kocha wake aliyekuwa nae kwa muda mrefu, Jurgen Klopp ambaye sasa anakinoa kikosi cha Liverpool. Gundogan ameliambia gazeti la Bild kuwa hajafanya uamuzi wowote na lazima atasaini kila kitu kwa sababu urefu ya taaluma ya mtu una ukomo. Ameongeza kuwa kila kitu kingali wazi na kuwa mkataba wake ujao utakuwa mrefu na sio wa mwaka mmoja tu. Amesema kwamba anataka kulinda kiwango chake, lakini haoni kwamba kuna timu ambayo inaweza kusaidia kikosi chake zaidi ya Liverpool kwa sababu katika kikosi hicho kuna mtu ambaye anajua kwamba anamfaa. Na wala hafichi, anamtaja mtu huyo kuwa ni Klopp ambaye anadai kuwa alikuwa nae katika kikosi hicho kwa kiwango cha mtu na kaka yake na alimsaidia sana. “Alikuwa kama kaka au baba yangu hapa, nikienda Uingereza kwa vyovyote vile sitakwenda Arsenal au Man United, sitakwenda Chelsea au Man City, nitakwenda Liverpool kwa sababu ya Klopp,” alisema.

………………………………………………………
ALEX Sandro tayari ameonyesha azma ya kutaka kuondoka Juventus ili akatafute maisha mbele ya safari katika usajili huu wa mwezi Januari. Tena amekwenda mbali zaidi kwa kuitaja timu anayoipenda kwenda kukipiga na kwamba mapenzi yake ni kuvaa uzi wa Manchester City. Mshambuliaji huyo ameuomba uongozi wa klabu ya Juve licha ya kumruhuasu aondoke, anataka kwenda kutimiza azma yake ya kucheza Ligi ya premier.  Sandro ambaye msimu huu amekuwa katika kiwango bora akiwa na Juve, ameweka bayana ndoto yake ya kucheza katika Ligi iliyo na mashabiki wengi. “Nina malengo ya kutimiza ndoto ya kwenda kucheza katika Ligi ya premier.” “Ninataka kuona ninalinda kipaji changu, sitaki kuwa msiri juu ya mimi kuondoka hapa.” “Soka ni kazi ninayokwenda kufanya popote, soka ni mchezo wa kuangalia leo na kesho, huu ndio msimamo wangu kwa sasa,” alisema Sandro. “Manchester City ni klabu ninayoipenda kwa ajili ya soka langu la baadae, ninaamini nina nafasi ya kucheza nikiwa kule na kutimiza ndoto yangu hii,” alisisitiza Sandro raia wa Brazil.

………………………………………………………..
PARIS Saint - Germain sasa ipo tayari kuweka mezani kitita cha pauni mil. 18 kwa ajili ya kumnasa straika wa Swansea, Bafetimbi Gomis, hii ni kwa mujibu wa Sky Sports. Straika huyo raia wa Ufaransa ameingia katika rada za PSG inayotaka kuendeleza ubabe katika Ligi ya Italia. Dalili za Bafetimbi kutua katika kikosi cha mabingwa watetezi zinatiwa nguvu na taarifa za kwamba kiwango chake kwa sasa kimewavutia baadhi ya mawakala wa klabu mbalimbali. Tayari PSG wameteta na wakala wa nyota uyo na kwamba hata Swansea wenyewe wamethibitisha kuwepo kwa pilika kuhusiana na straika huyo. Wakitambua hilo, PSG wamemtengea kiungo huyo kitita cha pauni mil. 18 wakiongeza dau waliloliweka awali ambalo lilikuwa pauni mil. 15. PSG walimthaminisha Mfaransa huyo kuwa ni wad au la mil. 18 ingawa wameonyesha dalili za kukubalim kushusha kiwango. Swansea pamoja na kuweka bayana thamani ya mchezaji huyo, wamethibitisha kuwa straika huyo ni miongoni mwa wachezaji wanaotakiwa na klabu mbalimbali za Ulaya. “Bafetimbi anawindwa na timu nyingi za Ulaya, lakini nataka acheze katika kikosi ambacho atapambana na kudumu.” “Ni mchezaji mwenye ofa nyingi, ila ni jambo la kusubiri kuona ifikapo kipindi cha usajili kikifika mwisho.”

…………………………………………………
STAA wa Arsenal, Mesut Ozil amesema kwamba hatalazimisha kuongeza mabao zaidi katika timu hiyo na badala yake ataendelea na kasi yake ya kuwatengenezea wenzake. Kiungo huyo mshambuliaji kwa sasa ni mmoja kati ya nyota wanaoongoza kuwatengenezea mabao wenzake na kwa sasa ndiye anayeongoza kufanya kazi hiyo kwenye michuano ya Ligi Kuu England akiwa ametoa pasi 16. Kwa ujumla Ozil ameshafunga mabao matatu katika mechi 20 alizoichezea Arsenal msimu huu, lakini Mjerumani huyo anasema kwamba anaona hakuna haja ya kuongeza idadi hiyo ya mabao yake. “Mwisho wa siku nitajaribu kupata mafanikio kwa kila mechi ili tuweze kushinda,” staa huyo aliuambia mtandao wa chama cha soka nchini Ujerumani. “Haijalishi kama nitafunga bao ama nitatoa pasi kwani jambo la msingi ni kwamba tumeshinda. Sioni kama itakuwa na mana zaidi kama nitaelekeza nguvu zangu katika kufunga mabao ama kuwa mchoyo nikiwa mbele ya lango,” aliongeza staa huyo. Ozil alisema kwamba alichokipania ni kuipaisha Arsenal msimu huu pamoja na timu ya taifa ya Ujerumani katika fainali za Mataifa ya Ulaya (Euro 2016).

……………………………………………………
MWANASOKA wa zamani, Roberto Carlos amepuuzia taarifa zinazodai kuwa nyota wa Barcelona, Neymar kwamba anaweza kuhamia kwa mahasimu wao, Real Madrid. Beki huyo wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil alisema kwamba anaweza kumhamisha Neymar kutoka Barcelona kwenda Real Madrid endapo atapewa jukumu la kuinoa klabu hiyo. Jumapili Neymar alikuwa kwenye ubora wake tena akiwa na Barcelona  baada ya kufunga bao moja kati ya sita ambayo timu yake iliibuka na ushindi huo mnono dhidi ya Athletic Bilbao katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga. Hata hivyo, pamoja na ubora huo Carlos anapotezea kama kunaweza kukawepo na uwezekano kwa nyota huyo akaitema Barcelona na kujiunga na Madrid. “Haiwezekani nimewahi kusema hivyo siku za nyuma na watu wamekuwa wakilichukulia jambo hilo kwa umakini kwa sababu Real Madrid huwa inasajili wachezaji bora duniani,” alisema Mbrazil huyo ambaye amerejea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Hispania akiwa na timu yake ya zamani kwa ajili ya maandalizi ya kujiendeleza na kibarua chake cha ukocha. Mshindi huyo wa Kombe la Dunia alisema kuwa ingekuwa jambo jema kama angeweza kufanya kazi chini ya kocha mpya wa klabu hiyo, Zinedine Zidane, lakini akasema kuwa dhamira yake kwa sasa ni kuendelea na mafunzo yake ya ukocha. “Ningefurahi kama kungekuwepo na uwezekano huo lakini nipo mahali hapa kwa ajili ya mazoezi na kujifunza,” alisema Carlos na kuongeza kuwa kwa sasa ameanza mafunzo yake ya ngazi ya juu baada ya kutumia muda wa miaka mitano akifanya hivyo katika nchi za Uturuki, Urusi na India huku akisema ameshajifunza mengi lakini anaomba apewe muda.

………………………………………………………………
STRAIKA wa timu ya Feyenoord, Colin Kazim-Richards amemtetea staa wa Man Utd, Mephis Depay akisema kwamba shutuma zinazomkabili ndizo zitakazomfanya ang’are. Depay aling’ara wakati wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014 baada ya kuiwezesha Uholanzi ushika nafasi ya 13 na huku msimu huu akiibuka mfungaji bora katika Ligi ya Eredevisie akiwa na mabao 22 yaliyoipa ubingwa PSV msimu wa 2014/15. Kiwango hicho ndicho kilichomfanya asajiliwe kwa bei kubwa na Man United, lakini tangu atue kwenye klabu hiyo, staa huyo mwenye umri wa miaka 21 ameshindwa kung’ara na hivyo kuandamwa na shutuma. Hata hivyo, Kazim-Richards ambaye juzi alitemwa kwenye kikosi cha kwanza cha Feyenoord, ambacho juzi kilikuwa kikiivaa PSV bada ya kuwaponda waandishi, anaamini kwamba shutuma hizo ndizo zitakazomjenga staa huyo.

…………………………………………………………..
LIGI KUU YA HISPANIA KUENDELEA TENA WEEKEND HII KWA MECHI KADHAAAAA/
LEO Jumamosi 
Malaga v Barcelona 
Saa 12:00 Jioni 
Espanyol Villarreal 
Saa 2:15 Usiku 
Granada v Getafe
Saa 4:30 Usiku


KESHO Jumapili 
Athletic v Eibar 
Saa 8:00 Mchana
Atletico v Sevilla
Saa 12:00 Jioni 
Deportivo v Valencia 
Saa 2:15 Usiku
Betis v Real Madrid

Saa 4:30 Usiku.



Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Atletico de Madrid
20
15
2
3
30
8
22
47
2
Barcelona
19
14
3
2
50
15
35
45
3
Real Madrid
20
13
4
3
57
19
38
43
4
Villarreal
20
12
4
4
26
16
10
40
5
Celta de Vigo
20
10
4
6
32
30
2
34
6
Eibar
20
9
6
5
32
21
11
33
7
Sevilla
20
9
5
6
28
22
6
32
8
Deportivo de La Coruna
20
6
10
4
27
24
3
28
9
Athletic Club
20
8
4
8
27
28
-1
28
10
Getafe
20
7
5
8
24
28
-4
26
11
Valencia CF
20
5
9
6
25
21
4
24
12
Malaga
20
6
6
8
15
17
-2
24
13
Real Sociedad
21
5
6
10
24
33
-9
21
14
Espanyol
20
6
3
11
18
33
-15
21
15
Real Betis
20
5
6
9
13
28
-15
21
16
Las Palmas
20
4
6
10
19
30
-11
18
17
Sporting de Gijon
20
5
3
12
22
35
-13
18
18
Granada CF
20
4
5
11
21
41
-20
17
19
Rayo Vallecano
20
4
4
12
23
45
-22
16
20
Levante
20
3
5
12
17
36
-19
14

………………………………………………………………..
LIGI KUU ENGLAND KUENDELEA WEEKEND HII
English Barclays Premier League
14:45
Norwich City
v
Liverpool
Carrow Road
17:00
Crystal Palace
v
Tottenham Hotspur
Selhurst Park
17:00
Leicester City
v
Stoke City
King Power Stadium
17:00
Manchester United
v
Southampton
Old Trafford
17:00
Sunderland
v
Bournemouth
Stadium of Light
17:00
Watford
v
Newcastle United
Vicarage Road
17:00
West Bromwich Albion
v
Aston Villa
The Hawthorns
19:30
West Ham United
v
Manchester City
Boleyn Ground
English Football League Championship
14:30
Queens Park Rangers
v
Wolverhampton Wanderers
Loftus Road Stadium
17:00
Birmingham City
v
Ipswich Town
St. Andrew's Stadium
17:00
Bolton Wanderers
v
MK Dons
Macron Stadium
17:00
Brighton and Hove Albion
v
Huddersfield Town
Amex Stadium
17:00
Cardiff City
v
Rotherham United
Cardiff City Stadium
17:00
Charlton Athletic
v
Blackburn Rovers
The Valley
17:00
Fulham
v
Hull City
Craven Cottage
17:00
Leeds United
v
Bristol City
Elland Road
17:00
Middlesbrough
v
Nottingham Forest
Riverside Stadium
17:00
Preston North End
v
Brentford
Deepdale
17:00
Reading
v
Sheffield Wednesday
Madejski Stadium
French Ligue 1
18:00
Paris Saint-Germain
v
Angers
Parc des Princes
21:00
Guingamp
v
Bastia
Stade Municipal de Roudourou
21:00
Lille
v
Troyes
Stade Pierre-Mauroy
21:00
Montpellier
v
Caen
Stade de la Mosson
21:00
Nantes
v
Bordeaux
La Beaujoire-Louis-Fonteneau
21:00
Nice
v
Lorient
Allianz Riviera
German Bundesliga
16:30
1. FC Koln
v
VfB Stuttgart
RheinEnergieStadion
16:30
FC Ingolstadt 04
v
1. FSV Mainz 05
Audi Sportpark
16:30
Hannover 96
v
SV Darmstadt 98
HDI-Arena
16:30
Hertha BSC
v
FC Augsburg
Olympiastadion
16:30
TSG 1899 Hoffenheim
v
Bayer 04 Leverkusen
WIRSOL Rhein-Neckar-Arena
19:30
Borussia Monchengladbach
v
Borussia Dortmund
Borussia-Park
Italian Serie A
19:00
Frosinone
v
Atalanta
Matusa
21:45
Empoli
v
Milan
Carlo Castellani
MultiChoice Diski Challenge
10:00
Bloemfontein Celtic
v
Platinum Stars
Siwelele Park
10:00
Kaizer Chiefs
v
Black Aces
Dobsonville Stadium
10:00
SuperSport United
v
Bidvest Wits
Bidvest Stadium
National First Division
15:30
Moroka Swallows
v
AmaZulu
Dobsonville Stadium
15:30
Witbank Spurs
v
Santos
Puma Rugby Stadium
15:30
FC Cape Town
v
Black Leopards
NNK Rugby Stadium
15:30
Thanda Royal Zulu FC
v
Vasco Da Gama
Umhlathuze Sports Complex
15:30
Baroka FC
v
Mthatha Bucks
Old Peter Mokaba Stadium
Portuguese Primeira Liga
18:00
Moreirense
v
Estoril Praia
Parque Joaquim de Almeida Freitas
18:00
União da Madeira
v
CD Nacional
Estádio do Centro Desportivo da Madeira
20:30
Benfica
v
Arouca
Estadio da Luz
22:45
Paços de Ferreira
v
Sporting Lisbon
Estádio Mata Real
Rwanda 2016 Chan
15:00
Zimbabwe
v
Mali
Rubavu
Spanish La Liga
17:00
Malaga
v
Barcelona
La Rosaleda
19:15
Espanyol
v
Villarreal
RCDE Stadium
21:30
Granada CF
v
Getafe
Los Carmenes
23:05
Rayo Vallecano
v
Celta de Vigo
Campo de Futbol de Vallecas
24 January 2016
Absa Premiership
15:30
Kaizer Chiefs
v
Platinum Stars
Cape Town Stadium
15:30
University of Pretoria
v
Black Aces
Loftus Versfeld Stadium
15:30
Chippa United
v
Ajax Cape Town
Buffalo City Stadium
English Barclays Premier League
15:30
Everton
v
Swansea City
Goodison Park
18:00
Arsenal
v
Chelsea
Emirates Stadium
French Ligue 1
15:00
Monaco
v
Toulouse
Stade Louis II
18:00
Reims
v
St Etienne
Stade Auguste-Delaune
22:00
Lyon
v
Marseille
Stade des Lumieres
German Bundesliga
16:30
Eintracht Frankfurt
v
VfL Wolfsburg
Commerzbank Arena
18:30
FC Schalke 04
v
SV Werder Bremen
VELTINS-Arena
Italian Serie A
13:30
Fiorentina
v
Torino
Artemio Franchi
16:00
Internazionale
v
Carpi
Giuseppe Meazza
16:00
Lazio
v
Chievo
Olimpico
16:00
Palermo
v
Udinese
Renzo Barbera
16:00
Sampdoria
v
Napoli
Luigi Ferraris
16:00
Sassuolo
v
Bologna
Città del Tricolore
16:00
Verona
v
Genoa
Marc'Antonio Bentegodi
21:45
Juventus
v
Roma
Juventus Stadium
MultiChoice Diski Challenge
10:00
Chippa United
v
Golden Arrows
Wolfson Stadium
10:00
University of Pretoria
v
Polokwane City
Loftus Stadium
12:00
Free State Stars
v
Orlando Pirates
Clarens Stadium
12:00
Jomo Cosmos
v
Mamelodi Sundowns
Olen Park Stadium
National First Division
15:30
African Warriors
v
Highlands Park
Charles Mopeli Stadium
15:30
Royal Eagles
v
Mbombela United
King Zwelithini Stadium
Portuguese Primeira Liga
18:00
Belenenses
v
Vitória Guimarães
Estadio do Restelo
20:15
Sporting Braga
v
Rio Ave
Estadio Municipal de Braga
22:30
FC Porto
v
Marítimo
Estadio do Dragao
Rwanda 2016 Chan
16:00
Morocco
v
Rwanda
Amahoro, Kigali
16:00
Ivory Coast
v
Gabon
Stade Huye
Spanish La Liga
13:00
Athletic Club
v
Eibar
San Mames
17:00
Atletico de Madrid
v
Sevilla
Vicente Calderon
19:15
Deportivo de La Coruna
v
Valencia CF
Riazor
21:30
Real Betis
v
Real Madrid
Benito Villamarin
……………………………………………………………..
MSIMAMO WA LIGI MBALI MBALI.
English Barclays Premier League |

Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Arsenal
22
13
5
4
37
21
16
44
2
Leicester City
22
12
8
2
39
26
13
44
3
Manchester City
22
13
4
5
43
21
22
43
4
Tottenham Hotspur
22
10
9
3
38
18
20
39
5
Manchester United
22
10
7
5
28
20
8
37
6
West Ham United
22
9
8
5
34
26
8
35
7
Stoke City
22
9
6
7
24
22
2
33
8
Crystal Palace
22
9
4
9
23
24
-1
31
9
Liverpool
22
8
7
7
25
28
-3
31
10
Southampton
22
8
6
8
31
24
7
30
11
Everton
22
6
11
5
39
32
7
29
12
Watford
22
8
5
9
25
25
0
29
13
West Bromwich Albion
22
7
6
9
22
30
-8
27
14
Chelsea
22
6
7
9
31
34
-3
25
15
Bournemouth
22
6
6
10
26
37
-11
24
16
Norwich City
22
6
5
11
24
38
-14
23
17
Swansea City
22
5
7
10
20
30
-10
22
18
Newcastle United
22
5
6
11
24
39
-15
21
19
Sunderland
22
5
3
14
27
45
-18
18
20
Aston Villa
22
2
6
14
18
38
-20
12


……………………………………………………………………….
German Bundesliga |

Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
FC Bayern Munchen
18
16
1
1
48
9
39
49
2
Borussia Dortmund
17
12
2
3
47
23
24
38
3
Hertha BSC
17
10
2
5
26
18
8
32
4
Borussia Monchengladbach
17
9
2
6
34
30
4
29
5
Bayer 04 Leverkusen
17
8
3
6
25
20
5
27
6
FC Schalke 04
17
8
3
6
23
23
0
27
7
VfL Wolfsburg
17
7
5
5
26
21
5
26
8
1. FSV Mainz 05
17
7
3
7
23
23
0
24
9
1. FC Koln
17
6
6
5
18
21
-3
24
10
Hamburger SV
18
6
4
8
20
25
-5
22
11
FC Ingolstadt 04
17
5
5
7
11
18
-7
20
12
FC Augsburg
17
5
4
8
21
26
-5
19
13
SV Darmstadt 98
17
4
6
7
17
26
-9
18
14
Eintracht Frankfurt
17
4
5
8
21
28
-7
17
15
VfB Stuttgart
17
4
3
10
22
37
-15
15
16
SV Werder Bremen
17
4
3
10
17
32
-15
15
17
Hannover 96
17
4
2
11
18
29
-11
14
18
TSG 1899 Hoffenheim
17
2
7
8
17
25
-8
13


……………………………………………….
Italian Serie A | LOGS

Pos
Team
P
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
1
Napoli
20
13
5
2
41
16
25
44
2
Juventus
20
13
3
4
37
15
22
42
3
Internazionale
20
12
4
4
25
13
12
40
4
Fiorentina
20
12
2
6
37
21
16
38
5
Roma
20
9
8
3
37
23
14
35
6
Milan
20
9
5
6
27
23
4
32
7
Sassuolo
20
8
8
4
25
21
4
32
8
Empoli
20
9
4
7
25
24
1
31
9
Lazio
20
8
4
8
25
29
-4
28
10
Chievo
20
7
6
7
26
22
4
27
11
Torino
20
7
5
8
27
26
1
26
12
Atalanta
20
7
4
9
21
24
-3
25
13
Udinese
20
7
3
10
18
31
-13
24
14
Sampdoria
20
6
5
9
29
32
-3
23
15
Bologna
20
7
2
11
22
27
-5
23
16
Genoa
20
6
4
10
23
26
-3
22
17
Palermo
20
6
3
11
19
33
-14
21
18
Carpi
20
4
5
11
19
35
-16
17
19
Frosinone
20
4
3
13
22
45
-23
15
20
Verona
20
0
9
11
13
32
-19
9
 MWISHOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO.

Similar Videos