Video Information
Mwanamuziki
nyota wa muziki aina ya pop Mariah Carey amempata mchumba na bilionea
kutoka Australia James Packer. Wawili hao walionyesha uhusiano wao hadharani
Juni mwaka jana baada ya kwenda likizoni pamoja nchini Italia.
Bw Packer, 47, ndiye wa nne kwa utajiri Australia, kwa mujibu wa Forbes. Utajiri wake unakadiriwa kuwa zaidi ya A$4.7bn ($3.1bn £2.3bn). Mariah Carey, 45, alichomoa albamu yake ya kwanza 1990 na ni mmoja wa wanamuziki waliofanikiwa zaidi duniani.

Bw Packer aliyerithi himaya ya kibiashara ya vyombo vya habari Australia kutoka kwa babake Kerry Packer, na sasa anamiliki kasino nyingi. Alitengana na mkewe wa pili, mwanamitindo ambaye pia ni mwanamuziki Erica Baxter, mwaka 2013. Bi Carey alitangaza kuvunjika kwa ndoa yake na mtangazaji wa kipindi cha "America's Got Talent" Nick Cannon mwaka 2014.
……………………………….
Leo kutakuwa na mchezo mkali wa
ligi kuu ya England kati ya mabingwa wateteziChelsea dhidi ya Arsenal.
Msanii Madee ni
mmoja wa mashabiki wa Arsenal ambaye leo atakuwa mpinzani mkubwa wa Chelsea.
Katika
kuonyesha mapenzi yake kwa klabu yake ya Arsenal, kwenye ukurasa wake wa@Instagram Madee ameahidi kuchoma gari yake moja
moto endapo timu yake ya Arsenal itafungwa na Chelsea.
……………………………..
Kama ya
shindano la Miss Tanzania, imetangaza kujiuzulu. Akiongea kwenye mkutano na
waandishi wa habari Ijumaa hii, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya maandilizi ya
shindano hilo Juma Pinto, amedai kuwa sababu ya kujitoa kwenye kamati hiyo ni
kutokana na kushindwa kujua nini majukumu yao na yale ya kampuni inayoyaanda,
Lino Agency.
Amedai kuwa awali iliwekwa wazi kuwa ni kamati hiyo ndiyo itakayoratibu mashindano hayo huku Lino Agency ikibaki kuwa washauri.
Pinto amesema Lino imeendelea kufanya kazi yake lakini wao wakibaki bila kujua kinachoendelea. “Sisi tumeona tuje tuzungumze tu kwamba sisi hatupo huko,” amesema Pinto.
Naye msemaji wa kamati hiyo, Jokate Mwegelo amesema kutokana na ukubwa wa kile Miss Tanzania imefanya kwa wasichana, wasilichukulie kwa wepesi na kiubinafsi.
“Waangalie wasichana wa Tanzania wanawatoaje? Na kuwatoa ni kuhakikisha kwanza misingi ya shindano lenyewe iwe ya kueleweka. Kama misingi haieleweki ndio tunarudi kule kule,” amesema Jokate.
Aliongeza kuwa makosa yaliyojitokeza miaka iliyopita pamoja na malalamiko mengi dhidi ya shindano hilo yanapaswa kufanyiwa kazi.
Kamati hiyo ya Miss Tanzania ilitambulishwa August mwaka ikiwa na wajumbe wafuatao:

1.
Juma
Pinto – Mwenyekiti
2.
Lucas
Rutta – Makamu Mwenyekiti
3.
Doris
Mollel – Katibu Mkuu
4.
Jokate
Mwegelo – Msemaji wa Kamati
5.
Hoyce
Temu – Mjumbe
6.
Mohamed
Bawazir – Mjumbe
7.
Gladyz
Shao – Mjumbe
8.
Magdalena
Munisi – Mjumbe
9.
Shah
Ramadhani – Mjumbe
10.
Hamm
Hashim – Mjumbe
11.
Khalfani
Saleh – Mjumbe
12.
Ojambi
Masaburi – Mjumbe
Wajumbe wa Sekretariet ni:
1.
Dr.Ramesh
Shah
2.
Hidan
Ricco
3.
Yasson
Mashaka
4.
Deo
Kapteni
…………………………………………………………
Kwenye interview aliyofanyiwa mwaka 2015 rapa Will Smith
alisema “Nilianza kupenda na kutaka kurap nikiwa na miaka 12,nilianda kuandika
mashairi mwaka huo kwenye kitabu changu kidogo ”
Kwanini Will Smith hajawahi kutukana kwenye nyimbo zake ?
"Bibi yangu alikuta kitabu changu cha mashairi na kusoma baadhi y nyimbo zangu,hakusema lolote ina alichukua kitabu hicho na kuandika nyuma kabisa kwenye kurasa ya mwisho, Dear Willard ‘Truly intelligent people do not have to use words like this to express themselves. Please show the world that you’re as smart as you think you are’ akimaanisha watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiria hawatumi maneno kama haya kuelezea mitazamo yao, tafadhali onyesha dunia unaakili kama unavyofikiria".
Toka siku hio sikuwahi kupanga kutukana kwenye muziki wangu.

……………………………………………………….
Zari kasema kachoshwa na maneno kuhusu mtoto wao Tiffah, kwanza hawahusu chochote kwa hiyo hata
kama ni mtoto wa Diamond au sio
wake, wanaozungumzia DNA hawamhusu chochote.
Kingine Zari amesema wana mtoto huyo mmoja lakini yuko
tayari hata kuwa na watoto watatu na Diamond.
………………………………………………
Chama cha kutetea haki za wasanii wa muziki wa kizazi kipya
(TUMA) kimeeleza kwamba wasanii wengi wa muziki huo wanakosa haki zao kwa kuwa
si wanachama wa chama hicho.
Katibu Mkuu wa Chama hicho, Samweli Briton, alisema ingawa kwa sasa baadhi ya wasanii wametambua hilo, lakini idadi ya wanaojitokeza inabidi iongezeke ili chama hicho kiwe na wanachama wengi kitakachoongeza nguvu katika utetezi wake.
“Wasanii zaidi ya 30 wameshachukua fomu za kujiunga na chama hicho, akiwemo Vanessa Mdee, Barnaba Boy, Wakazi, Ditto na wengine wengi, hivyo natoa wito kwa wasanii wengine chipukizi na wenye majina kujiunga na chama hiki kabla ya kusubiri matatizo katika kazi zao,’’ alieleza Briton.
Hata hivyo, mmoja wa wasanii hao, Wakazi alisema amekuwa daraja la kuwashawishi wasanii wa muziki huo ili wajiunge na chama hicho wanachoamini kitawasaidia katika harakati zao za kupata mirabaha itakayotokana na kazi zao………..

Alhamisi
Barakah Da Prince amedai kuwa hivi karibuni ataenda Kenya
akiwa na producer wa AM Records, Bob Manecky kwaajili ya kwenda kufanya collabo
na hitmakers wa ‘Uliza Kiatu’ Hartband pamoja na bendi maarufu zaidi Afrika
Mashariki, Sauti Sol.
Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM Jumamosi iliyopita, Barakah amesema lengo lake kubwa la kufanya hivyo ni kubadilisha muziki wake.
Hivi karibuni muimbaji huyo ameachia video ya wimbo wake mpya, Siwezi iliyoongozwa na Kevin Bosco Jr. Msanii huyo pia alitajwa na MTV Base miongoni mwa wasanii 32 wa Afrika wa kuwaangalia mwaka huu.

……………………………………………………………………..
Rapper wa kundi la Weusi, Joh Makini amesema anataka
kufanya video mbili za nyimbo zake za mazani, Kilimanjaro aliyomshirikisha Lady
Jaydee na Nikumbatie aliyofanywa na Fundi Samweli kwa kuwa anaamini nyimbo hizo
zinaweza kufanya vizuri zaidi kimataifa.
Rapper huyo aliyeachia Don’t Bother miezi kadhaa iliyopita, amekiambia kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV kuwa ana imani kazi hizo zinaweza kwenda mbali zaidi.
“Sina kitu ambacho nimekosa katika video zilizopita labda quality ambazo zinapatikana sasa hivi kama ningezipata wakati ule video zingeenda mbali zaidi,” alisema.
“Sina mpango wa kurudia video ya wimbo wowote lakini na mpango wa kufanya video za nyimbo zangu ambazo hazikupata video, Nikumbatie na Kilimanjaro, ni ngoma ambazo nahisi zilistahili kuwa na video kwa sababu ni nyimbo ambazo naona zikipata video zitaenda mbali zaidi. Pia standard ya video zangu nataka iwe inaenda mbele, kwahiyo watu wategemee kazi nzuri.”

………………………………………………………….
Wasanii wa
Nigeria wamekua wa kwanza kwenye stori kubwa au kuvunja rekodi kadhaa kwenye
muziki wanaoufanya ambapo miongoni mwa rekodi walizozivunja ni pamoja na P
Square kufanya kolabo na Rick Ross, Davido na Meek Mill.
Usiku wa
January 20 2016 Taifa la Nigeria limekua taifa la kwanza Afrika kwa kuvunja
rekodi kupitia msanii wake ambaye ni Davido kwa kuingia makubaliano na kuwa
msanii wa kwanza wa Afrika kutia saini ya record deal na kampuni ya sony music.
Sony
Music Entertainment ni kampuni ya maswala ya muziki ya Marekani na dili hili
inamaanisha kwamba Davido sasa hivi atakua kwenye mikono mikubwa zaidi na hata
jina lake litazidi kuwa kubwa duniani kutokana na Sony ambao wamefanya
kazi na mastaa kama Alicia Keys, Beyonce, Bruno Mars, Drake, Bow wow,
Ciara na wengine.
Davido
aliipost hii picha hapa chini na kuonyesha furaha yake kama msanii wa kwanza wa
Afrika kusaini dili ya kazi na Sony Music kwa dunia akisema pia Mama yake
atakua anatabasamu huko mbinguni kwa kinachotokea sasa hivi, stori yake ndio
kwanza inaanza.
………………………………………..
Mcheza filamu raia wa kenya Lupita Nyong'o ameungana na
wacheza filamu wengine kushutumu kutojumuishwa kwa wacheza filamu weusi au wale
wachache kutoka kwa orodha ya wale wanaowania tuzo la Oscars.
Katika mtandao wake wa Istagram Lupita alisema kuwa alikuwa amekasirishwa kwa kukosaa kujumuishwa kwa wacheza filamu weusi.
Mwaka 2014 Lupita Nyong'o alishinda tuzo la Oscar kutokana na wajibu wake katika filamu ya Twelve Years a Slave.
Anaungana na wacheza filamu wanaozidi kuongezeka wakiwemo David Oyelowo na Don Cheadle ambao wamekosoa tuzo za Oscars kuwa kukosa kuteua watu kutoka tabaka zote.

Producer maarufu wa Tanzania kwenye muziki wa bongofleva
Nahreel ameingia kwenye top stories za kwenye Dstv.com baada ya kukataa kumpa
beat yake staa mmoja wa hip hop nchini Kenya.
Nahreel ameweka wazi kuwa alimkatalia kurekodi baada ya kugundua kwamba jamaa hakuwa na pesa.
"Jamaa alikuja studio, sitaki kumtaja jina ila aliniambia bwana inabidi tufanye kazi pamoja, tutengeneze wimbo... mi nikakubali na kazi ikaanza ila baada ya kumaliza kusuka kila kitu mwishoni akasema hana pesa ya kulipia beat, nikamkatalia."
Nahreel aliongezea, "Alijua sababu yeye analo jina kubwa labda ningempa beat for free ila ukweli ni kwamba sina hiyo, mimi nafanya biashara.... kila msanii unayemsikia juu ya beat ya Nahreel ujue amelipia, akaniambia basi naomba beat niende nayo nitakutumia pesa nikamwambia hapana, sifanyagi hivyo, tafuta pesa njoo lipia nitakutunzia beat yako."
Bei moja ya Nahreel inapatikana kuanzia shilingi milioni moja mpaka milioni moja na nusu za Kitanzania na mara nyingi Nahreel anapenda kufanya kila kitu kwenye studio yake, yani hapendi wala hataki kuuza beat peke yake, anapenda asimamie kazi beat yake itendewe haki na msanii hata kama ameiuza.

…………………………………………………