Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

‘Hakuna mazungumzo ofisi ya Spika na wapinzani’

Views:
Video Information


Mkuu wa Mawasiliano, Elimu na Habari wa Bunge, Owen Mwandumbya

HAKUNA mazungumzo yanayoendelea kati ya Spika na Kambi ya Upinzani, baada ya kutokea sintofahamu katika kambi hiyo kuhusu washiriki wa kamati za kudumu za Bunge.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Mawasiliano, Elimu na Habari wa Bunge, Owen Mwandumbya alisema kuundwa kwa Kamati hizo kulifanywa kwa taratibu za Bunge. Aidha amesisitiza kwamba kanuni za Bunge haziwezi kuvunjwa kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watu binafsi.


Alisema hayo wakati alipokuwa akifafanua kuhusu madai kwamba Kambi Rasmi ya Upinzani imekuwa ikikampeni dhidi ya kamati hizo baada ya kutangazwa rasmi na Spika Job Ndugai. Hadi jana haikuwa inajulikana kama Ofisi ya Spika inashughulikia malalamiko hayo ya upande wa upinzani.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika alisema katikati ya wiki hii kwamba watazungumzia msimamo mwishoni mwa wiki; ingawa alisema kwamba hawafurahishwi na jinsi Spika alivyochagua wajumbe wa kamati hizo.
Hata hivyo, hadi kufikia jana Upinzani walikuwa hawajasema kitu na juhudi za kumpata Mnyika kwa kutumia njia zote za mawasiliano zilishindikana.
Owen alisema hata hivyo hakuna mazungumzo yoyote yale na upinzani kwa kuwa utaratibu wa Bunge umefuatwa katika kupata wajumbe wa kamati hizo.
Hata hivyo Owen alisema kwamba anaamini kwamba upande wa upinzani utawasilisha majina ya wagombea wenyeviti katika kamati zilizobaki hesabu za serikali na hesabu za mitaa.
Kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Bunge kifungu cha 116 kifungu kidogo cha 11 kamati hizo zinatakiwa kuongozwa na upinzani.
Pamoja na kamati hizo kutokuwa na wenyeviti, kamati zimeendelea kujadili mambo yanayokuja katika Bunge linaloanza Jumanne ijayo. Hata hivyo kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira ilifanya uchaguzi wa mwenyekiti wake na makamu wake ambapo Peter Kafumu ndiye mwenyekiti na makamu wake ni Vicky Kamata.

SOURCE;MAGANGA ONE.
Similar Videos