Video Information
Kwa picha zake za Instagram, inaonekana asilimia 70 ya maisha ya Agnes Masogange huyatumia akiwa nje ya Tanzania.

Kwa muda mrefu amekuwa akiishi Afrika Kusini ambako huenda hukutana na mastaa wengi wanaoishia kupagawa na umbo lake!
Kama si kumwona kama ‘mwanaume wa ndoto yake’, kuna dalili kuwa huenda mrembo huyo akawa na uhusiano na msanii na producer wa Nigeria, Tekno Miles.
Tekno Miles ni msanii aliyepewa jina la Chris Brown wa Nigeria kutokana na uimbaji wao kufanana na alizaliwa kwa jina la Augustin Miles.