Video Information
Mchezaji wa Bayern Munich Arjen Robben ametajwa kuwa mchezaji bora wa
mzunguko wa kwanza wa msimu wa Bundesliga, katika kura iliyopigwa na
wachezaji 240 wa Bundesliga.
Robben alitawala kura hiyo, iliyoendeshwa na jarida la michezo la Kicker
na kutangazwa leo Jumatatu, akipata asilimia 46.7, akiwatangulia
mchezaji wa kati wa Wolfsburg Kevin de Bruyne pamoja na mshambuliaji wa
Eintracht Frankfurt Alexander Meier.
Katika uchaguzi mwingine Manuel Neuer wa Bayern Munich ametajwa kama mlinda mlango bora, Karim Bellarbi wa Leverkusen ameteuliwa kama mchezaji chipukizi bora , na Markus Weinzierl wa Augsburg amekuwa kocha bora wa mzunguko wa kwanza.
Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre , afpe , dpae
Mhariri: Iddi Ssessanga