Video Information

Neymar amekuwa akigonga vichwa vya habari katika magazeti ya Brazil asubuhi ya leo. Namba
10 huyo wa Brazil akizungumza na waandishi wa habari jana, na
alipoulizwa kuhusu 'uzito' alionao mabegani kutokana na michuano hii
alisema "Ndio, katika Kombe la Dunia kuna shinikizo," alisema na
kuongeza "Lakini naitazama kama ndoto yangu tangu utotoni. Nimekuwa
nikiota kucheza Kombe la Dunia. Siku niliyomuona Ronaldo akifanya
maajabu mwaka 2002, nilijiambia kuwa siku moja na mimi nataka nifanye
hivyo. Na sasa zamu yangu imewadia. Nitacheza dhidi ya Colombia, kama
vile nacheza mtaani tu."