Video Information

Kipa Guillermo Ochoa.
Fortaleza, Brazil. Inawezekana kuwa Mexico imetolewa ‘kikatili’ kwenye hatua ya 16 bora ya fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.
Visa vya winga wa Uholanzi, Arjen Robben kujiangusha na hatimaye kupata mkwaju wa penalti vilikatisha safari ya Mexico.
Hata hivyo, wakati ikirejea Mexico City, timu hiyo
imeacha simulizi kubwa kwenye fainali hizo, na hasa juu ya umahiri wa
kipa Guillermo Ochoa langoni.
Ochoa, ambaye ana umri wa miaka 28, aliwazuia
washambuliaji wengi kutikisa nyavu zake, wakiwamo wa Brazil walioongozwa
na Neymar katika mchezo ulioisha kwa timu hizo kutofungana.
Kipa huyo alikuwa kizingiti kwenye lango la
Mexico, lakini ana kitu cha ziada; ni mwanadamu mwenye vidole sita vya
mkono wake wa kulia.
Ochoa, mwenye umri wa miaka 28 ambaye msimu ujao
hana timu bada ya klabu yake ya sasa Ajaccio ya Ufaransa kutompa mkataba
mpya, alikuwa kivutio kwa mashabiki wa nchi hiyo kiasi cha wengine
kumwita “rais”
Ameichezea klabu hiyo mechi zaidi ya 100. Umahiri wake langoni utaweza kumpatia timu.
Hakuna shaka, klabu za barani Ulaya kama Arsenal na Manchester City zimevutiwa naye, ingawa yeye anapenda kubakia Ufaransa.
Safari yake ya kwenda Ufaransa mwaka 2011
ilikumbwa na kiwingu baada ya kuhusishwa na matumizi ya dawa za kulevya.
Alikuwa miogoni mwa nyota watano waliokumbwa na kashfa hiyo. Alitiwa
hatiani kwa kutumia dawa aina clenbuterol na kufungiwa.