Video Information

Luis Suarez alitajwa kuwa mshambuliaji hatari zaidi barani Ulaya kwa
msimu uliopita, lakini kwenye Kombe la Dunia kwa sasa anapambana na muda
kupona maumivu yake baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti mwezi uliopita.
KILA wakati zinazofika fainali za Kombe la
Dunia, washambuliaji makini kila mmoja wao huwa na ndoto za kwenda
kufunga mabao ili kunyakua Kiatu cha Dhababu cha mikikimikiki hiyo. Hata
hivyo, ni wachache tu ndiyo waliofanikiwa kuibuka kidedea.
Zimefika fainali nyingine za Kombe la Dunia na
safari hii zitafanyika nchini Brazil kuanzia keshokutwa Alhamisi. Kama
kawaida washambuliaji wa timu zitakazoshiriki fainali hizo watakwenda
kupambana kwa dhamira moja ya kuonyesha uhodari wa kutikisa nyavu na
kuinyakua tuzo hiyo binafsi.
Kwenye orodha ya mastraika makini watakaochuana
kuwania tuzo hiyo wapo wengi, kuanzia kwa Mario Balotelli wa Italia,
Robin van Persie wa Uholanzi na Karim Benzema wa Ufaransa na wakali hao
watakuwa kwenye vita hiyo kali kumsaka bingwa wa Kiatu cha Dhahabu
kwenye Kombe la Dunia.
Makala haya yanazungumzia mastaa wanaopewa nafasi
kubwa zaidi ya kukinyakua kiatu hicho cha dhahabu kama wataanza michuano
hiyo wakiwa kwenye viwango vyao vya siku zote ambazo vimewafanya kuwa
mahiri zaidi wanapokuwa ndani ya uwanja.
5. Sergio Aguero
Licha ya kusumbuliwa na hali ya kuwa majeruhi
mfululizo, straika huyo wa Argentina ni hatari anapolikaribia goli.
Aguero ni aina ya washambuliaji ambaye timu nyingi zingependa kuwa na
huduma yake uwanjani. Staa huyo alifunga mabao 28 katika mechi 34
alizochezea mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City.
Hivyo kama straika huyo ataendelea kuwa kwenye
kiwango hicho kwa mechi zote kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia, huku
kikosini Argentina akiwa na uhakika wa kupata pasi za mwisho kutoka kwa
Lionel Messi na Angel Di Maria, hilo litamweka kwenye nafasi nzuri ya
kufunga mabao mengi.
4. Neymar
Mwanzo wake klabuni Barcelona umekumbana na
nyakati nyingi ngumu na kushindwa kuonyesha makali yake halisi, lakini
kwenye Kombe la Dunia, Neymar atakuwa na kitu tofauti cha kukifanya
ndani ya uwanja.
Staa huyo anapewa nafasi kubwa ya kulibeba taifa
la Brazil ambalo ni wenyeji wa fainali hizo na alianza kuonyesha makali
yake ya kutikisa nyavu kwenye mchezo wa kirafiki wa ushindi wa mabao 4-0
dhidi ya Panama.
Kama Brazil ya Luiz Felipe Scolari itakuwa kwenye
ubora wake na Neymar akawa staa wao kwenye safu ya ushambuliaji, fowadi
huyo mwenye umri wa miaka 22 ana nafasi kubwa ya kuwa mshindani wa kweli
kwenye vita hiyo ya kuwania Kiatu cha Dhahabu.
3. Luis Suarez