Video Information

Ingawa haijapenda kuwataja kwa majina, lakini
Mwanaspoti linajua ni wa Simba. Simba imedaiwa kufanya mazungumzo na
wachezaji, Deus Kaseke na Saady Kipanga, ambao wana mikataba isiyopungua
mwaka mmoja na nusu kila mmoja kitu ambacho ni kinyume na kanuni za
usajili.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Steven Mapunda,
aliongeza kuwa timu hiyo haitakaa mezani kuzungumza na timu yoyote ile
juu ya mauzo ya wachezaji kwani haina mpango wa kuuza mchezaji yeyote
katika dirisha hili la usajili zaidi ya kuimarisha kikosi chao kwa ajili
ya msimu ujao.
“Tunataka kuzifundisha nidhamu timu za Ligi Kuu,
msimamo wetu wa mwisho ni kwamba hatuuzi mchezaji yeyote na hatutokaa
mezani kuzungumza na timu yoyote ile, waache kutusumbua kwa kutupigia
simu, na kiongozi au mpambe yeyote atakayekuja Mbeya atakuwa amepoteza
nauli yake bure,” alisema.
“Kuna baadhi ya watu tumewabaini wamefanya
mazungumzo na baadhi ya wachezaji wetu ilihali wakitambua kuwa wachezaji
hao wana mikataba na ni mali ya Mbeya City, kamwe hao watu
hatutawafumbia macho na tutawapeleka kwenye mamlaka husika.
“Haijalishi mchezaji anataka kuondoka au la,
asiyetaka kucheza tutampeleka kwenye kazi nyingine, nawaomba na hawa
watu waache kuwasumbua wachezaji wetu kwani hakuna mchezaji atakayeuzwa
wala kuondoka kwa wale wote tunaowahitaji, hatubabaishwi na fedha zao.”
Jeuri ya Mbeya City imekuja siku chache baada ya
klabu hiyo kupata udhamini wa miaka miwili kutoka kampuni ya Binslum wa
Sh360 milioni ili kutangaza bidhaa za kampuni hiyo hivyo kuiongeza uwezo
wa kujiendesha. Timu hiyo inamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya.