Video Information
Swala la kubadili rangi ya ngozi limekuwa kama msumari moto, kunao
wanaoliunga mkono na wale wanaolipinga swala hilo katu hawawezi
kulifanya.
Baadhi wanasema kuwa ni wanawake wasiojithamini na kujiamini pekee ndio wenye kujichubua ngozi.
Mjadala huo ukiendelea, wasichana wengi wanajitafutia umaarufu sio
Marekani na Uingereza tu bali hata katika kanda ya Afrika ya Mashariki.
Wasichana hao wamekuwa wakifanya kila wawezalo ili kupata huo umaarufu.
Mmoja wa wasichana hao ni Vera Sidika anayejulikana sana nchini Kenya na
Afrika mashariki kwa kuwa na makalio makubwa ambayo ndiyo yaliyompa
umaarufu wake baada ya kuonekana katika wimbo mmoja wa video uitwao 'You
Guy' ambao baadaye ulipigwa marufuku nchini Kenya.
Vera amejizidishia umaarufu kwa kubadili rangi yake ya ngozi, zamani
kidogo akiwa mweusi na sasa amejichubua na kuwa mweupe na pia kuwaambia
watu kuwa kubadili rangi ya ngozi yake ni yeye mwenyewe kujitakia. Hiyo
isiwashughulishe watu.
Vera anajulikana kwa kuwa na mazoea ya kujipiga picha hasa za makalio
yake na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii. Vara analinganishwa sana na
Kim Kardhashian hasa kwa sababu ya umbo lake.
Kazi ya Vera hasa ni ya uwanamitido lakini mbali na hilo Vera hulipwa
ili kufika kwenye karamu mbali mbali , kwenye disco na katika hafla
mbali mbali za watu mashuhuri. Yeye pia hulipwa kuwa katika kanda za
video za wanamuziki maarufu Afrika Mashariki.
Alifichua kupitia televisheni Ijumaa kuwa alitumia maelfu ya dola kubadili rangi ya ngozi yake na kujifanya mweupe.
Shughuli hiyo aliifanyia nchini Uingereza na ilimgharimu karibu milioni
15 pesa za Kenya, hizo ni dola 170,000 na kwamba tayari kuna watu wengi
wanaotaka sana kujichubua ngozi na kufanana na Vera, kwa mujibu wa
mwanadada huyo.
Vera anasema kuwa watu wamemsema sana kwenye mitandao ya kijamii vibaya
kwa sababu ya anavyoendesha maisha yake. Amewataja kama wanafiki kwa
sababu anasema huku wakiendelea kumsema na kumkosoa kwa kujichubua,
wamekuwa wakimuuliza alichofanya ili na wao watafute pesa wakafanye
hivyo kwa wanataka sana kufanan naye.
Mtindo wa wanawake kujichubua ni swala tata nchini Kenya. Sio kama India
ambako vipodozi vya kujichubua huuzwa wazi wazi. Nchini Kenya bidhaa
hizo, huuzwa kimagendo.
Wataalamu wanasema, wanawake wengi wanaendelea kujichubua licha ya hatari za bidhaa zinazouzwa kimagendo.
Swala la wanawake kijichubua barani Afrika lilianza kujadiliwa waziwazi
pale ambapo msanii raia wa Cameroon Dencia kuzindua rasmi bidhaa zake za
kuchubua ngozi ziitwazo, Whitenicious.