Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

FIFA YATANGAZA IMANI NA MCHUANO BRAZIL

Views:
Video Information
140417153244_sepp_blatter_512x288_afp_f1c79.jpg

Na Ellah Daniel.
Rais wa shirikisho la soka duniani Fifa amesema kuwa ana imani kuwa kombe la dunia nchini Brazil litakuwa na ufanisi mkubwa.
Bwana Sepp Blatter ametoa wito kwa raia wa Brasil wajitolee vilivyo kusaidia kufanikisha mchezo huo mwaka huu.
Matamshi ya Bwana Blatter yamekuja huku hofu ikielezewa mjini Sao Paulo juu ya msongamano mkubwa wa watu na magari kufuatia mgomo wa wafanyikazi wa shirika la reli.
Maafisa wakuu wa Fifa wenyewe walikwama katika foleni ndefu ya magari barabarani.
Usafiri huo unatarjaiwa kutatizika zaidi kufatia kuvunjika kwa mazungumzo kati ya muungano wa wafanyikazi hao na serikali.
Orodha kamilifu ya timu zitakazoshiriki michuano wa Kombe la Dunia imetolewa. Majina ya makocha 32 ambao watasimamia mechi za mashindano hayo, pia majina ya wachezaji 736 watakaoshiriki mechi hizo zitakazochezwa kati ya Juni 12 hadi Julai 13 zimetangazwa..
Taarifa zaidi iliyotolewa ni kuwa timu zimepunguza idadi ya wachezaji, majeraha kukaguliwa na hali ya afya ya wachezaji kutathminiwa. Haya yote yakiwa ni matayarisho kwa michuano hayo yatakayo anza jijini Sao Paulo.
Timu zote zimetayarisha wachezaji 23 ambao kwa sasa watazingatia uwezo wa kufanikisha timu zao.

Similar Videos