Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

YANGA YAWASILI KWA ALYHALY VEMA

Views:
Video Information


Msafara wa kikosi cha Young Africans umewasili salama jijini Alexandria leo majira ya saa 7 na kufikia katika
hoteli ya Shaeraton ukitokea katika jiji la Cairo ambako awali mchezo wa marudiano ulipangwa kufanyikwa
kabla ya jana kutolewa mabadiliko ya uwanja na mchezo huo utachezwa kesho katika dimba la Uwanja wa El
Max Stadium jijini Alexandria.
Young Africans ambayo iliwasili juzi jijini Cairo na kuweka kambi katika hoteli ya Nile Paradise Inn na kufanya
mazoezi kwa siku mbili mfululizo katika uwanja uliopo ndani ya hoteli hiyo ambayo uongozi wa Young Africans
kwa kushirikiana na Ubalozi uliweza kufanikisha kambi hiyo.
Awali makamu mwenyekiti wa Young Africans Clement Sanga alitangulia jijini Alexandria jana asubuhi pamoja
na maofisa wa ubalozi kwa ajili ya kufanya maaandalizi ya sehemu ambapo timu itafikia na leo timu ilipofika
ilikuta kila kitu kmeshakaa kwenye mpangilio wake.
Mara baada ya kuwasili jijini Alexandria wachezaji na viongozi wa Young Africans wamepata chakula cha
mchana kisha wamepata mapumziko mpaka majira ya saa 12 jioni ambapo timu itakwenda uwanja wa El Max
kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo huo.
Morali ya wachezaji bado ni ya hali ya juu kuelekea mchezo huo wa kesho, haki ya kambi ni nzuri hakuna
majeruhi hata mmoja hivyo vijana wote wapo tayari kwa kesho kuipeperusha bendera ya nchi.
Jioni timu itafanyya mazoezi katika Uwanja wa El Max ambao ndio utakaotumika kwa mchezo wa kesho.

Similar Videos