Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

WARUSI WAWEKEWA VIKWAZO ZAIDI NA EU.

Views:
Video Information

Viongozi kutoka mataifa ya Jumuiya
ya Ulaya wanaokutana mjini
Brussels kuimarisha vikwazo
wanavyowekea Urusi,wameamua
kuongeza idadi ya Warusi
wanaopaswa kuwekewa vikwazo
kibinafsi.
Orodha ya awali ya 21 sasa
imeongezewa watu wengine 12.
Viongozi hao wa Jumuiya ya Ulaya
pia wametoa wito kwa Tume
inayosimamia jumuiya hiyo iwe
tayari kuimarisha vikwazo zaidi vya
kiuchumi dhidi ya Urusi iwapo hali
hiyo ya sintofahamu itaendelea.
Kiongozi wa Ujerumani, Angela
Merkel, amesema kuwa wale ambao
majina yao yameongezwa kwa
orodha ya hapo awali
hawataruhusiwa kutembelea Ulaya
na mali yao itapigwa tanji kama
ilivyofanyika kwa maafisa 21 wa
Urusi na Ukraine mapema juma
hili.
Bi Merkel pia alisema kuwa
Jumuiya ya Ulaya iko tayari kuunga
mkono Serikali mpya ya Ukraine
kifedha, bora tu iafikianena Hazina
ya Fedha duniani (IMF). Waziri
Mkuu wa Uingereza, David Cameron
amesema hatua muhimu
zimechukuliwa kufikia sasa.

Similar Videos