Akizungumza na U heard ya XXL, Clouds FM
leo,Shilole na Nuhu wamesema wanapendana sana
na wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa
zaidi ya miezi mitatu sasa.
“Tunajipanga mambo fulani yakae sawa pamoja na
mke wangu kila kitu kitakaa sawa,” alisema Nuhu.
“Kweli tunakama miezi miwili ,mitatu tunashukuru
Mungu tunapendana kiukweli. Yeye ananipenda na
mimi nampenda pia, mimi nipo real kwake na yeye
yupo real kwangu kila mtu yupo real kwa mwezake.
Nilikuwa na girlfriend kipindi hicho ila tumeachana,
tumegombana siunajua, na nimekaa muda mrefu bila
kuwa na girlfriend, yaani mambo yalifanya tukaonana
tukapendana hivyo .First time nakumbuka tulikutana
studio,alikuja studio Kijitonyama ambapo mimi
nilikuwa nafanya kazi natengeneza beat zangu
skeleton tukaongea mambo mengi ya kimaisha
hatukuwa in deep sana kihivyo, ila tulivyoendelea
kujuana tukaona kila mtu akamzoea mwenzie,mimi
nikiwa mbali anakasirika na mimi nikiwa mbali nay
yeye anakasirika. Kwahiyo end of the day tukawa
tunapendana kweli yakawa mapenzi.”
Naye Shilole alidai kuwa ni kweli wanapenda na
Nuhu.
“Sijamkana Nuhu,kwanini nimkane kwa sababu gani?
Yeye ananipenda na mimi nampenda,” alisema
Shilole huku akisema yupo tayari kwa kufunga ndoa
na msanii huyo.
SHILOLE AKIONGEA NA XXL YA CLOUDS KUPITIA U HEARD JUU YA NUHU MZIWANDA
Views:
Video Information