Video Information

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Dkt. Frank Steinmeier akizungumza waandishi wa habari kwenye mkutano huo jijini Dar es Salaam na kuelezea mafanikio ya ushirikiano wa nchi hizo mbili.

Baadhi ya wageni waalikwa na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ubalozi wa Ujerumani nchini.
Membe alilisisitiza kwamba ziara ya Waziri mpya wa mambo ya nje kutoka Ujerumani ina manufaa makubwa kwa Tanzania kwa sababu amekuja na wawekezaji 65 kutoka maeneo mbalimbali.
Amesema kuwa ukarabati wa reli ya kati ni muhimu katika kudumisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili kwa maslahi ya watu wao.
"reli ya kati kama mnavyojua ilijengwa na Wajerumani mwaka 1913 na kwa sasa ina miaka karibu mia moja na kitu," aliongeza Waziri Membe
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Dkt. Steinmeier amesema kuwa nchi yake itaendelea kudumisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii na Tanzania katika jitihada za kuharakisha maendeleo ya nchi na watu wake.
Amesema kuwa serikali ya Ujerumani imeamua kukarabati reli ya kati katika jitihada za kukumbuka na kudumisha historia ya muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.
"najisikia furaha na faraja kuona nchi yaTanzania inapiga hatua mbele kimaendeleo baada ya uhuru wake,"