Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

PAMBANO LA CHEKA LASOGEZWA MBELE

Views:
Video Information
Bondia Francis Cheka.
Dar es Salaam. Pambano la Francis Cheka na Varely Brudov wa Russia lilililokuwa lifanyike Aprili 5 jijini Dar es Salaam limesogezwa mbele hadi litakapotajwa tena, huku lile la Francis Miyeyusho na Ronald Pontillas wa Ufilipino likibaki palepale.
Promota wa pambano hilo, Mussa Kova alisema pambano la Cheka limesogezwa baada ya Brudov kuumia mguu akiwa mazoezini hivyo kutakiwa kutopigana kwa wiki mbili.
"Baada ya kupokea taarifa ya kuumia kwa Brudov, tuliwasiliana na rais wa WBF ili tubadilishiwe bondia, alituambia kama bondia atabadilika pambano halitakuwa la ubingwa wa dunia.
"Kwa kuwa lengo letu ni kuandaa mapambano yatakayowasaidia mabondia wa Tanzania kupanda kimataifa tumeamua kuliahirisha kwa muda hadi Brudov atakapopona,"alisema Kova.
Similar Videos