Katika ushahidi unaoendelea
kutolewa dhidi ya mwanariadha
mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar
Pistorius, rafiki ya mwanariadha
huyo, ameambia mahakama kuwa
Pistorius alipenda sana bunduki
Darren Fresco, alisema kuwa alikuwa
naye mara mbili alipokuwa na
bunduki aliyoiofyatua katika sehemu
ya umma.
Bwana Pistorius wakati mmoja
alifyatua bunduki yake akiwa ndani
ya mkahawa , ingawa yeye ndiye
aliyelaumiwa kwa hilo,alisema
bwana Fresco said.
Mwanariadha huyo amekanusha
madai ya kumuua mpenzi wake kwa
maksudi, akisema kuwa alidhania
kuwa ni mwizi aliyevamia nyumba
yake.
Bwana Fresco alisema kuwa katika
tukio lengine, alikuwa
anaendeshagari lake wakati ambapo
Pistorius alipofyatua tena bunduki
yake baada ya polisi kumzuia
kuendesha gari lake kwa kasi.
Alisema kuwa Pistorius alikasirika
baada ya polisi kuchukua dunduki
yake iliyokuwa kwenye kiti cha
nyuma ya gari lake na kumwambia:
'' hauruhusi kugusa bunduki ya mtu
mwingine, ikiwa chochote kitatokea
atakuwa wa kulaumiwa.''
Mwandishi wa BBC nchini humo,
Pumza Fihlani anasema kuwa
Pistotius katika kikao cha Jumanne
alikuwa mtulivu ikilinganishwa na
Jumatatu.
Aliketi akiwa kimya na kuandika
baadhi ya maneno yaliyokuwa
yanasemwa.
Ushahidi wa Fresco, ulitoa taswira
ya mchezaji huyo alivyopenda
maisha ya kifahari akiwa na rafiki
zake. Alipenda magari, wanawake
warembo , bunduki na kwamba
aliwashukia sana polisi.
Aliyekuwa mpenzi wa Oscar pia
alitoa ushahidi sawana huo
mahakamani, wiki ya kwanza ya
kuzikilizwa kwa kesi hiyo.
OSCAR PISTORIUS ALIPENDA SANA BUNDUKI....
Views:
Video Information