Video Information

Na Fadhy Mtanga
Mwananchi mmoja nchini Zambia, mwanaume mwenye umri wa miaka 34 anashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Livingstone kwa kosa la kuingilia msafara wa makamu wa rais, Guy Scott (pichani) na kuuovateki.
Gazeti la Daily Mail la nchini Zambia limemnukuu Kamishna wa Polisi wa Jimbo la Kusini, Charity Katanga kuwa kadhia hiyo ilitokea siku ya Jumapili wakati kiongozi huyo alipokuwa akielekea hotelini jijini hapo.
Kwa mujibu wa afisa huyo wa polisi, kitendo cha mtu huyo kuuvateki msafara wa makamu wa rais kilizua taharuki kubwa kwa maafisa usalama. Gari la polisi likamfukuzia na kufanikiwa kumsimamisha. Hivyo, mkazi huyo wa jiji hilo amefunguliwa mashtaka ya uzembe barabarani.
Hata hivyo, kitendo hicho hakikuwa na madhara mengine yoyote.