Lakini kwa vile wanategemewa sana
kumaliza katika 4 Bora za Ligi Kuu
England na hivyo kucheza UEFA
CHAMPIONZ LIGI, nafasi yao ya
kucheza EUROPA LIGI itakwenda
kwenye Timu itakayomaliza Nafasi ya 6
kwenye Ligi Kuu England.
++++++++++++++++++++++++++++
NANI HUCHEZA ULAYA:
-Timu 4 za Juu kwenye Ligi Kuu
England hucheza UEFA CHAMPIONZ
LIGI
-England inazo Nafasi 3 za kucheza
EUROPA LIGI: Bingwa wa FA CUP,
Bingwa wa Capital One Cup na Timu
ya 5 kwenye Ligi Kuu England.
-Ikiwa Mshindi wa FA CUP amefuzu
UEFA CHAMPIONZ LIGI, Nafasi yake
kucheza EUROPA LIGI itachukuliwa na
Mshindi wa Pili wa Kombe hilo.
-Ikiwa Mshindi wa Pili wa FA CUP
nae amefuzu kucheza UEFA
CHAMPIONZ LIGI, basi Nafasi yake
kwenye EUROPA LIGI itachukuliwa na
Timu itakayomaliza Nafasi ya 7 kwenye
Ligi Kuu England.
++++++++++++++++++++++++++++
Msimu huu Manchester United
wamekuwa wakisuasua na wapo Nafasi
ya 7 wakiwa Pointi 12 nyuma ya Timu
iliyo Nafasi ya 4 kwenye Ligi, Nafasi
ambayo ndiyo ya mwisho kucheza
UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Pia wapo Pointi 8 nyuma ya
Tottenham ambao wako Nafasi ya 5
ambayo ndio Nafasi ya kucheza
EUROPA LIGI.
++++++++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA TIMU P GD PTS
1 Chelsea 28 30 63
2 Liverpool 28 38 59
3 Arsenal 28 24 59
4 Man City 26 42 57
5 Tottenham 28 4 53
6 Everton 27 11 48
7 Man Utd 27 12 45
8 Newcastle 28 -2 43
9 Southampton 29 1 39
++++++++++++++++++++++++++++
Lakini huenda pia Timu ya Nafasi ya 7
nayo ikaweza kucheza EUROPA LIGI
ikiwa Mshindi wa FA CUP nae yupo
kwenye 4 Bora na hivyo kucheza UEFA
CHAMPIONZ LIGI.
Ikiwa Man United watafuzu kucheza
EUROPA LIGI kwa kumaliza Nafasi ya 7
hilo nalo litawaletea hali ngumu
kwani watalazimika kuanzia
Mashindano hayo Raundi ya Tatu ya
Mchujo inayoanza kuchezwa Julai 31.
MAN CITY YANYAKUA KOMBE LA CAPITAL ONE..
Views:
Video Information