Video Information
Ndege na meli kutoka nchi mbali
mbali zinaendelea kuitafuta
mabaki ambayo huenda
yanatokana na ndege ya Malaysia
iliyopotea takriban wiki mbili
zilizopita ikiwa imebeba takriban
watu 240.
Matumaini ya kutatua kitendawili
hicho yaliongezeka baada ya
Australia kutoa picha za Satelaiti za
vitu viwili vilivyoonekana baharini
vuikidhaniwa kuwa vifusi vya ndege
hiyo.
Hata hivyo hadi kufikia sasa hakuna
cha maana kilichopatikana.
Afisa mmoja mkuu wa New Zealand
amesema operesheni hiyo ilitatizwa
na kuchafuka kwa bahari na kutoona
vizuri.
Meli ya mizigo ya Norway ilitumia
taa kuyatafuta mabaki hayo pasina
kufanikiwa.