Video Information
Wakuu wa Vietnam wanasema
michirizi miwili mikubwa ya
mafuta imeonekana katika bahari
nje ya mwambao wa kusini wa
nchi hiyo, huku msako unaendelea
kutafuta ndege ya Shirika la Ndege
la Malaysia iliyotoweka Jumamosi
asubuhi.
Inasemekana michirizi hiyo miwili
sambamba ina urefu wa kama
kilomita 15 hadi 20.
Ndege na meli kutoka nchi kadha
zimekuwa zikifanya msako katika
eneo la bahari baina ya Vietnam na
Malaysia.
Usiku ulipoingia ndege hiyo ya aina
ya Boeing 777 ilikuwa bado
haikuonekana - ndege ilipoteza
mawasiliano na waongozi wa radar
saa mbili baada ya kuanza safari.
Ilikuwa imebeba abiria na
wafanyakazi wa ndege 239.