Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

Video Information

Mafunzo katika vyuo vikuu vya
umma nchini Kenya yameathirika
baada ya wahadhiri wa vyuo
kuanza rasmi mgomo wa kitaifa.
Wahadhiri hao wamekiuka agizo la
mahakama na kutogoma na kuamua
kugoma.
Wanailaumu serikali kwa
kutotekeleza makubaliano ya
nyongeza ya marupurupu yao kama
ilivyoahidi mwaka jana.
Mgomo huo unajiri wakati serikali
ya Kenya imewataka wafanyikazi wa
serikali kukubali mishahara yao
kupunguzwa hasa baada ya Rais
Uhuru Kenyatta na Naibu wake
William Ruto pamoja na baraza la
mawaziri kupunguza mishahara yao
kutokana nagharama kubwa ya
matumizi ya serikali.
Zaidi ya wafanyakazi 30,000 wa vyo
vikuu wameanza kususia kazi baada
ya waziri wa elimu kukosa kufikia
makubaliano ya kusitisha mgomo
huo ambapo wahadhri wanadai
shilingi bilioni 3.9 kati ya wahadhiri
na wakuu wa vyuo hivyo.
Kwa sasa idadi ya wanafunzi ambao
watakosa mafunzo ni kati ya 200,000
na 300,000, ikiwa serikali haitaleta
suluhu.
Mkutano wa awali kati ya waziri wa
elimu na makatibu wake wawili,
haukuzaa matunda.
Kiini cha mgogoro huo ni malipo ya
awamu ya pili ya shilingi bilioni 7.8
ya nyongeza ya mishahara ambayo
iliafikiwa mwaka 2012.
Pesa hizo zilipaswa kulipwa kwa
awamu, huku nusu ya pesa hizo
zikilipwa Disemba mwaka 2012.

Similar Videos