Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

MAANDAMANO YASHIKA KASI NCHINI VENEZUELA

Views:
Video Information

Maelfu ya wapinzani nchini
Venezuela wamefanya
maandamano katika mitaa
mbalimbali mjini Caracas,
maandamano yanayofanyika dhidi
ya Serikali ya nchi hiyo.
Baada ya maandamano,
wanaharakati walipambana na Polisi
katika manispaa zinazoshikiliwa na
upinzani, Chacao na Altamira.
Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro
ameahirisha maadhimisho ya
sherehe za kitamaduni mpaka
mwishoni mwa juma hili na kutoa
rai kwa Raia wa Venezuela
kusherekea kwa amani.
Takriban watu 17 waliuawa katika
vurumai tangu zilipojitokeza zaidi
ya majuma matatu yaliyopita.
Viongozi wa upinzani wamewataka
watu wapuuzie msimu wa sherehe
za kiutamaduni ambazo ni taratibu
za jadi ya nchi hiyo kusherekea.
Upinzani unadai kuachwa huru kwa
Waandamanaji na Wanaharakati
waliokamatwa tangu mwezi uliopita,
akiwemo mwanasiasa maarufu
Leopoldo Lopez.

Similar Videos