Kama ilivyokuwa imetarajiwa na
wengi mwigizaji mashuhuri kutoka
Kenya Lupita Nyong'o
amenyakuwa tuzo la Oscar la
mwigizaji msaidizi wa kike kwa
jukumu lake la kuelezea masaibu
ya Patseh katika filamu ya utumwa
ya ''12 Years A Slave.''
Baada ya kupokea tuzo hilo Lupita
amesema " Haikwepi mawazo yangu
kwamba hata dakika moja ya furaha
katika maisha yangu ni shukran na
maumivu makubwa kwa mtu
mwingine.''
Kisha Lupita akaongeza kusema, "
Na iwe ukumbusho kwangu na kila
mtoto kwamba kokote unakotoka,
ndoto zako ni halisi.''
Mwigizaji Jared Leto alinyakuwa tuzo
la mwigizaji bora msaidizi wa kiume
kwa jukumu lake la kuelezea maisha
ya mwanamke aliye na jinsia mbili
aliyekuwa na akiishi na virusi vya
HIV katika filamu Dallas Buyers
Club.
Alilazimika kupunguza uzani kwa
kipindi kifupi ili kuigiza.
Sherehe ya kutolewa kwa tuzo hizo
zimefanyika mjini Los Angeles
nchini Marekani.
LUPITA NYONG'O ANYAKUA TUZO YA OSCAR.
Views:
Video Information