Rais Uhuru Kenyatta, atapunguziwa
mshahara wake kwa Sh 248,000 za
Kenya karibu sawa na dola 3,000,
na naibu rais William Ruto
anapunguziwa Sh210,000. mawaziri
na makatibu wakuu wote
wanapunguziwa pia mishahara yao
kwa asili mia 10.
Rais Kenyatta alitangaza uwamuzi
huo siku ya Alhamisi baada ya
mkutano na maafisa wa juu wa
serikali na wajumbe wa kamati ya
bajeti ya bunge mjini Nyanyuki, na
kueleza kwamba serikali hivi sasa
inatafakari na kujadili kupunguza
matumizi ya safari za kigeni katika
lengo la kupunguza matumizi na
kuweza kupata fedha kutumika kwa
miradi ya maendeleo.
Akizungumza na waandishi habari
baada ya mkutano huo, Rais
Kenyatta alisema serikali
inatafakari pia juu ya kufutilioa
mbali matumizi ya umaa mabayo
hayaleti faidi au kuimarisha maisha
ya wakenya.
Wachambuzi wa kisiasa wanasema
uwamuzi huo wa kihistoria
unaonekana umechukuliwa kwa
lengo la kuanzisha mjadala wa
kitaifa juu ya kupanga upya
mishahara ya watumishi wa serikali
na matumizi, juhudi zinazoongozwa
na Tume ya Mishahara na
Matumizi, inayojaribu kupunguza
bajeti ya mishahara ambayo
inafikia $ bilioni 5 kwa mwaka.
Siku ya Jumatatu tume hiyo itakua
na mjadala wa umaa juu ya
mswada wa mishahara ya serikali
katika ukumbi wa jengo mikutano
ya kimataifa ya Kenyata KCC mjini
Nairobi.
KUPUNGUZIWA KWA MISHAHARA
Views:
Video Information