Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imeipiga
faini ya jumla ya sh. milioni moja
klabu ya Simba kutokana na
makosa mbalimbali ikiwemo vitendo
vinavyoashiria ushirikina uwanjani.
Simba ilifanya vitendo hivyo katika
mechi yake dhidi ya Mbeya City
ambapo imepigwa faini ya sh.
500,000. Pia imepigwa faini
nyingine ya sh. 500,000 kwa
makocha wake MCroatia ZDrako
Logarusic, Selemani Matola na Idd
Pazi kuingia uwanjani na kumzonga
mwamuzi kwenye mechi hiyo.
Naye mshambuliaji wa Simba,
anayekifukuzia kiatu cha dhahabu
Amisi Tambwe amepigwa faini ya
sh. 500,000 kwa kushangilia bao
alilofunga kwenye mechi hiyo kwa
kuonesha ishara ya matusi kwa
kidole.
Mbeya City imepigwa faini ya sh.
300,000 kwa washabiki wake
kuingia uwanjani kwenye mechi
dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa
mjini Bukoba. Klabu za Yanga na
Coastal Union zimepigwa faini ya
sh. 500,000 kila moja kwa
washabiki wao kurusha chupa za
maji uwanjani wakati timu hizo
zilipopambana jijini Tanga.
Kiungo wa Mtibwa Sugar, Shabani
Nditi amepigwa faini ya sh.
500,000 kwa kumpiga mchezaji wa
Simba, wakati Salvatory Ntebe pia
wa Mtibwa Sugar amepigwa faini ya
sh. 500,000 kwa kumtukana refa
kwenye mechi dhidi ya Mbeya City.
Pia mshambuliaji wa Mtibwa Sugar,
Musa Mgosi amepigwa faini ya sh.
500,000 kwa kosa la kupiga
uwanjani kwenye mechi dhidi ya
Ashanti United ambapo vilevile
atakosa mechi tatu za ligi. Coastal
Union imepigwa faini ya sh.
500,000 kwa washabiki wake
kumrushia chupa za maji kipa wa
Mbeya City.
Nayo JKT Ruvu imepigwa faini ya
sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika
uwanjani kwenye mechi dhidi ya
Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Vilevile wamiliki wa Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga
wameandikiwa barua ya kufanya
marekebisho ya vyumba vya
wachezaji, kwa vile havina hewa ya
kutosha.
KAMATI YA LIGI YADONDOSHA RUNGU LAKE KWA SIMBA.
Views:
Video Information