Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

CHATU AMSHINDA MAMBA AUSTALIA.

Views:
Video Information

Chatu ameshinda vita vikali dhidi
ya Mamba Kaskazini mwa mji wa
QueensLand, kupigana na Mamba,
kumpinda na kisha kumla.
Tukio hilo lilishuhudiwa katika ziwa
Moondarra, karibu na mlima Isa na
kunaswa kwa kamera na wakazi wa
eneo hilo siku ya Jumapili.
Nyoka huyo mwenye urefu wa futi
10, alijipinda kwa Mamba na kuanza
kupambana naye majini.
Hatimaye, Nyoka huyo alifanikiwa
kumshinda Mamba na kumtoa nje
ya maji na kisha kumla.
Nyoka alimvuta Mamba na kumtoa
ndani ya Maji
Chatu huyo alianza kumla Mamba
na kushangaza wakazi
Baada ya mlo huo mkubwa Nyoka
alijiendea zake
Tiffany Corlis,mkazi wa eneo hilo,
alishuhudia pambano hilo na
kupiga picha hizi.
"lilikuwa jambo la ajabu sana, ''
aliambia BBC
"Tulimuona Nyoka akipambana na
Mamba , alifanikiwa kumbana
mamba hasa katika sehemu ya
miguu ya ili kumdhibiti.''
"Pambano lilianzia ndani ya maji.
Mamba alikuwa anajaribu kuweka
kichwa chake juu ya maji wakati
mmoja ingawa Nyoka alikuwa
amembana sana.''
"Baada ya Mamba kufa nyoka
alijikunjua, na kuja mbele ya
Mamba huyo na kuanza kumla,''
alisema Tifanny.
Bwana Corlis alisema kuwa
ilimchukua nyoka muda wa robo saa
kumla mamba huyo.
''Bila shaka Nyoka huyo alishiba
vyema, na hatujui alikokwenda,
baada ya mlo wake,'' alisema mama
huyo ambaye hakutaka kusuburi
kumuona Nyoka tena.
Mtu mwingine aliyeshuhudia
pambano hilo Alyce Rosenthal,
alisema kuwa wanyama hao wawili
walipambana kwa karibu saa 5.
Hatimaye wote walionekana
kuchoka.
''Sio kitu unachoweza kuona kila
siku,'' alisema Alyce.

Similar Videos