Ben Pol amesema hata kwenye malipo hayo ambayo
amedai ni aibu kuyataja hupatikana mpaka
mfikishane kwenye vyombo vya dola.
“Nimeachana na RBT kwasababu haijawahi kunilipa
vizuri ni kama biashara kichaa kabisa.” Ben ameimbia
Bongo5.
“Halafu pia ukichukia hatua let’s say za kisheria ndio
unaweza kuona ripoti za mauzo nini, ndio watu
wanakuletea,lakini hivi hivi wanakuwa wanasumbua
sana. Hii ni kwangu mimi sijui kwa wenzangu.
Kwenye RBT nimeingiza nyimbo zangu zote ,isipokuwa
Jikubali,Pete na Unanichora ndio nyimbo ambazo
sikuingiza. Pesa ambazo wamenilipa kwa nyimbo
zangu nyingine nikisema nizitaje itakuwa aibu.”
Kutokana na ukweli huo, Ben Pol amesema yupo
kwenye maandalizi ya kuandika barua ili waziondoe
nyimbo zake.
“Kwenye kampuni zote ambazo nimefanya nazo
biashara hii naenda kutoa nyimbo zangu,sasa hivi
nipo kwenye kuandaa barua halafu nasitisha kwenye
kampuni zote,halafu naweza nisiuze tena.”
BEN POL APANGA KUJITOA KWENYE BIASHARA YA MIITO YA SIMU NI AIBU KUTAJA KIASI ALICHOWAHI KUPATA.
Views:
Video Information