Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

ATLETICO MADRID YAFUZU....UEFA

Views:
Video Information

Diego Costa amedumisha rekodi ya
kufunga katika mechi zake zote wa
kuwania kombe la klabu bingwa
barani Ulaya, msimu huu pale
Atletico Madrid ilipoishinda AC
Millan na kufuzu kwa robo fainali
kwa mara ya kwanza tangu mwaka
wa 1997.
Mshambulizi huyo, ambaye
aliifungia Madrid bao la pekee
katika mechi ya raundi ya kwanza,
alivurumisha kombora kali baada ya
kupata pasi nzuri kutoka kwa Koke
dakika ya pili.
Arda Turan naye alifunga la pili
kabla ya Raul Garcia kuongeza la
tatu.
Na ili kudhihirisha kuwa yuko katika
hali nzuri kwa sasa, Diego Costa kwa
mara nyingine tena aliliona nyafu
za wapinzani wao na kufunga bao
lake la pili katika mechi mechi.
Costa, ambaye aliichezea timu ya
taifa ya Uhispania mechi yake ya
kwanza, amefunga magoli saba
katika mechi tano za kuwania kombe
la klabu bingwa Ulaya msimu huu
na amefunga magoli 29 katika
mashindano yote aliyoshiriki.
Leo usiku kutakuwa na mechi mbili,
Barcelona watakwaruzana na
Manchester City nayo Bayer
Leverkusen wakisafiri Ufaransa
kuchuana na Paris Saint Germain.

Similar Videos