Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

ABATILISHWA HUKUMU YAKIFO MAREKANI

Views:
Video Information

Mwanamume mmoja aliyeishi jela
kwa zaidi ya miaka 25 akisubiri
hukumu ya kifo nchini Marekani,
ameachiliwa huru baada ya
mahakama kubatilisha uamuzi wa
mahakama kuwa alikuwa na hatia
ya mauaji yaliyotokea mwaka
1983.
Glenn Ford, 64, alikuwa jela
akisubiri hukumu ya kunyongwa
tangu mwaka 1988 mwezi Agosti.
Mahakama wakati huo ilimpata na
hatia ya mauaji ya Isadore Rozeman
aliyekuwa na umri wa miaka 56
akiuza mikufu. Bwana Ford alikuwa
mfanyakazi wake wakati huo.
Vyombo vya habari nchini humo
vinasema kuwa ni mmoja wa
wafungwa waliohukumiwa kifo kwa
muda mrefu nchini humo na
kuachiliwa.
Glenn alisema kuwa anahisi vizuri
sana kwamba ameachiliwa.
Alisema ana maudhi ndani ya moyo
wake kutokana na kufungwa bila
hatia kwa kitu ambacho hakukifanya
na kuwa amepoteza muda wake
mwingi jela.
"miaka 30 ya maisha yangu. Siwezi
kufanya mambo ambayo ningefanya
nikiwa na umri wa miaka 35, 38 au
40. Mwanangu nilipofungwa jela
alikuwa mtoto sasa ni mtu mzima
na watoto wake.''
Jaji aliymwachilia huru bwana Ford,
Ramona Emanuel alisema Jumatatu
kuwa kulikuwa na ushahidi mpya
kuonyesha kwamba Bwana Ford,
hakuhusika na mauaji hayo.
Makosa mengi yalipatikana katika
kesi dhidi ya Ford kama
yalivyoelezwa na vyombo vya habari
nchini Marekani.
Inaarifiwa kuwa kesi ya Ford
iliendeshwa na mawakili ambao
hawakua na ujuzi wa kazi.

Similar Videos