Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

TUTU AMSIHI MUSEVENI KUHUSU MSWADA MPYA

Views:
Video Information
Rais Yoweri Museveni82600-004-C8437ECB_0a75a.jpg
Askofu mstaafu wa Cape Town, Desmond Tutu, amemsihi Rais Museveni wa Uganda asitie saini mswada ulioleta utatanishi kuhusu wapenzi wa jinsia moja.
Akofu Tutu, aliyewahi kupata tuzo ya amani ya Nobel, alisema amevunjika moyo kuwa Rais Yoweri Museveni anaonesha kubadilisha msimamo wake, kwa vile awali alisema kuwa hataruhusu mswada huo kuwa sheria.
Desmond Tutu alisema haistahiki kuwa na ubaguzi kama huo, na alitoa mifano ya mfumo wa zamani wa ubaguzi wa rangi uliokuwako Afrika Kusini na ubaguzi wa Wa-Nazi wa Ujerumani.
Alisema hiyo ni mifano mibaya kabisa.
Awali mswada wa Uganda ulipendekeza kifo kwa vitendo vya kulawiti na baadae kubadilishwa kuwa adhabu ya kifungo.www.sayariblog.blogspot.com
Similar Videos