Video Information
Manchester
United sasa inajipanga kufungua mauzo ya mshambuliaji wa pembeni Luis
Nani licha ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureni kuongeza mkataba
na klabu hiyo majira ya kiangazi iliyopita.
David
Moyes alikuwa chachu ya kumshawishi winga huyo mwenye umri wa miaka 27
kusaini mpango mpya uliokuwa na thamani ya euro €96,000 kwa wiki ndani
ya Old Trafford, lakini sasa mambo yamemwendea kombo winga huyo kiasi
klabu hiyo kuamua kufungua duka kwa ajili ya mauzo ya nyota huyo wa
zamani wa Sporting Lisbon.
Mreno
huyo msimu huu ameanza michezo minne tu, na hajaonekan uwanjani tena
tangu mchezo wa mapema mwezi Disemba mwaka jana ambapo United ilipokea
kichapo kutoka kwa Newcastle na tangu wakati huo amekuwa akiuguza
majeraha ya msuli jambo ambalo limemfanya Moyes kutamka atamuweka
pembeni kwa muda.www.sayariblog.blogspot.com