Video Information

Mradi wa kurutibisha madini ya Uranium nchini Iran
Shirika la Umoja wa mataifa la
kudhibiti nguvu za nuklia, limesema kuwa Iran imeanza kutekeleza
makubaliano juu ya mkataba kuhusu mpango wake wa kurutubisha madini ya
Uranium.
Mkuu wa mpango huo wa Iran, alisema kuwa sehemu ya barafu inayotumika kwa shughuli hiyo imeanza kuyeyushwa.Marekani imeahidi kulegeza baadhi ya vikwazo dhidi ya Iran ikiwa itafanya hivyo.
Mkuu wa sera ya kigeni katika Muungano wa Ulaya, Catherine Ashton amesema kuwa anatumai kwamba katika awamu itakayofuata ya mazungumzo na Iran, suluhu ya kudumu itaweza kupatikana.
Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wa maswala ya kinuklia wako katika mji mku wa Iran, Tehran, na wanatazamiwa kuthibitisha kuwa Iran imesitisha kusafisha madini yake ya Uranium.
Mwishoni mwa siku, Iran huenda ikapata Uhuru wa kuuza mafuta na kemikali zake zenye mabilioni ya Dola kufufua uchumi wake.