Video Information

Mkuu wa Wilaya wa Arusha,John Mogella akizungumza kwenye ufunguzi wa Kongamano la walimu Mkoa Arusha juzi.Kushotoni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB,Abdulmajid Nsekela,Mkuu wa Wilaya Arumeru,Nyiremba Munasa na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini,Vicky Bishubo.Picha na Filbert Rweyemamu
Kampuni na taasisi mbalimbali nchini zimetakiwa kuchukua hatua ya kujua hali ya afya za wafanyakazi, kwa sababu jambo hilo litasaidia pia kuongeza mchango wao uzalishaji.
Kauli hii itolewa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam (RAS), Teresia Mbando wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Makao Makuu ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Mbando alisema suala la maambukuzi ya VVU/Ukimwi yakiwa yanaongezeka, ni muhimu kwa kampuni na taasisi kuchukua hatua ya kujua hali ya afya za wafanyakazi wake, akisema kuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kutekeleza harakati na mpango wa Serikali wa mapambano dhidi ya Ukimwi.Mbando aliipongeza TBL kwa kuweka mbele suala la afya ya wafanyakazi wake na kutoa wito kwa kampuni na taasisi nyingine kuiga mfano huo, kwani kwa kufanya hivyo kutapunguza kwa kiasi kiwango kubwa maambukizi mapya .(P.T)
Kwa upande wake, Meneja Rasilimali wa TBL, David Magesa alisema toka mwaka 1990, kampuni hiyo ilikuwa na mpango ambao unawawezesha kupata huduma ya upimaji wa hiari na ushauri nasaha .
Magesa alisema pia hadi sasa asilimia 80 ya wafanyakazi wa TBL wanajua hali ya afya zao.
"Mbali na upimaji wa afya hiari na ushauri nasaha, kampuni kupitia kliniki yake ambayo imejitosheleza inatoa bure dawa za kurefusha maisha ( ARVs), na mpango huo pia unashirikisha zaidi ya asilimia 40 ya wanafamilia wa wafanyakazi," alisema .www.sayariblog.blogspot.com