Video Information

Zipo Nchi 10 ambazo zimepangiwa Mechi 5, za Nyumbani na Ugenini, na Washindi watano ndio watakaoenda Brazil.
Ivory Coast watamtegemea Didier Drogba
watakapocheza na Senegal kwenye Mechi ya kwanza Mjini Abidjan huku
Cameroun wakifurahia kwa Straika wao hatari Samuel Eto’o kughairi
kustaafu na Wikiendi hii atakuwa huko Rades Nchini Tunisia kuiongoza
Cameroun itakapocheza na Tunisia.
Asamoah Gyan atakuwa na Nchi yake Ghana
watakapoikaribisha Egypt huko Kumasi na huko Addis Ababa, John Mikel Obi
atakuwa na Nigeria itakayocheza na Ethiopia.
Nae Jonathan Pitroipa, ambae ndie
aliteuliwa Mchezaji Bora AFCON 2013, atakuwa na Burkina Faso huko
Ouagadougou kucheza na Algeria.
KOMBE LA DUNIA 2014
AFRIKA
Raundi ya Mwisho ya Mtoano
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Mechi za Kwanza:
Jumamosi Oktoba 12
19:00 Burkina Faso v Algeria
20:00 Ivory Coast v Senegal
Jumapili Oktoba 13
16:00 Ethiopia v Nigeria
20:00 Tunisia v Cameroon
Jumanne Oktoba 15
19:00 Ghana v Egypt
Marudiano:
Jumamosi Novemba 16
18:00 Nigeria v Ethiopia
22:00 Senegal v Ivory Coast
Jumapili Novemba 17
17:30 Cameroon v Tunisia
Jumanne Novemba 19
19:00 Egypt v Ghana
21:15 Algeria v Burkina Faso
**FAHAMU: Washindi 5 ndio watacheza Fainali za Kombe la Dunia
Kwenye Fainali za Kombe la Dunia
zilizopita ambazo zilichezwa Afrika Kusini Mwaka 2010, Algeria,
Cameroon, Ghana, Ivory Coast na Nigeria ndizo ziliiwakilisha Afrika,
paamoja Wenyeji Afrika Kusini, na safari hii pia Nchi hizo, ukuiondoa
Afrika Kusini, zina nafasi kwenda Brazil.
Kocha wa Ivory Coast, Sabri Lamouchi,
amemwita Sentahafu wa Liverpool, Kolo Toure, ili kuungana na Kaka yake
Yaya Toure kuhakikisha wanaifunga Senegal Mjini Abidjan.
Senegal wamemwacha Demba Ba kwa vile
hachezi mara kwa mara Klabuni kwake Chelsea na badala yake kumtegemea
Papiss Cisse wa Newcastle.