UncategoriesMnigeria akamatwa Kenya na dawa za kulevya, inaaminika alipitia airport ya Julius Nyerere
Mnigeria akamatwa Kenya na dawa za kulevya, inaaminika alipitia airport ya Julius Nyerere
Views:
Video Information
Raia
wa Nigeria aliyefukuzwa nchini Kenya kwa kosa la kujihusisha na
biashara haramu ya dawa za kulevya amekamatwa jijini Nairobi na
inaaminika amepitia kwenye airport ya Julius Nyerere na kupitia mpaka wa
Namanga. Enobemhe Emanuel Peter amekamatwa na pakiti 425 za Heroin huko
jijini Nairobi. Mnigeria huyu ni moja kati ya watu waliofukuzwa nchini
Kenya kwa agizo la Rais Uhuru Kenyatta kuwafukuza watu wote
wanaojihusisha na biashara za dawa ya kulevya.
Idara ya uhamiaji Tanzania wamesema “Mtu akifukuzwa na nchi moja
haimaanishi kwamba haruhusiwi kuingia nchi nyingine. Kama jirani zetu
wangekuwa na ushirikiano na sisi baada ya kumkata mtu,wangetupa taarifa
ili anapoingia Tanzania tunakuwa makini naye. Huyo mtu alipita tu hapa
Tanzania”. So, haijulikani kama mtu huyo alipita airport ya Julius
Nyerere na hizo dawa au la.
Imeripotiwa na gazeti la Mwananchi Sept 16.