Video Information

Alhamisi mara baada ya Wachezaji kurudi
Klabuni kwao baada ya kuwa kwenye Mechi za Kimataifa na Nchi zao,
Mourinho alikikusanya Kikosi chake chote pamoja na Wachezaji wapya,
Straika Samuel Eto'o na Kiungo Willian, na kuwapa dibaji fupi ili
kuwaweka sawa.
Lakini tayari kuna minong’ono kuhusu
Mourinho ya kutowachezesha baadhi ya Wachezaji na Juan Mata ni mmoja wao
ambae amecheza Dakika 65 tu kwenye Msimu huu licha ya kuwa mmoja wa
Mastaa waliong’ara Msimu uliopita.
Lakini Mourinho amejibu: “Sijui kama
ninaweza kuwafanya wawe na furaha au hapana. Lakini mimi nina furaha kwa
sababu nina Wachezaji wengi wazuri na kama nafanya vizuri au vibaya,
nafanya kwa nia njema tu. Waache wazungumze Uwanjani. Nitaamua ya
Uwanjani tu na si Hadhi, Maneno, Mahojiano, Mawakala, Wazazi au
Marafiki, si Magazetini au Twitter au lolote. Nitaacha Mpira uzungumze!
Na Mpira utaamua!”
Alipohojiwa na Mwanahabari kutoka
Belgium kama Kevin De Bruyne atachezeshwa Mechi 20 Msimu huu, Mourinho
alijibu kwa mkato: “Kama hachezi Mechi 20 ni kwamba hastahili kucheza.
Kama anastahili atacheza tu!”
Kuhusu Mata, Mourinho alifafanua kuwa
Mchezaji huyo hatengwi na atapata Nafasi za kucheza kwani zipo Mechi
nyingi zinazokuja mfululizo.
WENGER AMTETEA JACK WILSHERE NAADA KUPONDWA ENGLAND
Arsène Wenger amemtetea Kiungo wake Jack Wilshere kwamba atakuwa nguzo ya Timu ya Taifa
ya England.

Wilshere alipondwa na Wadau wa England baada ya kucheza ovyo katika Mechi ya Ukraine na England iliyochezwa Jumanne iliyopita.
Wenger amedai Wilshere hayuko fiti kwa Asilimia 100 na hilo linamfanya kipaji chake kisionekana.
Wenger amesema: ”Akiendelea kucheza Mwezi Oktoba na Novemba basi hali yake itarudi kawaida.”
Pia, Wenger alafafanua kuwa Wachezaji
mara nyingi wanashindwa kuonyesha cheche zao wakiwa na Timu za Taifa kwa
sababu ya presha na matarajio makubwa ya Washabiki na Nchi zao.
Wenger alisema: “Wilshere akicheza
Arsenal chini ya kiwango tunamwelewa na kukubali ni leo tu. Lakini
kwenye Timu ya Taifa hilo likitokea kila Mtu anahoji uwezo wake.
Mchezaji anapata shida na presha hiyo. Timu za Taifa zinahitaji Mastaa
wanaoweza kuhimili presha hizo. France tulikuwa nae Zidane. Kabla
alikuwepo Platini. Katika historia ya France, matokeo yalisimama pale
Platini alipoacha kucheza. Yalisimama Zidane alipoacha. Unahitaji Kizazi
kizuri cha Wachezaji lakini unahitaji Mchezaji spesho!”
Wenger anaamini Wilshere anaweza kuwa Mchezaji huyo Spesho kwa England.
DAVID MOYES ATETEA KUTOMCHEZESHA SHINJI KAGAWA

Mmoja wa Wachezaji hao ni Mchezaji wa Japan Shinji Kagawa ambae Msimu huu amecheza Dakika 7 tu akitokea Benchi.
Lakini Bosi huyo wa Mabingwa Manchester
United amesema ni kwamba Kagawa alichelewa kujiunga na wenzake kwa ajili
ya Mazoezi ya kujitayarisha kwa Msimu mpya kwa vile alikuwa na Timu ya
Taifa ya Japan huko Brazil kucheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara
na pia aliporudi Manchester alilazimika kupiga tripu mbili za kwenda
Japan kuichezea Nchi yake Mechi mbili huku kwao.
David Moyes amesema: “Kutocheza kwao ni kwa sababu ya kutokuwepo kwao.”
Vile vile, Moyes alifafanua kuwa
walitaka kumnunua Fulbeki wa kushoto wa Everton Leighton Baines si kwa
sababu ya kumwondoa Patrice Evra.
Alisema: “Tulihitaji Mtu wa kumsaidia.
Msimu una Mechi 60 au 70 na akikosekana Patrice kucheza lazima awepo
Mtu. Ukiichezea Man United Siku zote yupo Mtu anaejitayarisha kuichukua
Jezi yako! Ni juu yako kupigana na kubaki nayo!”