Video Information

Msimamo huo ni wa Jorge Mendes ambae ni
Wakala wa Supastaa Cristiano Ronaldo ambae pia Wateja wake wengine ni
pamoja na Jose Mourinho na Radamel Falcao.
Jorge Mendes vile vile amedai Ronaldo ni Mchezaji aliekamilika kila idara kuliko Lionel Messi.
Hapo Jana, Ronaldo, mwenye Miaka 28,
alisaini Mkataba mpya utakaomweka huko Real Madrid kwa Miaka mitano
zaidi na kumfanya awe ndie Mchezaji anaelipwa juu zaidi kupita yeyote
Duniani.
Akisisitiza kuwa Ronaldo ni Bora kuliko
Muargentina Messi, ambae ametwaa FIFA Ballons d'Or mara 4, na Mbrazil
Neymar, aliejiunga Barca hivi karibuni, Mendes alitamka: “Bila ya
kuwakwaza Messi na Neymar, ukweli ni kuwa Ronaldo ni bora yao na ni
Mchezaji aliekamilika. Lazima umsifie Mchezaji ambae, katika Miaka mine
iliyopita, amefunga Bao katika kila Mechi ya Real Madrid aliyocheza!”
Katika Mechi 203 Ronaldo alizoichezea Real Madrid tangu ahamie hapo Mwaka 2009 kutoka Manchester United amefunga Mabao 203.
Hata hivyo Mendes alikiri kuwa Barcelona
ndio Timu Bora Duniani pale aliposema: “Barcelona ndio Timu Bora katika
historian na ni msingi wa Timu ya Taifa ya Spain! Wachezaji wao wana
nafasi kubwa ya kufunga. Cristiano anachezea Timu ambayo akiwepo
inang’ara asipokuwepo Timu imefifia! Ni ngumu kwake!”