Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

BENK YA WANANCHI MUFINDI KUSOMESHA WATAKAOFANYA VEMA

Views:
Video Information
E84A0840_1dda1.png
Baadhi ya wahitimu darasa la saba Southern Highlands Mafinga
Na Francis Godwin Blogu
BENK ya wananchi wilaya ya Mufindi ( MUCOBA) imwevutiwa na kiwango cha elimu kinachoendelea kutolewa katika shule ya kimataifa ya Southern Highlands Mafinga na kuahidi kutoa kiasi cha Tsh milioni 2.5 kwa ajili ya kuwafuingulia akaunti katika benk hiyo wanafunzi watakaofanya vema katika matokeo ya mtihani huo mwaka huu.
Akitoa ahadi hiyo kwa niaba ya meneja wa MUCOBA mwakilishi wa benk hiyo Ben Mahenge jana alisema kuwa moja kati ya sababu iliyopelekea benk yake kujitokeza kuunga mkono jitihada za shule hiyo ni kutokana na ufaulu mzuri wa mitihani ya Taifa ya darasa la saba ambayo shule hiyo imeendelea kuongoza na hivyo kutoa heshima kwa wilaya ya Mufindi na mkoa wa Iringa kwa ujumla .(P.T)
Kwani alisema kuwa mbali ya benk hiyo kuendelea kutoa mikopo mbali mbali ila imekuwa karibu zaidi na shule hiyo ya Southern Highlands Mafinga ambapo mkurugenzi wake Bi Mary A. Mungai ni mmoja kati ya wateja wakubwa wa benk hiyo kutokana na wazazi wote wanaosomesha watoto katika shule hiyo kulipia ada kupitia benk hiyo hivyo kiasi hicho cha fedha kilichotolewa na MUCOBA ni kutambua mchango wa shule hiyo katika uendelezaji wa benk hiyo.
" Kati ya wateja wakubwa wa benk ya MUCOBA ni pamoja na shule ya Southern Highlands Mafinga ambapo wazazi wa watoto wanaosomesha hapo hulipa ada kupitia benk yetu .....hivyo kwa ajili ya kumpongeza mkurugenzi wa shule hiyo kwa kuzidi kuiunga mkono benk yetu bado tunazidi kuwahamasisha wananchi wa wilaya ya Mufindi na nje ya mkoa wa Iringa kujiunga nasi"
k_2d4d4.png
Mahenge alisema kuwa benk hiyo imeendelea kutoa mikopo mbali mbali kwa wateja wake ikiwemo mikopo ya ujenzi wa nyumba bora , ujasiliamali na mikopo ya kuendeshea biashara .
Hata hivyo Mahenge alisema kuwa wanafunzi watakaonufaika na msaada huo ni yule atakayefanya vizuri katika matokeo ya mtihami wa Taifa wa darasa la saba pamoja na mwanafunzi Aida Mhagama ambae aliibuka mshindi wa jumla katika masomo mbali mbali na kupongezwa wakati wa mahafali ya darasa la saba ya shule hiyo .
Alisema fedha hizo zitaingizwa katika akaunti zao baada ya kufunguliwa na benk hiyo kwa lengo la kusaidia kuwasomesha elimu ya sekondari pindi watakaojiunga na elimu hiyo ya sekondari mapema mwakani .
Mkurugenzi mtendaji wa Southern Highlands Mafinga Bi Mary Mungai akishukuru kwa msaada alisema kuwa msaada huo wa MUCOBA ni heshima kubwa kwa shule yake na kuwa ni chachu ya shule hiyo kuendelea kufanya vema zaidi ili kuwavuta wahisani wa ndani na nje kuendelea kuiunga mkono shule hiyo.
Bi Mungai alisema MUCOBA hawajakosea kuunga mkono jitihada za elimu katika shule hiyo kwani kweli ni shule inayotoa elimu bora na toka ilipoanzishwa zaidi ya miaka 13 iliyopita shule hiyo haijapata kufelisha mwanafunzi hata mmoja.www.sayariblog.blogspot.com
Similar Videos