Matangazo

ZILIZO KUPITA HIZI HAPA.

Bongo Flava ni sawa na mtoto anayelelewa na mama peke yake

WALICHO KIANDIKA CHADEMA KATIKA MTANDAO WA KIJAMII FACEBOOK

Views:
Video Information
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC) imekataa kupitisha ripoti ya hesabu ya mwaka 2011/12 za Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kutokana na kujaa dosari ikiwamo matumizi ya Sh. bilioni 9 kwa ajili ya kulipana posho za vikao vya mabaraza ya wafanyakazi.
Akizungumza jana na watendaji wa mamlaka hiyo walioambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari, Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe, alisema kuwa kamati imeikataa ripoti hiyo na wanamuandikia barua Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh ili kufanya ukaguzi maalum katika maeneo yaliyobainika kuwa na kasoro.
Filikunjombe alisema kuwa CAG atalazimika kupitia upya maeneo hayo ambayo hesabu zake zinautata ikiwamo matumizi ya Sh. bilioni 6.2 yaliyofanywa na mamlaka hiyo kwa ajili ya kugharamia matangazo.
Alisema kuwa taarifa za matangazo hayo zinaonekana tofauti katika ripoti hiyo wakati ni kitu kimoja.
“Unaposema katika ripoti umefanya publicity na advertisement (matangazo) kwa gharama tofauti hapo unamaanisha nini, hicho si ni kitu kimoja jamani au nakosea,” alihoji.
Alisema kuwa Utouh anatakiwa kufanya ukaguzi pia katika eneo la safari za watendaji wa mamlaka hiyo ambao wametumia Sh. bilioni 10 kwa ajili ya posho za safari pekee.
Filikunjombe aliwataka watendaji hao kuwa wazi kama matumizi hayo yanahusisha wizara ya uchukuzi. “Labda mkurugenzi utueleze kama fedha hizo zinagharamia na watu wa wizara yenu ...maana kuna maeneo mengine tumepata malalamiko hayo ya mamlaka kuombwa fedha,” alisema.
Alisema kuwa katika ripoti hiyo kwa mara nne mfululizo imeonyesha jinsi mamlaka hiyo inavyoshindwa kuzingatia manunuzi ya umma hatua iliyosababisha kufanya manunuzi yao kiholela ya kununua vifaa vya Sh. bilioni 30 bila kibali.
Filikunjombe ambaye ni Mbunge wa Ludewa (CCM), alisema kuwa mamlaka imetumia Sh. bilioni 3.2 kwa ajili ya kulipa matibabu ya wafanyakazi na kutaka kuanzia sasa mamlaka hiyo ijiunge na Mfuko wa Bima ya Afya ili kuepuka upotevu wa fedha za serikali.
“Yaani kuna wizi unaofanyika huwezi kusema umejaza magari mafuta ya lita 100 ni gari lipi hilo lazima tuangalie hilo na CAG afanye ukaguzi upya na tutakutana nanyi Desemba, mwaka huu,” alisema.
Similar Videos