Video Information
JAMES Hussein(kushoto fulana ya kijani), mkazi wa Kimara, Dar alikuwa
na wakati mgumu wa kukwepa kamera zilizotua Mahakama ya Wilaya Ilala,
jijini Dar juzi baada ya kufikishwa kwa kosa la kujifanya trafiki. Tukio
hilo lilijiri mahakamani hapo Agosti 22, mwaka huu ambapo mshitakiwa
alikana mashitaka mbele ya Hakimu Mfawidhi, Joyce Minde. Trafiki feki
huyo alitumia muda mwingi kujificha sura ili kamera zisimchukue lakini
alichemsha kwani kila alipojifunua kidogo alikuta kamera ziko mbele
yake. Hali hiyo ilimfanya mshitakiwa huyo aamue kujiachia kwa kutoa
kofia aina ya kapelo kichwani na picha za kumwaga kupatikana. Akisoma
mashitaka hayo, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Nassoro Katuga alisema
mnamo Agosti 14, 2013, huko Tabata Kinyerezi Mnara wa Voda, Dar,
mtuhumiwa alikutwa amevaa nguo za askari wa usalama barabarani
akijifanya ni mwajiriwa wa jeshi la polisi jambo ambalo ni kinyume cha
sheria. Hata hivyo, mshitakiwa alipelekwa rumande Segerea, hadi Septemba
5, 2013 baada ya kukosa wadhamini wawili kwa shilingi milioni kumi na
nne.VIOJA VYA TRAFIKI FEKI MBELE YA HAKIMU MFAWIDHI -ILALA....
Views: