Video Information
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Faustini Shilogile akitoa taarifa kuhusu
maadhimisho ya miaka 94 ya Jeshi la Polisi Nchini iliyoadhimishwa
jana.Ambapo Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro walifanya usafi
kwenye Kambi ya kulea wazee na wasiojiweza ya Funga funga na Kutoa
msaada kwa wazee hao pamoja na watoto yatima wa kituo cha Mgolole.
Mwenyeki
wa wazee akitoa Neno la shukrani wakati wa ugeni huo wa polisi
walivyotembelea kambi yao ya wazee na wasiojiweza wa funga funga Mkoa
Morogoro
Bibi aliyekuwa kwenye kambi ya wazee wa Funga funga anakadiriwa kuwa na miaka 105.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Faustini Shilogile akiwa Na Mkuu
wa Upelelezi Mkoa wa Morogoro Japhet Kibona wakifanya usafi katika
kambi ya kulea wazee na wasiojiweza ya Funga funga
Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro wakishirikian kufanya Usafi katika kambi ya wazee hao
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Faustini Shilogile Akikabidhi
Sehemu ya Misaada kwa Mlezi wa Kituo hicho Mtawa Felista Mwinuka.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Faustini Shilogile akiwa amembeba
Mmoja wa watoto yatima walio katika kituo cha kulea watoto yatima cha
mgolole. Picha Na MATUKIO NA MICHAPO BLOG